Kwa nini wanawake siku hizi wanaachika mapema?

Uwe mzuri au mbaya,uwe umesoma au hujasoma,ufikishwe kileleni au usifikishwe kama hamna upendo lazima huyo mwenza wako utamchoka tu na mwisho wake mahusiano/ndoa inavunjika mapema

Ndoa za siku ni mashindano, hakuna uvumilivu, kila mtu ana lake hakuna ushirikiano, jino kwa jino, adabu zimepungua kwa wote, mke na mume hawaheshimiani. Kwa upande mwingine nafikiri na ufinyu wa uelewa kiroho haupo.

Watu tunashindwa kuelewa kwamba kila mtu ana tabia zake, ni kiasi cha kukaa chini nakuongea huku mkiangalia wapi mrekebishe. siku hizi watu wanachoka mapema, akishauri mara moja mtu haelekei basi anaanza kufanya mambo tofauti, mwenzi wake akiona nae anajibu pigo mnabaki kuwa mashetani.

Mhh! Huku kutamu,Kama nimashindano inamana mshindi ndo anayetoa talaka( anaye acha).

Uwe mzuri au mbaya,uwe umesoma au hujasoma,ufikishwe kileleni au usifikishwe kama hamna upendo lazima huyo mwenza wako utamchoka tu na mwisho wake mahusiano/ndoa inavunjika mapema

Hapa kidogo tumeelewana mana kama waweza jua Upendo ndo tatiza.nashukuru sana

Tena mi naona wanaume ndo chanzo kuvunjika kwa ndoa, kama unavyosema mwenyewe. Mwanamke anaachwa, sasa kwa nini ninyi mnaacha wake zenu?
:confused2::confused2::glasses-nerdy:
nakuja kukujibu ngoja nimalizie haya mataputapu pamoja na chang'aa:mwaaah::shut-mouth:

Mmonyoko wa maadili, kutomjua mwenyezi Mungu, ujidai kuwa yote yanawezekana bila mwanaume/mwanamke, uvumilivu finyu. Ki ukweli unaweza kuwa na hela, nyumba, magari ukamiliki biashara zote nchi hii, lakini haki ya mke/mme huipati popote, utawazunguka wanaume/wanawake bado utakuwa na uhitaji wa mtu wa kukaa nae.

Mimi zamani nilijiuliza kwa nini wanaume/wanawake wanapenda nyumba ndogo vs vidumu? Ni kwa sababu tu ya tamaa zao si kwamba hawa watu waliozungukana hawapendani? Shetani ana mbinu nyingi sana za kuharibu maisha ya watu, hasa akikuta roho mtatakatifu ameshuka. Wazazi wetu siyo kwamba waliishi mbinguni nao walipitia mambo mengi sana mabaya lakini walibarikiwa kuwa na UVUMILIVU wakijua kwamba hata wakizunguka huku na huko ni yale yale.

Nyie wapenzi wa VIDUMU/NYUMBA NDOGO, nawapa pole sana kwa sababu zaidi ya kudhalilika na kuokota magonjwa, hakuna furaha huko. jenga nyumba, badilishaneni vile mnavyotaka ili kujenga familia bora.

Mungu atutie nguvu. AMEN

Tatizo lao hawapo moja kwa moja ktk mapenz ya dhati kwa wanaume wao! Hovyo sana!

Jamani mimi naona tatizo kubwa ni kwamba hakuna UPENDO WA DHATI kati ya wana ndoa wa siku hizi.Upendo unabeba kila kitu wapendwa,kuanzia huruma,msamaha,uvumilivu,uelewa,kuchukuliana na mengine mengi ya namna hiyo.

Ukiona umeweza kumuacha mume/mke eti ni mwasherati,mlevi nk then ukasikia kapata VVU au kagongwa na gari ukafurahia,jua hukumpenda wewe,otherwise hata kama mmeachana lazima utaendelea kuumia popote utakapoenda kwa kila habari yake inayosikitisha utakayoisikia kama kweli ulimpenda.Je nani wakumsaidia kama si wewe mke/mume?Wewe ndie mlezi wake kwa level hii ya ndoa.

Simaanishi ndoa iwe ndoano,la hasha!Ila busara itumike zaidi.Halafu hebu ongeeni na ndugu,jamaa,marafiki,Kuna ambaye anasema ndoa yake tamu?Je wanaume/wanawake wangapi walioko ndoani wana affairs nje ya ndoa?(japo si wote).Kijana kike/kiume asipokuwa na hulka ya kudumu na affair moja hata akioa/olewa hawezi badilika.

mfumo dume uliokuwapo kwa miongo mingi umewaathiri sana kina mama na hii ilichangiwa na utegemezi waliokuwa nao kipindi cha nyuma,,,kwa sasa kina mama wameelmika wana nafasi sasa wanachokifanya ni kutafuta power ambayo wameikosa kwa miongo mingi..........sasa basi yawezekana wana overdue.....katika hali ya kawaida binadamu akikandamizwa sana pindi atakapo achiwa atataka kuwa mbabe au tofauti sana
kwa mfano
1.africans /americans walibaguliwa sana usa....na sasa wao ni wabaguzi kupita kiasi na wanabagua hata watu wa asili yao I means africans
kwahiyo ndo hivyo ni ubinadamu

Simbamwene una akili, hongera kwa ufahamu ulio nao juu mwanamke na dunia tulio nayo sasa.

Ukweli ni kwamba matatizo mengi ya wanawake tumeyatengeneza sisi wanaume, mwanamke ukitaka kumbadilisha atabadilika na kukuheshimu tu, tatizo letu tunataka kuujenga mji kwa siku moja, mwanamke ni kama karatasi nyeupe unachokiandika kitakaa mradi utumike upendo kueleweshana, tujaribu tu kuchukulia uzito wa mtu kuamua kuachana na familia yake anaamua kujakuishi kwako na hajui kama una matatizo gani ya kurithi! Hii pekee ni hatua kubwa sana inayotupelekea kuwahurumia na kuwaheshimu wanawake. Naamini siku ya mwisho hilo pekee litatufanya wanaume wengi sana kwenda jehanam. Tufikiri kwa kina kuhusu hili, mimi nikikumbuka hata kama mke wangu kanikosea kiasi gani huwa narudi chini na kumwomba msamaha. Pia ujue mimi siyo wa zamani kivile 32yrs

Wanawake wa karne hii sio wale wa zama za mama zetu ( Digital age Vs Analogue) ni wasomi, wana uelewa mkubwa ( Upeo wa kufikiri na kutafakari mambo mbali mbali) ni watafutaji wazuri wa maisha, wanajituma na mwishi wanajua mbinu nyingi kupambana na mfumo dume. Hivyo ni lazima Wanaume tuishi na kinamama kwa nidhamu na kuheshimiana na kushauriana, kutambua kama mke ni mwenzi wako katika maisha wala si mtumwa wako.

Kwa kauli hizi mimi nahisi nawewe una mfumo jike!!. Samahani mkuu kama nimekukwaza lakini! ( Ingekuwa heri utupe experience ya ndoa yako ilivyo ili uwe role model wa ndoa za wale wasiozingatia uliyoyahainisha hapa)

ukweli ni kwamba matatizo mengi ya wanawake tumeyatengeneza sisi wanaume, mwanamke ukitaka kumbadilisha atabadilika na kukuheshimu tu, tatizo letu tunataka kuujenga mji kwa siku moja, mwanamke ni kama karatasi nyeupe unachokiandika kitakaa mradi utumike upendo kueleweshana, tujaribu tu kuchukulia uzito wa mtu kuamua kuachana na familia yake anaamua kujakuishi kwako na hajui kama una matatizo gani ya kurithi! Hii pekee ni hatua kubwa sana inayotupelekea kuwahurumia na kuwaheshimu wanawake. Naamini siku ya mwisho hilo pekee litatufanya wanaume wengi sana kwenda jehanam. Tufikiri kwa kina kuhusu hili, mimi nikikumbuka hata kama mke wangu kanikosea kiasi gani huwa narudi chini na kumwomba msamaha. Pia ujue mimi siyo wa zamani kivile 32yrs

hata mwanamke wako akikukosea unarudi chini na kumuomba msamaha!! Amekukosea au umemkosea??! ( una uhakika sio limbwata hilo bwana mkubwa?) au pengine bado kijana manake miaka 32 sijui ndio umekaa katika ndoa au ndio umri wako?! Sina mengi mkuu!!

Mmonyoko wa maadili, kutomjua mwenyezi Mungu, ujidai kuwa yote yanawezekana bila mwanaume/mwanamke, uvumilivu finyu. Ki ukweli unaweza kuwa na hela, nyumba, magari ukamiliki biashara zote nchi hii, lakini haki ya mke/mme huipati popote, utawazunguka wanaume/wanawake bado utakuwa na uhitaji wa mtu wa kukaa nae.

Mimi zamani nilijiuliza kwa nini wanaume/wanawake wanapenda nyumba ndogo vs vidumu? Ni kwa sababu tu ya tamaa zao si kwamba hawa watu waliozungukana hawapendani? Shetani ana mbinu nyingi sana za kuharibu maisha ya watu, hasa akikuta roho mtatakatifu ameshuka. Wazazi wetu siyo kwamba waliishi mbinguni nao walipitia mambo mengi sana mabaya lakini walibarikiwa kuwa na UVUMILIVU wakijua kwamba hata wakizunguka huku na huko ni yale yale.

Nyie wapenzi wa VIDUMU/NYUMBA NDOGO, nawapa pole sana kwa sababu zaidi ya kudhalilika na kuokota magonjwa, hakuna furaha huko. jenga nyumba, badilishaneni vile mnavyotaka ili kujenga familia bora.

Mungu atutie nguvu. AMEN

Je wewe unayaishi haya au unahubili wengine? (ore wao watwishao wenzao mizigo mizito amabyo wao hawataki hata kuigusa kwa ncha za vidole vyao.)

Haya jamani zungukeniiii zungumzeniii jadiliniiiii mwisho wa siku mtapata jibu langu nililoleta kwenye post yangu mkanipinga!

Katika ndoa nani anayeachika?fikiria dadaa wacha LIGI

Unaishi dunia gani wewe? Kakuambia nani kuwa katika ndoa wanawake tu ndio huachika? Ushakuwa kwenye ndoa wewe? Kuachika ni yeyote haijalishi ni mwanamke au mwanaume. Inategemea aliyeamua kukatisha uhusiano. Unadhani talaka ni zile za kuandika karatasi?

Back
Top Bottom