Kwa siku unakula sh ngapii???

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
Habari
Nina kawaida ya kula nje,nimejitahidi kujibana
Breakfast. 2000
Lunch. 3500
Dinner. 2000
Maji/drinks 2500
Jumla ni alfu kumi
Sasa wadau naomba tupeana maujanja namna ya kubana matumizi hata ikibidi kupika niko teyari lakini vyakula viwe simple maana si mjuzi wa kupika na tufundishane kupika maana hiyo alfu kumi inaniharibia sana bajeti yanngu nashindwa kumudu vitu vingine...nawasilisha
 
Weka wazi wewe mchana unakuwa wapi, kama ni mfanyakazi sio rahisi upate breakfast na lunch nyumbani hata ukianza kujipipikia utapata nafuu jioni tu na week'nds.
 
Weka wazi wewe mchana unakuwa wapi, kama ni mfanyakazi sio rahisi upate breakfast na lunch nyumbani hata ukianza kujipipikia utapata nafuu jioni tu na week'nds.
Mchana ninakuwa nyumbani, kwa sababu niko na pikipiki na ninapofanyia kazi ni karibu na ninapokaa
 
Kama kipatu kinaruhusu ni poa tu, elfu 10 kwa siku sio nyingi sana coz kuna watu wanakula 50 kwa siku.

ila ni vizuri ukawa unapika home msosi unao upenda, kama hujui kupika mwambie wa ubavu wako mtarajiwa akufundishe, lakini swala la kula nyumbani inabidi uwe na kiasi maana ukipitiliza unaweza jikuta kila siku unakula kilo 1 ya nyama na garama zikazidi za kula nje.

ni hayo tu
 
Nakula laki tatu,
Chai Home
lunch Home
Dinner Bar( Nyama) 30,000/= tshs
bia 230,000/= za kitanzania
 
We nae bana msimbazi moja tu unapiga kelele ungekuwa unakunywa na ka valuu na konyagi ingekuwaje.

Pole nitakufundisha kupika tuwasiliane
 
jitahidi kujipikilisha.
nunua maandazi ukanywee chai kazini.
mchana piga desh
usiku nunua mihogo ya kuchoma
hapo utakula buku kwa siku
 
Kama unakula 3500 mchana, usiku unakuwa na njaa ya kula tena 2000 kweli, any way, nunua unga, mchele, mafuta weka ndani ni rahisi kutafuta mboga, hata kama ni dagaa!!
 
asubuhi kikombe cha chai ya rangi - shs. 200/-

mchana ndizi mbivu 2 au embe moja shs. 500/=

ugali (dona) unabadilisha mboga - mchicha, matembele, samaki wa kukaanga [hapa unakula nyumbani]

utakula less than 2,000/= na afya tele - hupati kisukari wala pressure

ngozi itakuwa nzuri na hupati kitambi

:poa:poa
 
Then matumizi mabovu kama hayo halafu unaandamana kuwa maisha magumu? haya ndio maajabu ya mussa. Dogo acha kuiga vitu, fanya kadri ya uwezo wako. Kinachokuhangaisha ni kutaka kuonekana saaaana acha ujinga huo. bila hata kuambiwa na mtu unajua jinsi ya kupunguza matumizi
 
Au ukitaka kufata formula yangu
chai desh
mchana msosi wa buku 2
ucku home

kwahiyo kwa mwezi max ni elf 50
 
Unataka kuniambia katika kipato chako, tshs 300,000 inahusika na kula ww wenyewe!! Unataka kubana matumizi kwa sababu gani, ili iweje?
 
Habari
Nina kawaida ya kula nje,nimejitahidi kujibana
Breakfast. 2000
Lunch. 3500
Dinner. 2000
Maji/drinks 2500
Jumla ni alfu kumi
Sasa wadau naomba tupeana maujanja namna ya kubana matumizi hata ikibidi kupika niko teyari lakini vyakula viwe simple maana si mjuzi wa kupika na tufundishane kupika maana hiyo alfu kumi inaniharibia sana bajeti yanngu nashindwa kumudu vitu vingine...nawasilisha

una umri gani mkuu?? mbona hesabu haiko realistic? what about other dependants siku za wikendi, siku za kazi etc?
 
Unataka kuniambia katika kipato chako, tshs 300,000 inahusika na kula ww wenyewe!! Unataka kubana matumizi kwa sababu gani, ili iweje?

Labda anataka kudunduliza ili aowe maana atakuwa amechoka kukamata kamata ovyo, kama unavyojua babu kisha toa onyo dawa ni mara moja tu.
 
Asubuhi: Nunua mikate/maandazi jioni, asubuhi tayarisha chai yako nyumbani.
Mchana: Kama ulivyosema unakula nyumbani, tayarisha msosi wako nyumbani (ubwabwa, ugali, mihogo, ndizi, viazi), badilisha mboga mara moja kwa wiki. (mboga za majani, samaki, kuku, ngombe). Ikiwa hukuathiriwa na Tanesco unaweza kuweka mboga yako kwenye jokofu. Pia unaweza kupika siku moja ukala siku mbili au tatu. Kazi yako kupasha moto tu.
Usiku: Tayarisha cha mchana cha kutosha ili kinachobaki kikufae usiku.

Ukifanya haya unaweza kupunguza kwa nusu au angalau robo ya matumizi yako
 
Nyie Acheni mamo ya kujibana, hasa kina kaka(sie) mghh unajibana kula mpaka unakula kwa jirani ,
Siku unajikuta umekula buku3 afu Hadija unampa buku 10? so umejibana au unajiua?
Kula we jilie tuuu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom