Kwa nini Rais analazimisha kitu ambacho hana madaraka nacho ya Kikatiba? (Video)

muulize mwanakijiji ni nini kimo na hakimo kwenye muswada hatasema kwa undani lakini hotuba ya Rais ataichambua utadhani ndio katiba yenyewe.

sijui umeingiiaje lakini huo mswada nilishauchambua vipengele kwa vipengele kabla CCM jhawajacharuka. Ipo thread tafute tu hapa.
 
That can be done too.
Imagine Obama angekuwa na 83% ya congress...... angepitisha mswaada wowote anaoutaka,
Are you sure ? Yaonekana huijui Marekani.
the only thing ambacho kingemzuia ni Supreme court based on constitutionality..... thats it.
Yeah, that's one and there's more.
Au labda na congressmen wake wamgeuke.....
Yeah, that's two and there's a lot more.
.....other than that, it's easy like.... (you know the rest).
Nay, it's not that easy.

SOBY, kuna mambo mengine yanawezekana tu hapa kwetu Bongo k.m. hotuba ya leo aliyotoa Kikwete, masikini Tanzania !
 
Jk katoa mfano jana kwamba hata kenya Rais alikuwa sehemu ya mchakato lakini hapa Tanzania hatutaki kabisa. kama kuna haja ya kuchanganya wateule wa rais na wasio wateule hoja ingejengwa lakini Tundu lissu alikimbia kuhudhuria vikao vya kamati na kuwaaacha wengine wakijenga hoja kabla ya kwenda bungeni lakini hivi leo anabisha na kukataa walioamua wenzake waliohudhuria vikao vya kamati kabla ya bunge ambako kulikuwa jukwaa muhimu la kutoa mapendekezo kwa mjadala wa wazi wa kamati ya bunge
 
Pipijojo, kama hujui sheria kama mie hapa, kukaa chini na kuwasikia wataalam siyo dhambi.

Ona sasa unavyojidhihirisha ulivyo mweupe.SOBY, MM Mwanakijiji, JMushi1 na wengine, nimeupenda mjadala wenu zaidi ya hotuba.

Endeleeni kutufungua macho wengine. Naona ngoma bado mbichi sana.

Nimelipenda swali la "Maadamu Kikwete na CCM wana kila kitu, kwa nini hawajaandika wao peke yao katiba......?"
 
muulize mwanakijiji ni nini kimo na hakimo kwenye muswada hatasema kwa undani lakini hotuba ya Rais ataichambua utadhani ndio katiba yenyewe.

kila post unabwabwaja tuu

acha upotoshaji na hakuna jipya unalolitetea zaidi ya ubinafsi,

"the enemies of God have started their stupidity aggression"
 
sijui umeingiiaje lakini huo mswada nilishauchambua vipengele kwa vipengele kabla CCM jhawajacharuka. Ipo thread tafute tu hapa.

kama ulitoa hiyo post hapa je umelidhika na mchango wa watanzania wenzako. je kwa nini usifanye muktasari wa mchango huo na kuleta tena hapa kisha tukupe baraka kama ni mapendekezo yetu ya katiba mpya badala ya kujadili mambo ambayo hayatakuwa sehemu ya katiba mpya kama ilivyo kwa kauli za JK ambazo hazina sehemu ya kipengere cha katiba lakini muda mwingi tunapoteza kujadili mistari ya hotuba hiyo. naona muda huo tungeupoteza na kuzama katika kuitengeneza katiba mpya faida ingekuwa upande wetu
 
Are you sure ? Yaonekana huijui Marekani.



SOBY, kuna mambo mengine yanawezekana tu hapa kwetu Bongo k.m. hotuba ya leo aliyotoa Kikwete, masikini Tanzania !
I do, more than what you think.
Hivi hii hotuba ina kasoro gani? Zaidi ya chuki dhidi yake?
What is so special ambacho wewe unaona kinahalalisha ukilaza wa JK kutoka kwenye hotuba hii?
 
faida ya kutoa maoni kuliko kujadili hotuba ya JK ni moja tu hata kama tume ya katiba itapuuza maoni yetu tutarudi tena hapa Jf na kukataa katiba kwa mtazamo wa pamoja lakini lazima tuwe na presentation yetu ya kusimamia hoja zetu na itapendeza kama itakuwa wazi kwetu sote
 
Mimi ni mmoja wa wasiopenda kujadili watu na matukio bali napenda tujadili hoja za kuweka au kutokuweka katika katiba mpya na hii itasaidia wengi kupunguza ubishani hapa (small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas.)
 
ameamuakujitiwisha jukumu hili kwa makusudi nakwa kukikua sheria za nchi ili historia imtambue kuwa yeye ndio kinara wa uundwaji wa katiba lakini ukweli ni kwamba kikwete na ccm yake wanacheza rafu
 
wengine mko nje ya nchi mnajifanya kuelewa sana kinachoendelea huku nyumbani hebu tuliizeni na sisi tulioko hapa ndio maana mnanukuu vitu ambavyo JK hakusema hata kama ni siasa sivyo hivyo

hivi kumbe na wewe ni mweupe hivi upstairs?!!!! hujui lolote na tatizo lako nimegundua kuwa hata huo mswaada ulipota jana hujausoma....
 
Kwa nini wameweka vitisho vya hukumu na vifungo mtu akihoji? kama huo si udikteta ni nini waache kabisa mchezo tutamalizana kwa ajili ya katiba, wachezee katiba ya CCM si hii.

Mkuu Rais na wabunge wa CCM na CUF kuna kitu wanaitakia Tanzania, tusubiri matokeo ya udikteta wa katiba. Katiba ya CCm si katiba bali ni utaratibu wa kulindana (Walaji wa nchi Mafisadi)
 
nimemnukuu tu yeye kuwa anadai kuwa anayo mamlaka hayo na katiba na pia ametoa mfano wa tume mbalimbali huko nyuma za kushugulikia maswala ya katiba mwaka 1963 na mwaka 1983 ambazo ni Rais ndio aliziunda utaratibu ambao binafasi sikubaliani nao kwani kwa kuwa ulitumika mwaka 1983 na 1963 basi unafaa kwa watu wa 2011 that is wrong. kwahiyo kama hakuna kipengele chochote basi ndio itatupa hoja nzuri ya kuingia barabarani hiyo jumapili.


Ndugu yangu @politiki bila kubishana sana hakuna kipengele kinachompa rais mamlaka ya kufanya anayotaka kufanya. Hakuna. Mwaka 1983 na 1963 nchi ilikuwa ya chama kimoja tofauti na sasa ambapo tuna vyama vingi. Kwa Kikwete kunukuu marekebisho yaliyofanywa na marais wengine waliomtangulia bila kusoma katiba iliyo mbele yake inasema nini ni kutuchezea akili. Tunajaua anaendesha nchi kwa mazoea na ndio maana hana jipya (hata kukutana na wazee ni mtindo wa kizamani sana), Sasa hivi watu wanakutana kupitia facebook, twitter, blogs, etc ni kizazi kipya.

Rais na wenzake wanakazana kunadi 'udomekrasia' wao katika huu mchakato, bija kujali kuwa watu wameusoma au la. Ukisoma ule mswada ni umejaa 'urais wa kifalme' na sio huo udemokrasia wanaoimba. Ni watu wawili ndio watakuwa na final say juu ya hii katiba mpya, rais wa Jamhuri ya muungano akishauriana na rais wa Zanzibar.
 
kwa kuanzia mwenye access na muswada uliopitishwa bungeni dodoma tuletee hapa tuone ni nini hakimo ambacho tulitaka kiwemo tutolee maoni kama JK alivyosema.

Jamani mbona huu muswada ulishawekwa hapa siku nyingi tu! PIPIJOJO changamka kidogo, search humu ndani utaupata na michango mingi tu toka kwa wadau.
 
chadema ndio hawaelewi ni kwa nini huwezi kumwondoa kabisa Rais aliyopo madaraka kuwa sehemu ya mchakato lakini alisema hiyo haina maana yeye ndiye ataandika katiba bali ni maoni ya wananchi na kura itakayopigwa ama kukubali au kukataa katiba kabla haijawa rasmi

mkuu usiwe kama jaji werema....mswaada ule una mapungufu makubwa sana...rais analazimisha ili wat wamtambue kuwa ana mamlaka ya kuongoza mchakato wa katiba kitum ambacho si kweli.....kama alivyosema mzee mwanakijiji...kwa kile alichokisema jk jana basi hakuna maana ya kuwepo kwa huo mswaada..jk angewatumia wabunge wake wale wale akawapangia mda wa kuunda katiba.....
 
mwanakijiji, i am sorry to say you are wrong. kama umemsikiliza vizuri jk leo amekuwa akinukuu katiba hii iliyopo ambayo ina mpa mamlaka ya kuunda Tume ya katiba kwahiyo kama aliyowahi kusema mnyika huko nyuma kilichotakiwa kufanywa bungeni ni kufanya mabadiliko ya katiba iliyopo sasa na kuigiza kipengele kitachowapa rasmi mamlaka kamili wananchi ya kuunda katiba yao wenyewe bila kuingiliwa na mamlaka yeyote kwahiyo mabadiliko ya katiba nchi hii hayawezekani kwa utaratibu uliopo inatubidi tuingie mtaani kudai haki ya kuamua namna nchi yetu itakavyotawaliwa. we have to fight back otherwise forget about having the constitution with political and legal legitimacy.

Nina hakika, labda tukaichunguze katiba iliyopo vizuri, hakuna sehemu iliyoandikwa/inayompa Rais kuunda katiba mpya. Haipo, isipokuwa kuna kipengele kinachomuruhusu kufanyia marekebisho katiba iliyopo. Kumbuka kwamba, katiba ya sasa tunayotumia ni ya 1977, ambayo walisema ni ya kudumu. Kama ni ya kudumu means hakutatengenezwa katiba yoyote, isipokuwa kuifanyia marekebisho ili iendane na vile CCM wanavyotaka au nchi wafadhili wananvyotaka.

Wewe na mwanakijiji, mmefanana kwa kipengele cha kuirekebisha katiba ya sasa, kuingiza kipengele kitachowezesha/ruhusu katiba mpya kuundwa. Umetofautiana na Mwanakijiji kipengele cha nani aendeshe mchakato wa katiba, japokuwa mwanankijiji hajasema, wewe umesema, kipengle hicho kiwape wananchi nguvu ya kutengeneza mkataba na wanasiasa, watumishi wa umma na asasi za kiraia-yaani KATIBA.

Mwanakijiji kakosea wapi? kutokusema kipengele kimpe nani nguvu ya kutengeneza katiba? Nyote mko sawa, kwani mwanakijiji amemalizia kwa kusema, wananchi watasusuia mchakato huo ambao haupo kikatiba, bali unalindwa na sheria ovu waliyoipitisha, hapo ndipo wanasiasa watakapojua kuwa, wananchi ni wakubwa kuliko wao.

Hii ni kusema kwamba, mchakato huo kuanza, tayari wamevunja katiba waliyoapa kuilinda..

 
By Mzee Mwanakijiji;


a. Kabla ya kuundwa kwa tume hiyo ya kukusanya maoni ilitakiwa kwanza yafanyike mabadiliko katika Katiba ya sasa ambayo yangeweza utaratibu wa kuandika Upya Katiba ya nchi. Katiba ya sasa inaruhusu kufanyiwa mabadiliko tu (ammendments) lakini hairuhusu kuwepo kwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya.

b. Mabadiliko hayo ya Katiba ya kuweka mchakato ndio yangejadili nani na kwa vipi teuzi za tume ya kuandika Katiba unatakiwa kufanyika. Haiwezekani Rais aliyeko madarakani anajiamulia tu kuandika Katiba Upya yeye mwenyewe halafu wengine wafuate; Tukumbuke tamko la kuandika Katiba Mpya lilitolewa kwenye salamu za mwaka mpya! Halikutolewa Bungeni na wala hakukuwa na utaratibu wa kuonesha kuwa umejali wananchi. Ulikuwa ni uamuzi binafsi wa Kikwete. Tukumbuke kuwa kwenye hotuba ile hakusema "amedhamiria" la hasha alisema "ameamua".

c. Ni kutoka hapo sasa ndio sheria ya kusimamia mchakato wa kuelekea Katiba Mpya ungeweka. Ina maana ya kwamba suala la Kuandika Katiba Mpya lingewekwa ndani ya Katiba ya sasa na kuangaliwa kama tunavyoangalia yale mambo 8 ambayo yanahitaji ridhaa ya pande mbili za Muungano (theluthi mbili ya wajumbe). Lakini kwa hivi ilivyo Kikwete na Shein wataamua wao wenyewe. Sasa hiyo sheria ndio ingezingatia maoni ya watu wengine.

Utaona basi kuwa kosa la kwanza limefanyika kwa kutozingatia Katiba ya sasa kwanza - haina mchakato wa kuandika Katiba Mpya - na hivyo kufanya hoja ya Katiba Mpya haiwezi kutolewa na wale walioapa kuilinda ya sasa na kama inatolewa walitakiwa kwanza kufanyia mabadiliko hii Katiba ili wajipe uwezo wa kuzungumzia "katiba mpya".


Kila mwenye busara na atambue maandiko haya ya MMM, lakini kwa kuwa busara zao zimekwenda likizo watadhani tunachuki nao, but we don't hate them, we hate their evil, we opposed them and gently instructed them, in the hope that God will grant them repentance leading them to a knowledge of the truth, But for they have eyes but do not want to see, ears but do not want to hear then the struggle against this corrupt and unaccountable political regime and more often the underlying poverty, unemployment, lack of education, and blocked avenues of economic opportunity is our duty.

T
his is a right time to employ non-cooperation, non-violence, peaceful resistance and judiciary as our weapons in this fight.
Sasa wakati wengine tunajipanga kwenda barabarani kudai haki zetu, basi wengine (wale wenye weledi wa sheria) wasijipange kwenda mahakamani kwa sababu hii sheria ya Mchakato ni unconstitutional They represent about 1 percent of the population. They know in numbers we can defeat them
 
Mimi ni mmoja wa wasiopenda kujadili watu na matukio bali napenda tujadili hoja za kuweka au kutokuweka katika katiba mpya na hii itasaidia wengi kupunguza ubishani hapa (small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas.)

wewe hujadili hoja, unajadili watu. mbona unataka rai walioko nje wakuulize J.K alichosema? Kwani kila alichokisema Rais ni sawa?
 
Back
Top Bottom