Kwa nini viwango vya kubadilisha dollar vinatofatiana kati ya Benki na Benk?

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Wadau,
Leo nilitaka kubadilsha dollar zangu kadhaa ,kwa 100 USD
NMB nimekakuta wanabadilisha kwa sh 1455 ,CRDB 1484,NBC 1488
Hivi ni kwa nini? viwango si sawa?
 
Hii ni kutokana na benki yenyewe inavyotaka 'profit margins' na timing ya soko lenyewe.
Ukiwa na bargaining power kubwa huweza kuapata rate nzuri. Mfano leo nilikuwa nalipa randi ya s/africa, nilipiga barclays wakanambia 1zar=230 tshs, baada ya kubargain wakanipa kwa shs 224.
 
Ni kwa sababu ni biashara kama ilivyo biashara nyingine. mbona bidhaa nyingine zote huuzwa kwa bei tofauti hata kama wauzaji wako sehem moja??? refer to response by Mestod above
 
Hii ni kutokana na benki yenyewe inavyotaka 'profit margins' na timing ya soko lenyewe.
Ukiwa na bargaining power kubwa huweza kuapata rate nzuri. Mfano leo nilikuwa nalipa randi ya s/africa, nilipiga barclays wakanambia 1zar=230 tshs, baada ya kubargain wakanipa kwa shs 224.

Kwa hiyo hakuna control katika hilo harta waisema 1USD wana-charge ka sh 800 ni sawa?
 
Kwa hiyo hakuna control katika hilo harta waisema 1USD wana-charge ka sh 800 ni sawa?

Mfanyabiashara yeyote aim yake ni kupata maradufu ya faida. Rate ya 1$ to 800tshs ni siku nyingi sana. Pamoja na kuwa zinatofautiana haziwezi kwa na tofauti kubwa hivyo. refer kwenye rate ulizopata kwenye bank hapo juu. Kinachokontrol bei ni demand and supply forces, kama watu wengi watataka dola basi bei ya dola itapanda tuu, na kama demand ya dola itashuka basi hata rate yake itakuwa chini.
 
Back
Top Bottom