Kwa njia hii Tutafanikiwa

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,061
5,393
ndugu wanaboard,

Nimekuwa nafikira njia ambayo tutaweza kuwafikia watanzania wengi katika mapigano haya ya fikra, na nikajaribu kuangalia wakati wa ukombozi ni njia gani ambayo ni effective zaidi.

Kwa hakika tukitumia wasanii kufikisha ujumbe ninauhakika tutafainikiwa zaidi. tukumbuke tu mama africa aliyefariki leo hii (miriam Makeba). Breda Facie, ukiangalia kina Bob marley na wengine walitumia music kuendeleza mapambano ya fikra.

Kwa Tanzania proffesor j alianza na ''Ndio mzee'', wagosi nao ''tanga kunani''
lakini tatizo la wasnii wetu wanaangalia fedha zaidi kuliko kuelezea matatizo yaliyoizunguka ili yapate ufumbuzi, hivyo nadhani ni wakati huu wa kuwatumia.

naelewa ni ngumu na gharama kurekodi music kwa Tanzania. lakini kama tukiwa determined tunaweza kusaidia kurecord, nyimbo zenye keleta mapinduzi ya kifikra nchini. Tahadhari kwenye njia hii ni nyimbo zenye mwelekeo wa chama fulani cha kisiasa, badala yake zitengezwe nyimbo zenye kuelezea hali hali ya siasa, uchumi, jamii ni njia mbadala ya kutatua hayo yote.

kazi kubwa tunayoweza kuifanya ni kutengeza mashairi kwa vijana wenye vipaji vya kuimba, hata kama kunamwana JF angependa kutoa single tumsaidie kwa hilo.

mimi niko tayari kuchangia fedha kwa hili na pia kutengeneza atleast 5 sound track- ama beats kwa yeyote anayetaka kurecord. Sijui kuimba lakini I will also try to make one before new year.

naomba michango na samahani kwa kuandika kwa kukosea nipo kwenye haraka kidogo but hope msg yangu imeeleweka
 
Hi Kichakoro,

Wazo zuri lakini unafikiri wasanii wengi watakubali??? Maana inaweza kuwa mwisho wa career yao ikitokea imewagusa mafisadi, serikali ama watu fulani fulani. Pili msanii anaweza kuonekana kaingia kwenye siasa hivyo kupoteza umaarufu na hata soko lake.
 
Back
Top Bottom