Kwa nini wanawake wanapenda sana kutikisa kiberiti?

demokrasia

Member
Apr 6, 2011
52
5
Mimi ni mwanaume nina mpenzi wangu ambaye anapenda sana kutishia kuniacha kila inapotokea ugomvi kidogo tu. Mara nyingi nimekuwa nikijitahidi sana kuomba msamaha hata kama kosa ni la kwake, ili tu mambo yaishe tusonge mbele. Wiki moja iliyopita kama kawaida yake amenitishia kuniacha na akaniambia kuwa niache kumpigia simu ili nimsahau. Lakini safari hii sijataka tena kuomba msamaha, badala yake nimemwambia kuwa ok waweza kwenda, nitapata mpenzi mwingine. Zikapita siku nne sijamtafuta, ghafla yeye kaanza kunitafuta na kuniomba nimsamehe kwa maneno aliyoniambia. Wana JF naombeni mawazo yenu, hii maana yake ni nini?
 
Hapo umemuonyesha umekomaa sasa!
Pia Demokrasia ndugu yangu, huitaji kuwa hivyo kwenye mapenzi....
Kabla hujachanganua kuhusu hicho "kutingisha kibiriti" cha maana kwako ni furaha pia una haki ya kupokea pendo!
So kikubwa jihoji mwenyewe je unapendwa... kuhusu kupenda sina wasi hadi kupost hii thread ni unampenda huyo binti!
Kuwa free n' fair katika mahusiano yote......
 
Msamehe ameshagundua sio kila siku jpili,baadhi yetu ndio tulivyo kila utakachotuzoesha inakuwa hivyo hivyo,cha msingi badili huo utaratibu na uonyeshe uanaume wako na sio kuomba omba msamaha hovyo,ungechelewa tu angekusumbua sana huko mbele ya safari!
 
kiukweli tunapendaga kubembelezwa!ni ka mchezo tu ako! kama ilivyo kidalii poo!
kubembelezwa ni haki yenu,na hako kamchezo ka kutishiwa eti ntakuacha_ni kwamba mnakua mmejua udhaifu wa huyo mwanaume,...wengine hatutishiwi nyau kamwe,...mna watu wenu wa kuwatishia kuwaacha,.....swaga poa ila sio eti ntakuacha.
 
Msamehe ameshagundua sio kila siku jpili,baadhi yetu ndio tulivyo kila utakachotuzoesha inakuwa hivyo hivyo,cha msingi badili huo utaratibu na uonyeshe uanaume wako na sio kuomba omba msamaha hovyo,ungechelewa tu angekusumbua sana huko mbele ya safari!
well said da Canta.....
 
Mimi ni mwanaume nina mpenzi wangu ambaye anapenda sana kutishia kuniacha kila inapotokea ugomvi kidogo tu. Mara nyingi nimekuwa nikijitahidi sana kuomba msamaha hata kama kosa ni la kwake, ili tu mambo yaishe tusonge mbele. Wiki moja iliyopita kama kawaida yake amenitishia kuniacha na akaniambia kuwa niache kumpigia simu ili nimsahau. Lakini safari hii sijataka tena kuomba msamaha, badala yake nimemwambia kuwa ok waweza kwenda, nitapata mpenzi mwingine. Zikapita siku nne sijamtafuta, ghafla yeye kaanza kunitafuta na kuniomba nimsamehe kwa maneno aliyoniambia. Wana JF naombeni mawazo yenu, hii maana yake ni nini?

Welcome to the club brother. Sasa umeanza kufanana fanana na wazoefu. Bado kuna mengi hujayafahamu kuhusu hawa viumbe na unatakiwa kujifunza zaidi.
 
Huyo ni kichaa nusu, mpe last warning, ameshajua we ni **** kwake while unampenda akikuzingua mtimue and try to find the most suitable chick for you. Asikuchezee mazee kwani wanaotafuta hzo chance wako kibao baab sema kuwajua ndo ishu.
 
Hahahaha! The Boss. wanaume gani sasa wenye uwezo wa kuwasoma wanawake?

trust me.....hakuna mwanaume ambae ni 'bingwa' kwa hawa viumbe....and vice versa....

wazee wetu walisema siku nyingi mno....'ukimchunguza kuku huwezi kumla'.....tafakari....
 
trust me.....hakuna mwanaume ambae ni 'bingwa' kwa hawa viumbe....and vice versa....

wazee wetu walisema siku nyingi mno....'ukimchunguza kuku huwezi kumla'.....tafakari....

Nakubaliana na wewe kuna mzee wangu mmoja ana umri wa miaka 75..

Siku moja ananiambia mpaka nimefika umri huu sijajua wanawake wanaitaji kitu gani katika hii dunia ili watulie...lol
 
kuwa strong wewe ni mwanaume, ukiwa too fair kwa wanawake wanajenga mazoea mabaya ambayo yatakushinda mbeleni
 
Mkuu hawa watu usipokuwa na msimamo wanasumbua ajabu. Amini wanaume na wanawake wametofautiana mambo mengi sana hususani kitabia.
 
ndo maana wanaume wasomi na wenye akili 'hushindwa' sana kuwaelewa wanawake...

Umeona aisee!

wanaendesha maisha kwa artificial behaviour walizosoma kwenye books

mwanamke peleka kama kidume dume atakupenda na kuhadisia wengine

Kwamba huyu mume wangu balaa usimchezee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom