Kwa nini Ulizaliwa Tanzania?

Haya maswali mengine bana, sababu ni kuwa mzazi wangu alikuwa Tz wakati nazaliwa na sikuwa na choice kwa kuwa sikuwa na uwezo wa kumake choice
 
Urenga one nakushauri usifike hatua ya kujilaumu kwa nini umezaliwa Tanzania. Huko unakotamani kwenda/kuwa inawezakana wana matatizo makubwa ambayo kama ungepata neema ya kufika ungemshukuru Mungu kwa wewe kuwa Mtanzania.

Nimepata neema ya kuwa nje ya africa mara tatu katika nchi mbili na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka kadhaa. Pamoja na kupata neema hiyo bado sijashawishika kuiacha nchi yangu kutokana na changamoto ninazoziona katika nchi hizi nyingine.

Ninafahamu matatizo ni mengi sana ya kijamii na kiuchumi ambayo watanzania tunapitia lakini swali kubwa la kujiuliza tumefanya nini kupambana na hali hii. Japo mimi siyo mwanasiasa na si mwanachama wa chama chochote Naamini mheshimiwa Dr. Slaa ametoa/anatoa mchango mkubwa sana wa kuhakikisha taifa hili linarudi kwenye mwelekeo ulio sahihi. Ninalojiuliza ni kuwa je akina Dr Slaa wengine tuko wapi? Tumechangia nini kuelekea uponyaji na ukombozi wa nchi yetu? Kwa nini tusidhamirie kila mwaka kila mmoja JF aende kijijini au kwenye mtaa wake ahakikishe anahamasisha watu kujiandikisha kupiga kura na wachague watu makini badala ya kudanganywa na kanga pamoja na kofia.

Kumbuka watu wengi wakati wa kampeni tunahudhuria mikutano na tunakuwa na ushabiki ambao tunajadiri maofisini, makanisani, misikitikini, kwenye vijiwe na hapa JF lakini ni asilimia ndogo sana ya hao ambayo inakuwa imejiandikisha kupiga kura na kuchukua hatua ya kwenda kupiga kura siku husika.
 
hoja kama za huyu urenga one ndizo hasa zinazopaswa kuitwa UFISADI!!!!!!!!!!

ndiye anayesababisha tuendelee kuishi na matatizo hapa SWEET HOME (TZ).

jamani tusidanganyane, kwa wale tuliobahatika kuvuka mipaka ya nchi zaidi ya moja katika dunia ya nchi zinazoitwa za ulimwengu wa kwanza, hivi nyie mmewahi kuona nchi nzuri, maishi kwa raha na bashasha kuliko tanzania? kama mmeishaiona niambieni nijaribu kuitembelea siku moja!

long live TZ Mungu ibariki TZ.........................

wasaliti na malimbukeni wote, na wote mnaolilia dual citizenship, mshindwe na mlegee...........................
 
Mimi sina uhakika kama nilizaliwa tanzania,bali ninachojua ni kwamba naishi Tanzania,siri ya wapi nilizaliwa wanajua wazazi,na hata wakinidanganya sintoujua ukweli,vyeti vya kuzaliwa wanapewa hata *********s waliozaliwa Mumbai!!
 
Back
Top Bottom