Kwa nini Watanzania hawana ujasiri wa kuwakataa mafisadi waziwazi?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kumekuwa na wimbi kubwa la ufisadi hapa Tanzania,mafisadi hawa wamekuwa wakijificha nyuma ya amani na utulivu wa Watanzania.Wamekuwa wakitumia fedha haramu kuwarubuni wananchi wasichukue hatua,sasa nini kifanyike ili Watanzania wawe na ujasiri wa kuwakataa mafisadi na kuwataka warudishe fedha walizoiba bila kusita na bila kikomo.Yaani kutumia hata nguvu ya umma inapobidi.

Nawasilisha.
 
Ukweli ni kwamba tunao watanzania wachache ambao ni majasiri,walio wengi ni wachumia tumbo.Akitishiwa tu kitumbua chake hana ujasiri na hilo halipo kwa raia/wananchi tu hilo lipo hata kwa viongozi tulionao. Hatuna kiongozi yeyote shujaa. Akina Kaborou walipo gangwa njaa yao walitelekeza vyama vyao huo ni mfano mmoja tu kati ya mingi.
 
Hiki ni kitu ambacho muda wote kinakuja kichwani napofikiria siasa za nyumbani. I have not heard of any peaceful or violent demonstrations abt what happened at bot and other institutions..hamna walio wakali abt the remarks of idrissa rashid..nchi nyingine hawa wafanyakazi wa hizi institutions wangekuwa hawana kazi saizi..there is something about tanzanians. Nadhani tunapenda kupelekeshwa.
It has not sank into the majority of tanzanians heads kwamba SERIKALI IMEAJIRIWA NAO and they not doing us favours when they are providing us with services..nimeshawahi kuona wanakijiji wakimshukuru mmbunge wao kuleta kisima alichopromise miaka 5 iliyopita.
Its clearly psychological...upinzani kama mnaitaka tanzania , you need to answer this question first.
ps: on the other hand juzi london watu wamepigana na mapolisi over climate change, unemployment and the financial crisis..sisi tunazimiwa umeme kimya, central bank ni kama personal bank ya wanasiasa kimya, i can go on and on. :-(
 
Kumekuwa na wimbi kubwa la ufisadi hapa Tanzania,mafisadi hawa wamekuwa wakijificha nyuma ya amani na utulivu wa Watanzania.Wamekuwa wakitumia fedha haramu kuwarubuni wananchi wasichukue hatua,sasa nini kifanyike ili Watanzania wawe na ujasiri wa kuwakataa mafisadi na kuwataka warudishe fedha walizoiba bila kusita na bila kikomo.Yaani kutumia hata nguvu ya umma inapobidi.

Nawasilisha.

Mkuu Mmaroroi heshima mbele.

Hii mada ni nzuri sana tena sana.
Binafsi nimekuwa nikipata shida kujua ni kwanini hawa mafisadi bado wanaendelea kupeta pamoja na ubaradhuli mkubwa waliolitendea taifa letu.
Tunakumbuka jinsi waheshimiwa E Lowasa na Mzee wa vijisenti walivyopokelewa kwa shangwe waliporejea kwenye majimbo yao mara baada ya kujiuzulu kwa kashfa zilizoitia hasara kubwa taifa.

Mawazo yangu nadhani uelewa wa wananchi wengi bado ni mdogo sana kiasi kwamba watawala wetu wanatake advantage ya kufanya mambo watakavyo.
Wanachi wengi wanadhani watawala wamewekwa na mwenyezi mungu na wana haki ya kufanya jambo lolote.

Elimu ya kutosha kwa raia wengi inaweza kuwasaidia wananchi kuwakataa kwa ujasiri viongozi wabadhirifu.Bila elimu ya kutosha tusitegemee kuwa na jamii iliyo tayari kuwakabili kwa ujasiri viongozi mafisadi.

Kitu kingine kinacho punguza au kuondoa ujasiri wa kuwakataa waziwazi mafisadi ni umaskini uliokisiri katika sehemu kubwa ya jamii ya watanzania.
Tukiweza kuondoa umasikini au kupunguza kwa asilimia kubwa nadhani wananchi watakuwa na ujasiri mkubwa wa kuwakataa mafisadi
 
Bila maandamano ya mara kwa mara kushinikiza mambo yafanyike, Tanzania na Africa kwa ujumla zitabakia nyuma nyuma milele. Tumezubaa na kulemaa kwa kuogopa nguvu za dola, dola ambayo imeacha kulinda maslahi yetu na kuzingatia maendeleo yetu kama wanajamii.

Hii topic ni muhimu. Mmaroroi angechelewa kidogo tu, angekuta nimeanzisha thread ya "Nguvu ya Maandamano Tanzania Inahitajika" !!
 
Kumekuwa na wimbi kubwa la ufisadi hapa Tanzania,mafisadi hawa wamekuwa wakijificha nyuma ya amani na utulivu wa Watanzania.Wamekuwa wakitumia fedha haramu kuwarubuni wananchi wasichukue hatua,sasa nini kifanyike ili Watanzania wawe na ujasiri wa kuwakataa mafisadi na kuwataka warudishe fedha walizoiba bila kusita na bila kikomo.Yaani kutumia hata nguvu ya umma inapobidi.

Nawasilisha.

Mkuu umenikumbusha siku moja tulikuwa tunaangalia documentary ya national geographic kuhusu maisha wanyama. Simba mmoja alikuwa anawakimbiza nyumbu zaidi ya 200... katoto kadogoo ka miaka kama mitatu kakauliza "mbona hawamchangii??". Labda hili swali linaweza kutupa mwanga kwanini sisi Watanzania hatuna huo ujasiri ....
 
Macho, kuna hiii pia, ilishawahi kuwekwa hapa JF....

Hakika hata wanyama wanatushinda!!

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=LU8DDYz68kM]YouTube - Battle at Kruger[/ame]
 
Kumekuwa na wimbi kubwa la ufisadi hapa Tanzania,mafisadi hawa wamekuwa wakijificha nyuma ya amani na utulivu wa Watanzania.Wamekuwa wakitumia fedha haramu kuwarubuni wananchi wasichukue hatua,sasa nini kifanyike ili Watanzania wawe na ujasiri wa kuwakataa mafisadi na kuwataka warudishe fedha walizoiba bila kusita na bila kikomo.Yaani kutumia hata nguvu ya umma inapobidi.

Nawasilisha.

Kwa maoni yangu Mafisadi wanawalipa baadhi ya Watanzania wawatee kwa kila hali. Hata hapa jamvini kwetu kama utaona kuna watu wengi wameibuka siku za karibuni kuwatetea mafisadi kwa nguvu zao zote. Hatuna umoja Watanzania maana wengine njaa zao zinawasumbua kiasi cha kuweka maslahi ya nchi pembeni ili kuwatetea mafisadi pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mafisadi hao. Mimi naamini tukishikamana dhidi ya mafisadi basi ni lazima tutawashinda tu pamoja na kutumia mabilioni yao ya kifisadi kuwanunua Watanzania wenye njaa na wasio na mapenzi ya kweli na nchi yetu. Mvunja nchi ni mwanannchi.
 
kazi ipo kaka, watanzania wengi hata watu wa chini kabisa ni mafisadi, Kikwete anawakilisha mafisadi asilimia 8o!
 
Mkuu umenikumbusha siku moja tulikuwa tunaangalia documentary ya national geographic kuhusu maisha wanyama. Simba mmoja alikuwa anawakimbiza nyumbu zaidi ya 200... katoto kadogoo ka miaka kama mitatu kakauliza "mbona hawamchangii??". Labda hili swali linaweza kutupa mwanga kwanini sisi Watanzania hatuna huo ujasiri ....
Mafisadi wanatumia mbinu ya 'divide and rule' lakini kama tulivyowashinda wakoloni weupe,ujasiri uleule unahitajika kuwashinda hawa wakoloni weusi.Wana JF tuendelee kuelimisha juu ya ujasiri wa kudai haki,kama ambavyo imeanza na jarida la CHECHE na nyingine.Wapalestina wasingeanzisha kujitoa mhanga Waisraeli wangefuta Taifa lao.Kadhalika Kenya,Zimbabwe,Madagasca na sehemu zingine.Ijulikane tu kuwa wakati mwingine unaweza usifaidi matunda ya ushujaa wako bali watafaidi wengine baada ya wewe kudhurika.Chukulia minazi na maembe tunafaidi sasa lakini waliotesha wengine.Tuchukue hatua sasa tusiendelee kuwaachia mafisadi/wasanii kuihujumu nchi yetu.
 
"Hiki ni kitu ambacho muda wote kinakuja kichwani napofikiria siasa za nyumbani. I have not heard of any peaceful or violent demonstrations abt what happened at bot and other institutions..hamna walio wakali abt the remarks of idrissa rashid..nchi nyingine hawa wafanyakazi wa hizi institutions wangekuwa hawana kazi saizi..there is something about tanzanians. Nadhani tunapenda kupelekeshwa.
It has not sank into the majority of tanzanians heads kwamba SERIKALI IMEAJIRIWA NAO and they not doing us favours when they are providing us with services..nimeshawahi kuona wanakijiji wakimshukuru mmbunge wao kuleta kisima alichopromise miaka 5 iliyopita......"

*************************

Kapinga: Ni kweli kabisa. Akina Lipumba ambao tulitegemea wahamasishe maandamano kabambe dhidi ya mafisadi, badala yake wanasapoti mafisadi -- kama vile kupigia debe mitambo ya umeme ya mafisadi inunuliwe na serikali.

Hali kadhalika mrema, Mtikila na wengine. lakini mimi bado nina imani kubwa ndani ya moyo wangu kwamba hali hii itakuja kubadilika ghafla, tena kwa njia ya ajabu na pengine ya kutisha -- kwa sababu njia za kitulivu zinashindikana.
 
Wanaoweza kupigana na ufisadi ama wanaelewa vita ni ngumu kiasi gani, kiasi cha kugwaya, ama wananunuliwa na mafisadi.

Wasioweza kupigana na ufisadi (kwa kutokuwa katika nafasi zitakazowapa wigo mzuri wa kufanya shambulio la maana) ndio wanaoendesha mapambano, ambayo kwa kiasi kikubwa hayako effective.

Katika hao wasioweza kupigana na ufisadi, lakini wenye nia na upeo, baadhi yao huenda kupata nafasi za kuwawezesha kupigana na ufisadi vizuri, lakini wanafikia ama kugwaya kwa kuhofia mtandao mkubwa wa ufisadi, kujidanganya kwamba wanaweza kuupiga vita ufisadi kutoka ndani ya ufisadi -na kujikuta wanazama katika bahari ya ufisadi polepole- au wanajikuta wakiamini katika itikadi ya "tatizo hili ni kubwa sana na mimi peke yangu suilimalizi" kwa hiyo walio na chembe ya uadilifu kidogo wanafumbia macho ufisadi bila kushiriki, wengine wanashindwa kishawishi na kuchukua mlungula.

Wanakubali msemo wa Marijani Rajabu.

Kula ugali wako ukalaleee.

Ninayo mifano miiingi sana.

Sikia mambo..
 
usiseme kwa nini watanzania wana sema kwa nini watanzania tuna...ina maana umejitoa wewe kuwa si mtanzania?...
 
Watanzania chini ya CCM ndivyo tulivyo. Labda Watanzania watakaokua chini ya utawala wa chama kingine -- na hili linawezekana kabisa.
 
Back
Top Bottom