Kwa nini uteuzi wa wakurugenzi wa bodi unawalenga zaidi wanasiasa wastaafu?

hittler

Member
Jul 18, 2011
55
10
Tanzania ya leo imekumbwa na mfumo siasa, kila kitu siasa, chakula siasa, ushuru siasa,watendaji wa wizara siasa uteuzi wa wakurugenzi siasa hii ina kera sana. Huu mfumo ni wa kibaguzi kwa maana mtu amekaa kwenye siasa takribani miaka 40 anaamua kustaafu kwa idhini yake alafu la kushangaza rais anapekuwa pekuwa majina na kumteua ata kama hafai. Watanzania jiulizeni, hatuna watu ambao wanasifa za kuwa wakurugenzi zaidi ya wanasiasa wastaafu waliokaa kwenye nadhifa mbalimbali za serikali bila kuleta mabadiliko yeyote ya kiuchumi? Hizo ajira kwa vijana zitapatikana vipi kama wazee ndiyo wanaopewa vipau mbele? Naomba mnisaidie kujua hilo
 
Ndio maana hatuendelei! Mtu hata mbinu za kisasa hana halafu unampa ukurugenzi atatoa ushauri upi kama sio kuua shirika?
 
Back
Top Bottom