Kwa nini reli isitumike kupunguza bei za vyakula?

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
INGAWA serikali imeshindwa kudhibiti upandaji holela wa bei ya mafutanchini na kusababisha kupanda kwa gharama za usafirishaji hususan wa vyakula,lakini bado kulikuwa na njia ya kudhibiti bei upandaji huo wa bei iwapo nguvukubwa zingeelekezwa katika kujenga reli nchini.
Upandaji wa bei huu tunaoushuhudia kwa sasa usingekuwa kwa kiwango hikiiwapo tungekuwa tunategemea zaidi usafirishaji wa bidhaa hasa mazao ya nafakana matuna kwa nje ya treni badala ya malori.
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba wakati wananchi wa maeneo mengiwakilia kukosa mahindi, baadhi ya maeneo yanayosifika kwa kulima mahindi kwawingi wanalia kukosa wanunuzi.
Juzi nilijikuta nailaani serikali, baada ya kuzungumza na swahiba yangummoja aliyepo Sumbawanga, ambaye aliniambia kwamba amekwama kulima shamba lakekwa sababu hadi sasa bado hajauza mahindi yake ya mwaka juzi na mwaka jana nawanunuzi hawaonekani kabisa kwa sasa.
“Ndugu yangu naona mwaka huu nitakwama kabisa kulima kwa sababu nimekosawanunuzi wa mahindi yangu nilikuwa tayari, kuuza japo kwa shilingi 10,000 tukwa gunia lakini hamna wanunuzi na msimu wa kilimo unakaribia kupita,” alisema.
Baada ya kumsikiliza na kujadiliana sana na ndugu yangu huyo, baadayemimi nikajikuta nazama katika fikara, suala hilo likabaki kunizunguka kichwani,nikajiuliza huyu ameshindwa kulima kwa sababu anayo mahindi yasiyo na mnunuzikisa usafiri wa barabara unawakwamisha wanunuzi kufika huko.
Ninajiuliza mahindi yamejazana kwenye maghala hayana wanunuzi, maeneomengi nchini mahindi hayapatikani jambo linalosababisha katika maeneo menginchini bei ya unga wa sembe kuwa juu.
Jambo moja nililolibaini hapo ni kuwa serikali imefanya kosa la kutowekakipaumbele katika usafiri wa reli, badala yake ianataka tuendelea kuiangalia nakuitegemea barabara kama njia kuu ya usafiri na usafirishaji nchini.
Ni wazi kuwa pamoja na kupanda sana kwa bei mafuta nchini, bado chakulakingeweza kusambazwa kutoka sehemu moja ya nchi na kupelekwa sehemu nyinginekwa gaharam ndogo na kingeuzwa kwa bei ndogo kama tungetegemea usafiri wa reli.
Tumesherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania lakini bado tunashindwakujua masuala ya msingi, yatakayotupunguzia madhila tungalia tunategemeausafiri wa barabara, ambao gharama zake ni kubwa kulinganisha na reli.
Uwapi msaada wa wataalamu wetu katika taifa hili, iwapi faida yakuwasomesha nje na kurejea na shahada lukuki iwapo wanashindwa kuwashauriwatawala wetu kwenye mambo ya msingi kama haya.
Wawapi wataalamu, wanaomshauri Rais na Baraza lake la Mawaziri kuhusunamna ya kuinusuru nchi yetu na fitina hii ya kupanda kwa bei ya vyakulanchini?
Bila ya shaka hili ni tatizo kubwa nchini mwetu kwa sasa, wataalamu wetuhasa wale wa uchumi walipaswa kuwaambia watawala wetu kwamba tunaweza kupunguzakwa kiasi kikubwa matatizo ya usafiri na gharama za maisha kwa kutumia usafiriwa reli badala ya barabara.
Kwa hakika mfumuko huu wa bei tunaoushuhudia sasa upande wa vyakulaumesababisha bei za vyakula mijini na vijijini kutokuwa na tofauti, ambapozimepanda kwa kiasi cha kuogopesha, ingawa imebainika kuwa tatizo ni kushindwakukisambaza kutoka kwa wakulima.
Hii ni kwa sababu karibu asilimia 95 ya wananchi wanategemea usafiri wabarabara, badala ya aina nyingine za usafiri ambazo bila shaka zingetuwezeshakuepuka gharama hizi tunazokumbana nazo.
Tujiulize iwapo maeneo mengi hapa nchini yanalia kutokuwa na chakula chakutosha kiasi cha kuililia serikali iagize kutoka nje, wakati kumbe kunawenzetu hapa hapa nchini wanacho chakula kingi lakini wameshindwa kukiuza kwakukosa wanunuzi.
Kukwama kwa vyakula kutoka kwa wakulima kunawaathiri wakulima kwa upandemmoja ambao wanashindwa kukujipatia fedha za kuwawezesha kufanya mambo mengineikiwemo kulima tena, wakati huo huo wakazi wa mijini wanajikuta wakikumbwa naupungufu wa chakula na bei ya kile kidogo kinachopatikana inakuwa ya kuruka.
Ni muda muafaka kwa serikali kuangalia upya sera yake ya usafirishajibadala ya kutenga fedha nyingi kushughulikia barabara, itenge fedha kwa ajiliya reli ambayo moja ya faida yake ni kuwa ikishatengenezwa inachukua muda mrefukuharibika ikilinganishwa na barabara.
Usafirishaji wa njia yareli ungesaidia kusambaza chakula kingi kwa haraka zaidi tofauti na ilivyo njiaya barabara ambayo kunahitajika magari mengi kusomba chakula kingi kwa wakatimmoja
 
Naweza nikaonekana nina jazba lakini ukweli ni kwamba naandika hii post kabla sijasoma post ya hapo juu kwa kuwa nimeona kichwa cha habari kinachohusu Reli. Nimeshindwa kujua hiyo reli itakayopunguza bei ya vyakula ni ipi? Mimi najua Tanzania kwa sasa hatuna reli hata moja kuna mataruma tu ya reli toka DSM, Tanga, Moshi hadi Arusha. Pia yapo mataruma yanayojiozea toka DSM, Morogoro, Dodoma, Manyoni, Tabora hadi Mwanza na Tabora hadi Mpanda na Tabora - Kigoma.

Kuna mataruma mengine ambayo yanasuasua toka DSM hadi Mbeya.

Barabara zetu zinakufa kwa sababu hatuna reli.
 
Naweza nikaonekana nina jazba lakini ukweli ni kwamba naandika hii post kabla sijasoma post ya hapo juu kwa kuwa nimeona kichwa cha habari kinachohusu Reli. Nimeshindwa kujua hiyo reli itakayopunguza bei ya vyakula ni ipi? Mimi najua Tanzania kwa sasa hatuna reli hata moja kuna mataruma tu ya reli toka DSM, Tanga, Moshi hadi Arusha. Pia yapo mataruma yanayojiozea toka DSM, Morogoro, Dodoma, Manyoni, Tabora hadi Mwanza na Tabora hadi Mpanda na Tabora - Kigoma.

Kuna mataruma mengine ambayo yanasuasua toka DSM hadi Mbeya.

Barabara zetu zinakufa kwa sababu hatuna reli.

ni kweli kiongozi viongozi wetu wamezifumbia macho kana kwamba hawajui kitu kinacho itwa reli ni nini
 
Nnahisi kutapika nikimsikia huyu dogo ningekuwa na uwezo ningewahamisha dunia yeye na baba yake
 
Namshaangaa huyu kuwa hajui reli imeuawa ! Watu wako bize kuua barabara

only in Tanzania! Ukiangalia gharama za barabara, mizani, biashara ya mitambo tunayokosa, inashangaza hatuandamani. Hivi haiwezekani watu binafsi waingia kwenye biashara ya mabehewa? Yani reli na kichwa na baadhi ya mabehewa yawe ya serikali lakini mabehewa watu waruhusiwe kumiliki na kukodisha kusafirisha mizigo kama makontena?
 
ni kweli kiongozi viongozi wetu wamezifumbia macho kana kwamba hawajui kitu kinacho itwa reli ni nini

Kitu kinachoitwa reli wanakijua vizuri sana ndo maana ktk kampen za ccm mwaka 2010 jk aliahidi kuijenga reli toka ubungo na kuelekea city centre
 
ni kweli kiongozi viongozi wetu wamezifumbia macho kana kwamba hawajui kitu kinacho itwa reli ni nini

Kitu kinachoitwa reli wanakijua vizuri sana ndo maana ktk kampen za ccm mwaka 2010 jk aliahidi kuijenga reli toka ubungo na kuelekea city centre vinginevyo ni kiburi tu kimewajaa ila uelewa wanao
 
only in Tanzania! Ukiangalia gharama za barabara, mizani, biashara ya mitambo tunayokosa, inashangaza hatuandamani. Hivi haiwezekani watu binafsi waingia kwenye biashara ya mabehewa? Yani reli na kichwa na baadhi ya mabehewa yawe ya serikali lakini mabehewa watu waruhusiwe kumiliki na kukodisha kusafirisha mizigo kama makontena?
hawana muda wa kufikiri na hawako tayari kupewa fikra na maarifa labda deal !
 
We hujui ufufuaji wa Reli aloushikia Bango Nundu ndo umemng'oa,Reli ya TAZARA na TRC hazijafa,zimezuiwa na wenye malori,we hukumbuki Mramba alipewa wizara inayoisimamia Air Tanzania wakati wote wanajua ndio alikuwa mmiliki wa Precision,nini kilitokea kwa Air tz?
 
Nchi hii imejaa wendawazimu wa kujitakia...feel sorry for ourselves
 
T 2015 CDM, reli ikitumika, makampuni ya usafirishaji za vigogo zitafilisika. Kumbuka kauli ya Waziri Maige kuwa na hisa kwenye kampuni ya usafirishaji? Hutaki unaacha, Maige na kampuni yake ni cha mtoto.
 
Back
Top Bottom