Kwa Pombe Mkapa Anatisha

Mkuu unaua!!!!!! Hata hivyo umekamilisha siku yangu!!!
Hili la mzee wa kokoto kupanga baraza la mawaziri la mkwere liko hewani siku nyingi na linaonekana kuwa na vinasaba vya ukweli. Inaweza kuwa ndiyo maana mkwere hajawapeleka ngurudoto kula bata?


 
Pombe ni bonge la waziri.

Mandela Road panachimbika.

Inapigwa lami kama ile ya Nyerere Road wanakopita mafisadi na misafara.

Sambamba na hilo, nguzo za taa mpya za barabarani (kama zile za Sam Nujoma zinasimikwa).

Kubwa zaidi junction ya Tabata na Mandela Road inapigwa taa za kuongozea magari.

Pombe anatisha.

Hii si credit kwa CCM. (CCM majungu tu. Bila Mkapa Pombe na Dr. Mwakyembe wasingepewa wizara moja. Au Mwakyembe asingekuwa NW.)

Ni credit kwa Pombe mwenyewe, na credit kwa Mzee wa 'Kokoto'. Aliyemteua Pombe kuwa waziri wa ujenzi.

Mkwere alikuwa na baraza lake la kupongezana, mzee wa Kokoto akalipangua.
source ?
 
Hapo wanajamii mmegundua chanzo cha tatizo! Hata kama zitajengwa fly overs kwenye kila junction bado foleni zitakuwepo tu. Kwa hali ilivyo sasa ni ndoto kwa Serikali kuhamia Dodoma hivyo nashauri kama wakuu watasikia kilio cha wananchi wake ni kuhamisha baadhi ya maofisi ya Serikali na kuyapeleka nje ya mji. Maeneo kama Kibaha, mkuranga na Bagamoyo yangefaa sana kwenye utekelezaji wa mpango huu
 
Mbona zipo jamani, hamjaziona? ina maana hata ukifumba macho huzioni? ndo hizo hizo hakuna nyingine, ngoja tumalizie sasa mradi wa mabasi yaendayo kasi na treni itokayo mwanza dar kwa masaa! mkwere bana, yaani anadanganya kama anadanganya wajukuu zake hivi!!

ha hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii jamani mbavu zangu ooooooooooooooooooooooooh ahhhhhhhhhhhhhhhh
:teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth::teeth:
 
Mhe Pombe ww unatisha kila kona ukienda ila Mkuu wako pesa hana zimekwenda kwa mafisadi wa dowans na huko kwingineko,hii ina weza kula kwako wananchi tunakutegemea sana kuwa utaboresha miundo mbinu mbovu, sasa kama hela hamna utafanyeje ? wafadhili wanatoa misaada mingi fedha zinaishia mfukoni kwa wachache wanao itafuna Tanzania kama mchwa kila kukicha wanaifanya nchi yetu **** chuma ulete sawa sawa na Mti wa zambarau kila fisadi anachuma akijaza kikapu analala mbele wengine wanapopoa zambalau na mawe, ahadi alizo ahidi Mh hazitekelezeki dream it again hamna kitu hapo kinacho tushangaza Mkuu anakimbilia barabara za juu je za chini zimeisha?ss wananchi sio limbukeni tuna mfahamu vizuri sana huyo mkuu wako ahadi lukuki alizo ahidi wakati wa uchaguzi ni kitanzi kikubwa kwa CCm mwaka 2015 huyu Mh hana huruma Muogopeni mungu jamaani Yatima wanazidi kuongezeka,wajawazito wanakosa dawa wanakufa, huduma kwa jamii mbovu, wanapishana na wenzake angani wana beba Almasi,Dhahabu , pembe za ndovu kwenda ulaya n.k Mh anakuja kutoka ulaya na mradi wa vyandarua ina shangaza sana.
 
Pombe peke yake hawezi kuleta miujiza nchini. Kinachotakiwa ni serikali nzima kufanya kazi kwa style hiyo.
 
Raha mtu hujipa mwenyewe faraghani siku hizi, ilmradi tu huvunji sheria wala kuchuuza nchi yako kwa bei reja reja.

Ni kwamba tu usitembee na muhuri wa Jamhuri yetu ya Tanzania mfukoni ukisubiri wa kunaswa UFISADINI huko ughaibuni.
 
QUOTE=Chimunguru;TUNATAKA FLY OVERS

Flyovers za nini mkubwa? Izo si suluhisho la jams hapo Dar. Mpango mbovu wa jiji na ofisi za serikali kuendelea kung'ang'ania na kujengwa Dar ndio vyanzo vya jams. Wewe angalia asubuhi population yote ya Dar inaelekea Posta na Kariakoo. Jioni wote wanatoka Posta na Kariakoo. Sasa kwa namna iyo jams become inevitable. Pia ofisi za serikali zina magari mengi mno yanayokua chanzo cha jams. Suluhisho la kudumu ni kuhamishia ofisi za serikali Dodoma na kuanzisha ujenzi wa miji mipya yenye sehemu za biashara na ofisi nje ya Posta na Kariakoo. Pia ipigwe marufuku kujenga tena Posta na Kariakoo. Asante.
Hivi unavyolazimisha ofisi ziwe mbalimbali hivyo unajua gharama za uendeshaji wa serikali kama ofisi zikiwa mbali? hivi unajua concept ya CBD? wenzetu walioendelea waliona umuhimu wa kuwa karibu kiutendaji! tatizo letu ni planning na flyovers zitasaidia ila kama serikali inakuwa dar au dodoma ni bora ofisi zikawa karibu sio moja iko Posta nyingine ipo Kibaha! ndo mambo ya Bunge liko Dodoma na serikali ipo dar es salaam gharama zake tunaziona kila siku!
 
Namkubali sana Pombe ila natia shaka jamaa aking'aa JK anaona wivu hachelewi kumbana. Bravo John Pombe Magufuli (Dr) mwingine wa ukweli.
 
QUOTE=Chimunguru;TUNATAKA FLY OVERS

Flyovers za nini mkubwa? Izo si suluhisho la jams hapo Dar. Mpango mbovu wa jiji na ofisi za serikali kuendelea kung'ang'ania na kujengwa Dar ndio vyanzo vya jams. Wewe angalia asubuhi population yote ya Dar inaelekea Posta na Kariakoo. Jioni wote wanatoka Posta na Kariakoo. Sasa kwa namna iyo jams become inevitable. Pia ofisi za serikali zina magari mengi mno yanayokua chanzo cha jams. Suluhisho la kudumu ni kuhamishia ofisi za serikali Dodoma na kuanzisha ujenzi wa miji mipya yenye sehemu za biashara na ofisi nje ya Posta na Kariakoo. Pia ipigwe marufuku kujenga tena Posta na Kariakoo. Asante.

Tumesema haya mara nyingi sana, ahsante kwa kusisitiza. Wizara ya mifugo ina ofisi zake Temeke, je kuna jambo lolote limeharibika kwa ofisi hizo kutokuwepo Posta? Dar es salaam haina magari mengi kama watu wanavyoamini, ni mipango mibovu tu ya sisi waafrika(samahani kwa nitakaowaudhi), suala la ujezi na upangaji wa miji ni la wataalamu na si wanasiasa.
Foleni hazisababishwi na magari mengi bali kutozingatia sheria. Nenda kituo cha urafiki, dala dala zimeziba bara bara na foleni inarudi nyuma hadi kimara! hatuhitaji flyovers tunahitaji : 1. Feeder roads ziimarishwe ili watu wasitumie main road kwa wakati mmoja. 2. Sheria za usalama wa bara barani zizingatiwe na tuwe na askari wanaojua tatizo na sio wanaokamata ili kupata mshiko. 3. Ofisi za serikali zitawanywe ili watu waende mielekeo tofauti, hapa ndipo suala la satelite towns linapoingia.
Nilikuwa Botswana wanamipango mizuri sana ya miji kama nchi zilizoendelea, jambo la kushangaza ukiingia ofisi zao ukazungumza kiswahili kila mmoja atafurahi maana wataalamu wote wamesoma chuo cha Ardhi(zamani), iweje sisi tushindwe kuwatumia wataalaumu wetu kutatua matatizo madogo kama haya! Hili si suala la Rais au waziri mkuu ni suala la waziri husika na Meya wa jiji. Sijui wanajua hili au wapo kwa ajili ya kuvaa majoho na kusherehekea sikukuu za kitaifa. Huu si umasikini wa rasilimali ni umasikini wa kufikiri.
 
QUOTE=Chimunguru;TUNATAKA FLY OVERS

Flyovers za nini mkubwa? Izo si suluhisho la jams hapo Dar. Mpango mbovu wa jiji na ofisi za serikali kuendelea kung'ang'ania na kujengwa Dar ndio vyanzo vya jams. Wewe angalia asubuhi population yote ya Dar inaelekea Posta na Kariakoo. Jioni wote wanatoka Posta na Kariakoo. Sasa kwa namna iyo jams become inevitable. Pia ofisi za serikali zina magari mengi mno yanayokua chanzo cha jams. Suluhisho la kudumu ni kuhamishia ofisi za serikali Dodoma na kuanzisha ujenzi wa miji mipya yenye sehemu za biashara na ofisi nje ya Posta na Kariakoo. Pia ipigwe marufuku kujenga tena Posta na Kariakoo. Asante.

Umesema vizuri lakini umeshindwa kunishawishi kuhusu kutokuwa na Flyovers. Nakupa mfano mrahisi sana hapa, kama unaishi Tegeta kunakuwa na foleni sana asubuhina inasababishwa na matuta yaliyopo shule ya Makongo, ukipita tu hayo matuta brake utashikia hapo Mwenge kwenye taa, ukitoka hapo brake nyingine ni pale kwenye taa TBC makutano na barabara ya shekilango. Ukitoka hapo brake nyingine ni hapo kwenye taa za sayansi, nyingine ni hapo kwenye Taa za Morocco, baada ya hapo taa zenye kero nyingine ni hapo Kenyata drive etc. Mpango wowote lazima uendane na uboreshaji wa barabara na kwa kuanzia makutano yote makubwa yawekwe fylovers, barabara ziongezwe na pia tubuni usafiri wa majini pia, why mtu atoke posta ende tegeta through the same road? hawawezi kuwa na barabara inayopita pembezoni mwa bahari mpk Bagamoyo? Kuna barabra walisema inatakiwa iwekwe lami from Bunju kupitia Kimara mpka Uwanja wa Ndege, hii ingepunguza sana magri katikati ya jii
 
Back
Top Bottom