Kwa silinde mbunge wa mbozi(tunguma kwa wajanja)

FUNGO jr

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
252
22
Kweli kwa sasa tunduma ni chadema ccm ilisha kufa na ikazikwa. Swali langu kwa mbunge wangu elenest silinde(without prejudice) tujidaie nini na wewe? Swala la maji tunduma ni kero kubwa na mikakati ya kuleta maji inaendaje ingawa ccm walokaa kwa zaid ya miaka hamsini(50) walishindwa kabisa lakini sikuforce wewe ndani ya miaka 3. Ukitatua swala la maji utakuwa shujaa tunduma. Tunakuomba utuoneshe mikakati gani ipo ya kuleta maji tunduma
 
2naanza na wewe muanzsha mama unaushaur gan

ushauri wangu ambayo ni mawazo yangu tu yanaweza yakawa mazuri au mabaya. nikianza swala la visima, visima vilivyopo ni finyu na havitoshelezi na vya kienyeji sana kwa hi yo tuige mfano mzuri wa visima ni kile alicho chimba mchina maeneo ya nyerere vikiwa ishirini angalau tunaweza kushusha pumzi kidogo. pia maji ya pipeline hayajashindikana.
 
Mbozi magharibi inachangamoto nyingi sana,hiyo tunduma unayosema ina taabu yamaji ni 'half london' ukilinganisha na Tarafa ya MSANGANO ndani ya jimbo hilohilo,lakini ukweli ni kuwa katika tarafa hii kuna mto mkubwa sana (Nkana) usiokauka wenye maji ya kutosha kwa kilimo na matumizi ya majumbani kwa mwaka mzima!Cha ajabu kwa kipindi chote cha miaka hamsini tangu uhuru angalau enzi za operesheni msogezo ya nyerere ndio watu watu walipata maji, lakini kwa sasa vijiji vyote vilivyo karibu na mto huu havina maji!Najua jaiwezi kuwa rahisi kwa kipindi cha miaka mitano kutatua tatizo la miaka kumi ila nataka nione angalau bidii inafanyika ya kuondoa kero hii!hasa kwa vijiji vya msangano, ntinga, msia, ndalwe na chindi!
 
Jamani lazima tuelewe majukumu ya mbunge ni yapi na tusichanganye mambo. Ingekuwa halmashauri ni ya CHADEMA hapo mbunge angekuwa na nguvu zaidi kwenye ile budget inayoingia jimboni kwake. Kwasasa anachoweza kufanya ni kusimamia kwa ukali zaidi lakini hawezi kubadilisha budget ya halmashauri. msimalaumu Sana Mheshimiwa Silinde kwa kweli anajitahidi sana na suala la maji ya Tunduma linamnyima usingizi
 
Katika wilaya ya mbozi na sasa tunduma iko momba hakuna eneo lenye watu wenye uwezo kifedha km tdm.kwa hiyo siyo vibaya wanatunduma wenyewe mkajipanga mkatumia uwezo wenu wa kifedha.mkaongeza kuchimba visima vingine au mkavuta maji kutoka kwenye mito ya karibu na kuyafikisha hapo tdm. kwani ni kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe.mkitegemea kuletewa maji na mb wenu siyo raisi kupata maji.mkizingatia kuwa mb wenu hana fedha ya kuwachimbia visima.pili ndio kwanza ameanza ubunge sasahivi na ndio ametoka shuleni na anaanza maisha.3 jimbo lote lina mtazama yeye tu.4 mwenye majukum ya kuwaletea maendeleo ni sekali ilioko madarakani.mb ni mpelekaji wa shida za wananchi serekalini.kwa vile tdm ina uchumi mkubwa inamaana hata mapato yanayo kwenda serekalini ni makubwa hivyo mb anacho weza kufanya hapa ni kuishawishi serekali iwarudishie sehemu ya mapato ili ya tumike kwenye maji.lingine ninyi wenyewe tumieni sehemu ya fedha zenu kujiletea maendeleo tdm ni yenu.mbona munaweza.
 
huu mto nkana unatakiwa ufanyiwe kazi na kuleta manufaa ya wanatunduma
 
Back
Top Bottom