Kwa nini tume inachelewa kutangaza matokeo Igunga? Vurugu zimeanza

Mimi nilipita Igunga jana. Hali halisi CDm walionekana kushinda....Ila Kama CCCM watachakachuo nawaambia ipo siku yao!
 
Wa Jikoni kanipenyezea data mpya CDM wanaongoza tofauti ya kura 20,000 bado kata 3 ndio wanamalizia kuhesabu!
 
Wale wenye access, watch Channel Ten Now!

Mwandishi wa Channel Ten Tabora, Juma Kapipi ameripoti live kuwa mapanga yameanza kutembea Igunga!.

Kwa mujibu wa Kapipi, vurugu hizo zimeanza pale wafuasi wa Chadema, walipojitokeza mitaani asubuhi hii kujipanga kuivamia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wakidai haki yao ya ushindi.

Katika rabsha hiyo, kundi hilo la wafuasi wa Chadema, waliizingira hoteli waliofikia viongozi wa CCM na kuleta fujo kubwa ikiwepo kutupa mawe na kuvunja vioo gari moja ya Landcruiser Prado. Ndipo kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM, liliibuka kutoka ndani huku wameshika mapanga, na kuwasambaratisha wafuasi hao wa Chadema, ambapo kuona mapanga, kila mmoja alishika njia yake kujiokoa maisha yao!.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofurushwa, waliliripoti tukio hili polisi, na mara polisi na FFU walifika na kuizingira hoteli hiyo, ikiwemo kuingia hotelini humo kuyasaka mapanga hayo, cha ajabu, hakuna hata panga moja lililopatikana!.

Kapipi amesema, maduka yamefungwa, FFU wametanda likiwemo lile gari la maji ya upupu, ila amani imedibitiwa.

Mtangazaji David Ramadhani, aliwatafuta viongozi wa CCM, Chadema na Jeshi la Polisi kuzungumzia hali hiyo.

Mpaka sasa Ch.10 iko hewani Charles Hilila akihojiana na Studio.

Naomba Kuwakilisha.

Pasco.

2vcdboi.gif
....KWA TAARIFA!!
 
mimi sio shabiki wa CCM, mimi ni CCM yenyewe.

Kwa hiyo unaona risasi inawafaa waTanzania siyo? Sawa bwana lakini ukae ukijua hakuna jeshi liliwahi kushinda umma wa wananchi. Hata wewe risasi yaweza kukuhusu ila kwa ushabiki wako hujui tu.
 
Kwa hiyo unaona risasi inawafaa waTanzania siyo? Sawa bwana lakini ukae ukijua hakuna jeshi liliwahi kushinda umma wa wananchi. Hata wewe risasi yaweza kukuhusu ila kwa ushabiki wako hujui tu.
Risasi haiwezi kushinda umma lakini huko Igunga hakuna umma bali ni genge la wahuni wa CDM.
 
mkileta fujo tunapiga risasi tu. Dr. Kikwete alishasema hataki uhuni Igunga.

Aibu!! yani kwa utaratibu huu 2015 Ocampo anatia timu hapa yani kwa vyovyote vile nchi yetu imekwisha!
 
Wa Jikoni kanipenyezea data mpya CDM wanaongoza tofauti ya kura 20,000 bado kata 3 ndio wanamalizia kuhesabu!
Ni sawa tu, sisi CCM tutakubali matokeo na tutawapongeza wana CDM. Je CCM ikishinda watatupongeza au watarusha matusi?
 
Wanachama na wapenzi wa cdm wamekizunguka kituo cha kutangaza matokeo wakiwa ni wengi kwa mamia na kuna askari wengi sana na magari ya washawasha. Wanaimba wimbo wa Mungu bariki cdm. Madai yao ni matokeo yatangazwe kwani muda tayari umepita na uchakachuaji unafanyika.Je matokeo tunayotangaziwa na Nape, Mtanzania, kwamba ccm wameshinda yametoka wapi?

Source Radio 5

Chanzo cha vurugu ni CCM na serikali yake...ngoja tuone!!!
 
Ndugu yangu si ZITTO walaDK SLAA waliothubutu kutoa matokeo hapa JF, DK KIGWANGALA na NAPE ndio wanao tamba humu JF alfajiri hadi asubuhi hii bado ujasoma alama za nyakati?
Hoa wehu, nani aliwaajiri tume ya uchaguzi???ndo mana tunasema tume iwe huru, maana Nape na Kingwa wanahisi tume ni moja ya Departments za CCM ndo mana wanahisi wanapower ya kuropoka utumbo. Muda si mrefu itatafsiriwa kuwa wanalazimisha ushindi, tuishie kuwabatiza makofi. Jibwaaaaaaaaaaaaaaaa weeeeeeeeee!!!!
 
Back
Top Bottom