Kwa nn baadhi ya wanawake wakipata pesa zaidi ya mumewe..........

Sasa hao kama ni hivyo.......huyo jamaa anapumua kwa msaada wa mapafu ya mkewe???????
Au ndo mambo ya "i cant live without you my wife..........................."
wote wanafanya kazi sehemu moja,maybe juu ya yote hawezi kuishi bila mke wake.hata afanyiwe vituko vipi.
 
Sasa hivi tunaishi kama dada na kaka.....................NINA MWEZI SASA TANGU NIPATE!!!!,na alishanitahadharisha kuwa nisijaribu kumwambia swala hilo
Wacha upumbavu wa kutudharirisha Wanaume wewe unaweza kulala kitanda kimoja na Dada yako? wewe hapa inaonekana unaficha ukweli, lakini ukweli unaonekana Mwanamke ndiyo anayeendesha nyumba na siyo wewe, inawezekana ulimpenda huyo Mwanamke kwa sababu ya vitu fulani sasa Target zimefeli unakuja kudanganya watu hapa.

Hainiingii akili mtu una shughuli zako na kipato chako, Dunia ya leo upelekeshwe na Mwanamke kwa viwango hivyo!!...never otherwise wewe ni maliyoo tu na huna pa kwenda na isitoshe hata anayelipa kodi ya nyumba atakuwa ni Mwanamke.

So watoto wa mjini wanasema usimuonee wivu mkeo wakati pesa huna.
 
Runner, Pole kwa hayo yote

Kama hakua hivyo kabla atakua kapata mwalimu anaemdanganya

Lakini kama Wewe hukumfanya awe MKE WAKO kabla, hiyo ndio gharama ya wewe kuacha kukalia kiti cahako cha MUME

Lakufanya ni kuelezana ukweli ili kila mmoja akalie kiti chake ili ndoa iendelee
 
Kwa mimi ambaye namiliki gari/magari tangu mwaka 1997, ninakwambia huyo mke wako hajui lolote kuhusu kumaintain gari, yeye anadhani kuvaa miwani ya juwa na kukoleza lipstic huku yupo kwenye kiyoyozi basi amemaliza!!

Kwa mwanamke Mbumbumbu kama amenunuwa gari na wewe hauna usikubali kujidharirisha, wake up ur mind, maisha yako yasiwe tegemezi kwake kiasi kwamba bila yeye hakuna maisha huko ni kutoitendea haki nafsi yako mwenyewe.

Nijibu kwanza maswali haya hili tufikie conclusion ya kesi yako bila kupoteza muda;
1. What is your source of income?
2. Mnaishi nyumba ya kupanga au mnaishi kwenye nyumba yenu?
3. Mmefunga ndoa kanisani/ msikiti/ serikalini?
4. Je mmejaliwa kupata watoto? kama ndiyo ni wangapi?
5. If u don't mind, unaweza kutaja kabila la mke wako na kabila lako?
6. Je mke wako ana kiwango gani cha Elimu?

Majibu ya hapo juu ndio yatakayoleta conlusion ya haraka katika kesi kama hii ya kwako. sometime i beleive huwa tunacreate wenyewe Timer explode bomb!!

Maswali yaliyoulizwa hapo juu ni muhimu sana kusaidia katika kumwelewa huyo mama. Saikolojia yote ya huyo mama imefichwa kwenye swali namba 5 na 6. Naomba mhusika ayajibu ili tujue tatizo la huyo mama maana ananishangaza kwa ulimbukeni wake.
 
Maswali yaliyoulizwa hapo juu ni muhimu sana kusaidia katika kumwelewa huyo mama. Saikolojia yote ya huyo mama imefichwa kwenye swali namba 5 na 6. Naomba mhusika ayajibu ili tujue tatizo la huyo mama maana ananishangaza kwa ulimbukeni wake.

 
Maswali yaliyoulizwa hapo juu ni muhimu sana kusaidia katika kumwelewa huyo mama. Saikolojia yote ya huyo mama imefichwa kwenye swali namba 5 na 6. Naomba mhusika ayajibu ili tujue tatizo la huyo mama maana ananishangaza kwa ulimbukeni wake.
Yalishajibiwa.........
 
Kwanza Pole ndugu yangu. Lililotokea hapo ni kitu kinachoitwa jeuri ya fedha. Fedha inaposhikwa na mtu asiye hekima inajeuka kuwa madhara kabisa na hili pia ni kwa pande zote (MONEY CHANGE BEHAVIOUR). It seems huyu hajazoea kushika hela, sasa zimempa psychological reaction na nguvu fulani. Badala nguvu hiyo kuitumia kusolve issues nyingine, zimempa empowerment kuwa sawa na wewe. Kama ni mtu wa maombi inabidi usali sana kwa stage kama hii. Pia kama kuna mshauri unaweza kumconsalt amkalishe chini na fanya hivyo kwa haraka maana as time goes it will be even more worse. Na pia usijaribu kabisa kushindana naye, endelea kumpenda kwa sana, hiyo ni dawa tosha kuliko kuanza kuonyesha any negative reaction.
 
Habari wapendwa wa JF, nimekaa nikafikiria sana hili swala nikaona bora niliweke jamvini tupeane mchango. Unakuta umeoa na mwanamke alikuwa anakutegemea kwa kila kitu ingawa kuwa nae anafanyaka kazi, mmeendelea na maisha ya kila siku lakini ikaja ikatokea kuwa mwanamke akapata mkopo ofisini kwao ambao ukiulinganisha na ile niliyokuwa nampatia kiukweli mkopo ni mkubwa kiasi chake, sasa kinachokuja hapa ni kwamba "BAADA YA KUPATA MKOPO AMEKUWA MTU WA NYODO, JEURI, MANENO YA KASHFA NA MAJIVUNO".

Hata nikisema nimuulize lolote atanijibu kwa mkato......na mbaya zaidi sasa hivi tunaishi kama kaka na dada............,na mara ya kwanza alikuwa nawahi sana kurudi nyumbani lakini baada ya hiyo pesa kurudi kwake nyumbani ni saa 3 usiku?......

Naomba wana JF mniambie hapa huwa inakuaje kwenye hili? Maana mimi nimeamua kuwa kimya bila kuzungumza chochote.....mbaya zaidi amekuwa busy na simu anaweza ku-chat hata mpaka saa 6 za usiku, wakati mara ya kwanza mm nikitumiwa sms hata moja saa 3 usiku ilikuwa ugomvi ntaambiwa niwaambie hao watu wasinisumbue nipo na mke wangu.

Lakini leo yeye ndo amekuwa kinara wa kuchat, nikimwabia najibiwa "KILA MTU ANA UHURU WAKE WA SIMU",.........Wapendwa wa JF maneno ninayo mengi sana lakini kwa haya niliyoyatoa naamini mtakuwa mmepata picha halisi............NAWASILISHA

Kaka kuwa mpole kabisa hivyo vijisenti vikiisha atakuwa mdogo kama Piriton.Baadhi yao ndivyo walivyo wakipata wanataka hadi majukumu ya ndani mbadilshane yaani we ufue, upike and so forth...
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom