Kwa nini wanashindwa kuongea live?

Kwa nini mtu mnakuwa pamoja kila siku, mnazungumza mambo mengi tu, lakini anapotaka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi anakuandikia kadi au sms. Kwa nini watu wanashindwa kuongea live!?

Due to lack of experience

 
No, mwanaume kamili lazima uwe tayari kum-face mwanamke live na kumweleza kilichomo moyoni. Mambo ya kuzungukazunguka yanaumiza moyo bila sababu ya msingi. Wanaoona aibu wanakuwa bado hawajakamilika. Sifa mojawapo ya kiume ni guts, courage, n.k. Kama huna hizo basi kuna jambo siyo la kawaida.

Si unajua mambo ya makuzi tena mkuu
 
wanaume wengi wanaogopa sana kibuti kutoka kwa wanawake wengi inawanyima confo, unakuta mtu anajiuliza hivi huyu amenionaje hadi amenikataa, kwa hiyo wanatumia msg kuangalia upepo unaendaje !
 
ule umri wa aibu aibu ukishavuka hupaswi tena kumwogopa mwanamke,tene anapaswa yeye ndo ale kucha na kuchora chini wakati unamwimbisha,,,,
 
Hivi mara ya mwisho mie kutongozwa ni lini vileeee ....,da sikumbuki .mambo mengine kipaji mkuu la sivyo mtoto wa kiume utaumbuka.mwanamke wa kweli haitaji kutongozwa kwa maneno kibaooo.muandae mwanamke kihisia kujua km anaelekea ulipo.ukiona pozi sio we sepa kabla hujabwagwa kweupeee.usije ukaenda na barua hata km unamtaka denti wa plaimari,utaonekana mshamba.wajanja huwa hawatongozikabla hawajawa na uhakika wa jibu
 
Wengine mpaka wastue kidogo na ze kili ndo wanapata ujasiri wa kuzoza live.
 
Unamface wa nini wakati we shida yako ni kuchapa na kusepa.Labda kama atakuwa mkeo hapo unasema ukweli.UKITAKA KUMUA NYANI USIMWANGALIE USONI.do it then run
 
Jamani kutongoza si kazi rahisi kama mnavyodhani,kuna wanawake hata baada ya kuwa nae kama rafiki lakini si rahisi kuingilika kwa kumtamkia suala la mapenzi ndio maana wanaume wengi huwa wanahofia kuwaambia live,pia kuna mambo ambalo wanaume huogopa kama vile kumpoteza mwanamke yule baada ya kuwa amekataliwa na mwishowe kupoteza urafiki,sasa jambo hilo linapofanyika live huumiza sana wanaume.
Lakini pia inawezekana na tabia,malezi na utaratibu wa mtu wa namna anavyoishi,wengine si waongeaji hivyo hutumia njia mbadala kufanikisha mambo,kila mwanaume ana namna yake ya kutongoza.
 
Nafikiri hapo ni kukosa ujasiri wa kuface reaction,kibuti kinauma ukikiwazia,ila mwanaume kamili anaongea live tena kwa kukuangalia usoni.sio hiyo tu hata kwenye mahusiano ukiona mtu anakuambia kitu halafu hakutazami usoni,mfano anakuambia "nakupenda"then hakuaangalii anza kuhamisha vitu bomu hilo!:mullet:
 
Unapenda kutamkiwa live? Vizuri sana. Ila inaonyesha huwa unamuangalia sana machoni wakati mnaongea

Inaleta raha sana hii maana mwanaume anaonekana shujaa sana kama zamani watu shujaa tu ndio walikuwa wanapata madem sababu lazima ujitose mzimamziam sio siku hizi hata madomo zege nao wanatupa visms vyao wamemaliza, mapenzi yameingiliwa sana siku hizi
 
Back
Top Bottom