Kwa nini tunasema "kuota jua" ?

Mahmood

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
7,909
2,477
Ndugu wapendwa,

Mimi ni mswahili lakini mpaka sasa sijafahamu kwa nini tunatumia neno kuota ? kwa

mtu aliejianika juani tunasema "fulani anaota jua" ?

tujadili, nataka kujifunza kiswahili zaidi.
 
Ndugu wapendwa,

Mimi ni mswahili lakini mpaka sasa sijafahamu kwa nini tunatumia neno kuota ? kwa

mtu aliejianika juani tunasema "fulani anaota jua" ?

tujadili, nataka kujifunza kiswahili zaidi.

Mahmoud,

Neno katika lugha linaweza kuwa na maana zaidi ya moja, chukulia "paa"
Ndege inapaa.
Paa la nyumba yetu linavujisha/linavuja.
Tulikwenda kuwinda paa jana lakini hatukubahatika.

Kwa hiyo neno ota liko kama hilo paa. Katika maana yake moja ni kutafuta ujoto.

Wewe umetaja hapa kuota jua. Iko pia kuota moto

Hii link ninayoiweka hapa itakusaidia siku nyengine na katika kujifunza kiswahili kama ulivyosema kwenye mada yako
Ingia hapa, bonyeza, bofya kiungo hiki :-

http://www.kamusiproject.org/en/lookup/sw?q=lookup&Word=ota&EngP=0&pos_restrict=14
 
Nadhani wewe si mswahili wa Lugha fasaha! au wewe ni mswahili wa uongo na Umbeya?! Sorry ni utani!
Mimi ni scientist lakini nakumbuka kiswahili cha Olevel tulijifunza maana ya sentensi tata kwamba kuna maneno yanayoweza tumika zaidi ya mara moja.
Kaa: Kaa chini, Sehemu ya Mkaa, Mdudu wa Baharini!
Maneno kama Meza, nk
 
Ota, lina maana zaidi ya moja kama wataalam hapo juu walivyofafanua.
 
Back
Top Bottom