Kwa nini waalimu wanadharaulika?

Mbona walimu enzi za Mwalimu walikuwa wanaheshimika sana?
Enzi hizo mwalimu mshahara wake unamtosha kula yeye na wanae nane, mke/mume, wakwe n.k
Hebu angalia sasa hivi kipato cha walimu jinsi kilivyo......wanaishi kama hayawani!
Na dharau inaanzia kwa wakubwa wao serikalini yaani utakuta mfagizi tu kwenye idara ya ualimu eti anamdharau mwalimu!! Hivi kwa hali hii kuna mtu atafanya kazi hii kwa moyo kweli?
 
mishahara wanayolipwa ni kidogo mno na pia bado hawalipwi on time.ndio maana wengine huwa wana focus kufanya biashara ndogo ndogo shuleni badala ya kufundi.

serikali yetu ndio inaongoza kuwadharau walimu.
 
Nadhani wao wenyewe wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kudharauliwa.Naweza kusema wenyewe wanajidharau na wanatoa mwanya wa kudharauliwa.Inatakiwa tufike mahali tuondokewe na haya mawazo tegemezi ya kusubiri mshahara wakati unajua hautoshi kabisa.Na siku zote ujue Pesa inamchango mkubwa wa mtu kuheshimiwa au kudharauliwa.Waache kufanya mambo ya kujidharaulisha.Matatizo walito nayo yawape changamoto ya kujikwamua kiuchumi.Zipo kazi nyingi za kufanya na kuwaongezea kipato bila kuharibu utendaji wao.Ukiisubiri serikali ikuangalie utaishia kulia kila siku mapaka Yesu anarudi.
 
Baba vipi?
Kwanini Benno Ndullu asjitafutie pesa za kukarabati nyumba ya kuishi wakati anamshahara mkubwa unaoweza kuwa mtaji tosha wa kufanyia ujasiliamali? kwanini atumie pesa za umma??
 
Baba vipi?
Kwanini Benno Ndullu asjitafutie pesa za kukarabati nyumba ya kuishi wakati anamshahara mkubwa unaoweza kuwa mtaji tosha wa kufanyia ujasiliamali? kwanini atumie pesa za umma??

Ndio hapo tunapokoseaga.Tutalia na akina Beno ndulu mapaka lini? kwanza wametia pamba masikioni mwao.Kumbuka aliye juu mfuate hukohuko juu........
Inabiidi ifike mahali tubadilike kufikiri kwetu.ngoja nikuulize swali,kwani ukisoma level yoyote ni lazima uajiriwe? ni uoga wetu ndio unaotuponza.Hao waalimu wanadharaulika kwa vile kila mtu anakimbilia hiyo hfani ili apate ajira.Lakini ukiangalia kwa jicho la tofauti kama hao wanaokimbilia kwenye ualimu wangelima mihogo na kuiuza au kufanya biashara nyingine basi kungekuwa na walimu wachache wanaothaminiwa na serikali na wangelipwa vizuri.
Alafu mimi sio baba tafadhali.
 
Back
Top Bottom