Kwa nini watuhumiwa wa ufisadi hawapelekwi mahakamani? au upelelezi bado haujakamilika?

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Nijuavyo mimi nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Je ni sababu zipi zinazoifanya serikali isiwafikishe watuhumiwa wa ufisadi mahakamani? kwani kwenye sheria kuna madaraja?

Mara kadhaa tumeshuhudia watuhumiwa wengi wakiachiwa huru na Polisi kwa kukosa ushahidi wa kuwapeleka mahakamani je hawa watuhumiwa ambao miaka inapita bila kuwafikisha mahakamani? je huku sio kwenda kinyume na haki za binadamu? kwanini wasitendewe haki?

Hizi taasisi zinazojigamba kuwa ni watetezi wa haki za binadamu hili hawalioni? mara kadhaa nimekuwa kinyume na wale wote wanaotuhumu wenzao bila kuwa na ushaidi wa kutosha, sina tatizo kabisa na mtu yeyote kama ushahidi utakuwepo, wasiwasi wangu ni kuwa kama utaratibu huu wa kuamini tetesi utakuwa unaaminiwa kuna baadhi ya watu ambao hawana hatia wakajikuta wanaadhibiwa kwa majungu, hisia au njama zinazosukwa na mahasimu wao.

Ningefurahi sana kama nitaelezwa sababu za watu ambao ni watuhumiwa wa ufisadi kutokufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake ikibidi kama kunafedha walizokwapua za watanzania waagizwe zirejeshwe kama wakina Maranda.
 
Kwani anayewafikisha mahakamani ni nani? Siyo mkurugenzi wa mashtaka?

Tatizo hakuna kipengele kinachomlazimisha kupeleka faili haraka mahakamani hasa pale anaposema kuwa hajakamilisha upelelezi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Hizi mahakama zetu siku hizi ni kwa ajili ya kuwakamata CDM na Viongozi wa Dini!
 
Hao wana mshiko,si rahisi kuwapeleka mahakamani kama wengine wasiokuwa na kitu.Tz hii bwana.
 
Back
Top Bottom