Kwa nini serikali ya Tanzania haiwapendi wananchi wake?

sarikoki

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
1,194
721
Ni swali ninalojiuliza kila siku lakini sipati jibu,kila siku ya Mungu inayopita watawala wetu wanalala wakiwaza mbinu mpya ya kuzidi kumdidimiza huyu mlalahoi.

Utaniuliza nina ushahidi gani....kama kawaida yetu na mimi nitakuuliza ni lini umesoma magazeti au umesikiliza taarifa ya habari ambayo haina habari ya kummaliza MTanzania? ni lini umesoma sheria mpya inayompa matumaini MTanzania? Ni lini umesikia MTanzania akiifuraia badget ya serikali? ni lini mwekezaji amemnyanyasa MTanzania akachukuliwa hatua?

Watu wananyang'anywa mali zao... wananyang'anywa ardhi zao.... wanafungwa kwa kubambikizwa kesi....wanapigwa risasi kwa kudai haki zao za msingi...wanateswa kwa kuhoji mambo ya msingi..... na kubwa zaidi ni hili linaloendelea sasa hivi hata mafao yao wanataka kuporwa kisiasa.

Nimesoma kuhusu viwanja vya gezaulole nimegundua sasa wanataka kuwa na ngome yao... nafikiri ni ngome ambayo itavitenganisha na kuvilinda vizazi vyao na mlalahoi.

Najiuliza hii amani itaweza kuendelea kweli kwa namna hii?. Kwa nini wanaishi kama vile hamna kufa? Kwa nini wanaifanya Tanzania kua mali yao?

Mungu atusaidie na tuendelee kumuomba Mungu atubariki na atuondoe kwenye hili wingu jeusi.
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa.
 
UJAMBAZI,ULIMBIKIZAJI MALI na ndio maana tunawaponda kila leo iyendayo kwa MUNGU!

(UBINAFSI)
 
Back
Top Bottom