Kwa nini roho huuma?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Jamani msaada, hivi kwa nini ikitokea wapenzi wawili wakiachana, roho huuma sana pale mmoja amwonapo mwenzie ana mpenzi mpya?
 
Kama ulimpenda kwa dhati roho lazima ikuume as she or he was part of you.
 
Jamani msaada, hivi kwa nini ikitokea wapenzi wawili wakiachana, roho huuma sana pale mmoja amwonapo mwenzie ana mpenzi mpya?

Wifu ati, yaani hupendi uliyemuache afanikiwe, akipata mpenzi wewe kiroho razima kikuume vile sasa atakusahau wewe na kuwa karibu zaidi na candidate mpya. Basi hapo wewe ndo utajiona hufaiiii!!!!
 
Lakini pia uliyeachwa utakaa week moja mawazo yanakwisha hamna noma wala nini maana mapenzi siku zote kubali kila kitu mpaka uoe ndio unasema chako.........
 
Roho ni nini? Na ipo wapi?

Au unatumia "roho" kurahisisha mjumuiko mzima wa mawazo?
 
Mimi kukuchinja siwezi.....ngoja ntamwambia chinjachinja.........

...sawa, je huyo ndiyo anayejua kipi kati ya "roho" au "moyo" vinavyo sononeka au kufarijika kutokakana na kughafirika au kuridhika kimapenzi au ndani ya mahusiano?
 
...sawa, je huyo ndiyo anayejua kipi kati ya "roho" au "moyo" vinavyo sononeka au kufarijika kutokakana na kughafirika au kuridhika kimapenzi au ndani ya mahusiano?

No hajui...ila akishakuchinja....wewe ndio utanionyesha mimi au yeye "roho" yako iko wapi....

We si ulinambia nikuchinje utanionyesha?
 
No hajui...ila akishakuchinja....wewe ndio utanionyesha mimi au yeye "roho" yako iko wapi....

We si ulinambia nikuchinje utanionyesha?
goofy.gif

Nyani, kwa hiyo roho ni kitu cha kuaminika tu lakini moyo siyo au vipi... Sasa kwa vile mwanzilishi wa thread ameulizia roho nawe ukasema labda anamaanisha moyo, kwanini sasa huo moyo (physical organ) huuma pale mtu anapogafirika ndani ya mapenzi?! Ni blood pressure au kipi kinachosababisha physical organ kama moyo kuuma kutokana na matatizo ndani ya mapenzi?
 
Bana eeeh mie sijui bana...mbona wataka kunishikia bango....?

Kwanza rudi kule kwenye thread ya Cynth ukamjibu Kuhani.....naona umekimbia baada ya kukamatwa na ile definition ya "groupie"....ahahahahahahaa
 
..Ubinafsi tu ndio tatizo!!!!
Inawezekana ikawa ndio sababu ya msingi kabisa -- Ubinafsi.

Sio kwa wapenzi tu, hata bosi akimfukuza mfanyakazi wake kazi hapendi afanikiwe kupata kazi nzuri zaidi...kwa kifupi mtu anapomwacha mwingine anataka amwone akiteseka ili aseme si mnaona nilivyokua namsaidia?

Roho ni nini? Na ipo wapi?

Au unatumia "roho" kurahisisha mjumuiko mzima wa mawazo?
Nadhani roho sio kitu cha kushikika. Kuumia roho ni hisia tu, kama ilivyo kufurahi, kuhuzunika n.k.
Labda swali hili laweza kueleza kidogo.... unaposema mguu wako, mkono wako, ubongo wako, macho yako, moyo wako, damu yako, mwili wako; kwa hiyo wewe (mmiliki wa vyote) ni nani au uko wapi?
 
Because there is always unfinished business between the two of yu .. kwani sometimes relationships zinakatishwa ghafla na wote mnabaki yearning for something ndo maana .. laiti binadaamu tungekuwa kama chakula .. ukimpata mwenzio unamla mpaka akaisha .. then .. like its closed chapter .. tena after a flash in the toilet ndo kabisa ... unasahau ... situation would have been different my dear .. so midhali bado atakuwa hai akitoka kwako roho bado itakutuma ujue je yukoje after yu .. wengine wakimkuta kadhofu ni furaha tosha ila wengine wakiona kanawiri wivu na visasi vinaanza hapo ...
 
Inaeleweka kama wewe ndiyo umeachwa.Lakini kwanini roho ikuume wakati wewe umemkataa mwenyewe? Kuna kesi zimewahi kutokea ambapo ( na hii hasa ni kwa wanaume) hata mauaji yametokea kisa mtu kakuta mtalaka wake yuko na mtu mwingine.Huo wivu wa nini wakati mlishafunguana mashati?
 
Jamani msaada, hivi kwa nini ikitokea wapenzi wawili wakiachana, roho huuma sana pale mmoja amwonapo mwenzie ana mpenzi mpya?

...sababu hujui thamani ya mtu mpaka umpoteze.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom