Kwa nini Rais analazimisha kitu ambacho hana madaraka nacho ya Kikatiba? (Video)

Amesema kwa sababu ni "tunu ya Taifa."

Sababu za Muungano za kijinga jingaaa! Tunu ya Taifa ni madini yanayochimbwa na Barrick bure na twiga wanaotoroshwa na ndege.
Article 20(1)(b).
Unaruhusiwa kuuongelea muungano, kwa mfano kuwa na serikali tatu au moja, au mbili kama zilivyo.
Ila chama chochote cha siasa hakiruhusiwi kushawishi watu kuuvunja muungano.
 
Article 20(1)(b).
Unaruhusiwa kuuongelea muungano, kwa mfano kuwa na serikali tatu au moja, au mbili kama zilivyo.
Ila chama chochote cha siasa hakiruhusiwi kushawishi watu kuuvunja muungano.

Nani kaamua kuwa chama chochote hakiruhusiwi kushawishi watu kuvunja muungano?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nani kaamua kuwa chama chochote hakiruhusiwi kushawishi watu kuvunja muungano?
Wananchi kupitia wawakilishi wao.
Ndiyo katiba yetu inavyosema kaka!!...
Au wawakilishi wenu hawakuapa kuienzi hii katiba?
 
Huwezi kuandika katiba mpya, bila kutunga sheria ya kuandika katiba mpya.

Ili uweze kuandika sheria ya kuandika Katiba Mpya lazima uwe na madaraka ya kuandika Katiba Mpya na mabadaraka ya kuandika Katiba Mpya yanatakiwa yawe ndani ya Katiba iliyopo. Kwenye Katiba yetu hiyo option ni NIL au N/A!
 
Wananchi kupitia wawakilishi wao.
Ndiyo katiba yetu inavyosema kaka!!...
Au wawakilishi wenu hawakuapa kuienzi hii katiba?

waliapa "kuilinda, kuitetea na kuihifadhi" siyo kuiondoa na kuleta nyingine. Wamepewa uwezo wa kuifanyia mabadilikoo hii ila wakitaka mpya ni lazima waje kwa wananchi. WAnbunge hawakuchaguliwa kuandika Katiba Mpya! Sijui ni kipi hapa hakieleweki. Viongozi hawana madaraka nje ya yale waliyopewa. Unafikiri rais kwa vile ni Rais anaweza kwenda kwenye nyumba ya mtu na kusema "toka kwenye nyumba hii" na mtu akatoka kwa vile "rais kaagiza"?
 
Article 20(1)(b).
Unaruhusiwa kuuongelea muungano, kwa mfano kuwa na serikali tatu au moja, au mbili kama zilivyo.
Futa hiyo serikali moja. Sio kweli, Rais amesema leo, na Sheria iliyopitishwa imesema, kwamba hakuna kuongelea kufuta serikali ya Zanzibar wala ya Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo ni serikali mbili na kwenda juu, moja hakuna.

Hii ni TUME YA RAIS YA KUCHAGUA MAONI YA WANANCHI NA KUANDIKA RASIMU YA KATIBA MPYA.
 
Ili uweze kuandika sheria ya kuandika Katiba Mpya lazima uwe na madaraka ya kuandika Katiba Mpya na mabadaraka ya kuandika Katiba Mpya yanatakiwa yawe ndani ya Katiba iliyopo. Kwenye Katiba yetu hiyo option ni NIL au N/A!
Si kweli.
Hata Regia mtema angeweza kuandika mswaada wa kuwa na katiba mpya, halafu kama bunge likiridhia (i.e National assembly + President ) itakuwa sheria na mchakato utaanza.
 
Si kweli.
Hata Regia mtema angeweza kuandika mswaada wa kuwa na katiba mpya, halafu kama bunge likiridhia (i.e National assembly + President ) itakuwa sheria na mchakato utaanza.

Kama ni rahisi hivyo kwanini tunahangaika? si bunge lingeandika tu Katiba Mpya yaishe? Kwanini Kikwete ametumia muda mrefu sana wakati Bunge llote lao, rais yeye? Si angeamua tu kutuambia "nimeagiza x,y, na za watuandikie katiba mpya halafu ikiwa tayari nitawataarifu?". Kama ingekuwa ni rahisi hivyo kwanini wamehangaika na huu mswada na wanatumia nguvu kubwa sana kuwashawishi watu wakubali kuwa wako sahihi? Si wangeendika tu wenyewe - wasomi wanao, chama wanacho, na 'madaraka' unaamini wanayo?

Unless unaamini kuwa wanachofanya ni hisani au geresha a.k.a kiinimacho...
 
Kama ni rahisi hivyo kwanini tunahangaika? si bunge lingeandika tu Katiba Mpya yaishe? Kwanini Kikwete ametumia muda mrefu sana wakati Bunge llote lao, rais yeye? Si angeamua tu kutuambia "nimeagiza x,y, na za watuandikie katiba mpya halafu ikiwa tayari nitawataarifu?". Kama ingekuwa ni rahisi hivyo kwanini wamehangaika na huu mswada na wanatumia nguvu kubwa sana kuwashawishi watu wakubali kuwa wako sahihi? Si wangeendika tu wenyewe - wasomi wanao, chama wanacho, na 'madaraka' unaamini wanayo?
That can be done too.
Imagine Obama angekuwa na 83% ya congress...... angepitisha mswaada wowote anaoutaka, the only thing ambacho kingemzuia ni Supreme court based on constitutionality..... thats it.
Au labda na congressmen wake wamgeuke..... other than that, it's easy like.... (you know the rest).
 
chadema ndio hawaelewi ni kwa nini huwezi kumwondoa kabisa Rais aliyopo madaraka kuwa sehemu ya mchakato lakini alisema hiyo haina maana yeye ndiye ataandika katiba bali ni maoni ya wananchi na kura itakayopigwa ama kukubali au kukataa katiba kabla haijawa rasmi
 
awali tulisema vitendo vya chadema kususasusa havina faida pekee bali na hasara pia wangebaki bungeni kutoa maoni yao na sisi wananchi tungewasikia na kupima upande wenye hoja. walisusa wakidhani mchakato utasisimama na sasa wanaanza kulalamika
 
Jamani kikubwa hapa ni Chama cha wanasheria kitamke kuwa sheria hii iliyopitishwa ni batili kwa sababu inapingwa na watanzania wengi. hawaridhishwi nayo. Kuna sheria nyingi tu ambazo wamedeclare ni unconsititutional. Hii iwe mojawapo na ipingwe hasa. Hotuba ya raisi naona inatumika kama mpira wa kiume kuwezesha kikundi kimoja tu kupitisha Katiba. Kama ameshindwa kutupa katiba tunavyotaka aache anayekuja atupatie. Kwa nini hii sheria ina vitisho vingi na vikwazo hasa kwa suala nyeti kama muungano.

UNAFIKI NI HUU- Wananchi wamepata fursa ya kuujadili, Muswada umejadiliwa Dar, Dodoma na Zanzibar. kote huko hakukuwa na matokeo ya muafaka. Kuna haki gani ya kusema wananchi wameshiriki? Eti wengine kwa e mail, hizo e mail ni wangapi kati ya 44 milion.

Wazanzibari wanaupinga muungano ,viongozi wao ndani ya vyumba na majukwaa wanautaka hiki kiini macho cha nini? Hivi hatuoni vita ya wazi kabisa inakuja jamani.Naunga mkono uanzishwe mchakato PARALEL na huu wa CCM na CUF kwa sababu sheria hii imeshaziba haki nyingi za wananchi.

RAIS WANGU INAUMA INAUMA INAUMA.
 
waliapa "kuilinda, kuitetea na kuihifadhi" siyo kuiondoa na kuleta nyingine. Wamepewa uwezo wa kuifanyia mabadilikoo hii ila wakitaka mpya ni lazima waje kwa wananchi. WAnbunge hawakuchaguliwa kuandika Katiba Mpya! Sijui ni kipi hapa hakieleweki. Viongozi hawana madaraka nje ya yale waliyopewa. Unafikiri rais kwa vile ni Rais anaweza kwenda kwenye nyumba ya mtu na kusema "toka kwenye nyumba hii" na mtu akatoka kwa vile "rais kaagiza"?
Yaani hapa sioni haja ya kutoka jasho.
Rais akiandika sheria inayomuwezesha kuingia nyumbani kwako muda wowote, na bunge likapitisha, na mahakama kuu ikahalalisha constitutionality ya hiyo sheria.... basi mkuu hutakuwa na jinsi.
Unanikumbusha US History 205 (pre civil war US history) ambapo waingereza waliandika Quartering act, 1764 inayoruhusu askari wa uingereza kuingia nyumba yeyote ile na kupata mkogo na usingizi wa pono chumba chochote anachohitaji.... na Parliament ya UK ikapitisha.
Once yo have the legislature(more than two thirds), you can be a dictator, easily!
 
Kwa haraka inawezekana kudhaniwa kuwa Rais Kikwete ameweza kutetea kwanini yeye ndiye aanzishe na kusimamia mchakato wa Katiba Mpya. Kwamba alitumia madaraka yale yale ambayo yalitumiwa na viongozi wengine wa nyuma- japo mara zote hizo haikuwa kuhusu Katiba Mpya bali kubadilisha katiba iliyokuwepo na kuiboresha na pale ambapo kulikuwa na kwenda kwenye Katiba ya kudumu kulifanyika katika mazingira ya chama kimoja na hivyo kuondoa hoja ya ushiriki wa vyama vingine na hata kuhoji. Rais ndiye alikuwa mkuu wa chama hicho kimoja na ndiye mkuu wa serikali na hivyo inaeleweka kwanini ilikuwa hivyo. Hili halihalalishi hali iyo kurudiwa sasa katika uelewa wetu wa demokrasia ya vyama vingi na ukuu wa wananchi (siyo chama kama ilivyokuwa zamani).

Hatujawahi kuwepo hapa tulipo sasa. Njia hizo za zamani zilizotumika ndizo zilipotufikisha hapa na tunahitaji ubunifu wa hali ya juu. Kurudia mambo yale yale kwa namna ile ile kuna jina lake lakini kwa vile tunaishi katika zama mpya tungetarajia ubunifu zaidi.

Katiba ya sasa haimpi Rais kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ana uwezo akitaka wa kusimamia kwa kupitia chama chake mchakato wa kufanya mabadiliko ya katiba ya sasa. Lakini kwa vile anachotaka ni katiba Mpya napendekeza kuwa Katiba ya sasa haina madaraka hayo kwa Rais au kwa mtu mwingine yeyote na kiukali kabisa tunaweza kugeuza na kudai zoezi zima haliwezi kufanya na wale walioapa kulinda Katiba ya sasa! Hakuna kipengele chochote kinachohusiana na kuandika katiba mpya katika Katiba yetu ya sasa. Sasa kama hakuna imekuwaje Rais aamini kuwa ana madaraka ya kuanzisha hata kuitisha Bunge la Katiba?

Kujibu swali lake la mwisho ni kuwa:

a. Kabla ya kuundwa kwa tume hiyo ya kukusanya maoni ilitakiwa kwanza yafanyike mabadiliko katika Katiba ya sasa ambayo yangeweza utaratibu wa kuandika Upya Katiba ya nchi. Katiba ya sasa inaruhusu kufanyiwa mabadiliko tu (ammendments) lakini hairuhusu kuwepo kwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya.

b. Mabadiliko hayo ya Katiba ya kuweka mchakato ndio yangejadili nani na kwa vipi teuzi za tume ya kuandika Katiba unatakiwa kufanyika. Haiwezekani Rais aliyeko madarakani anajiamulia tu kuandika Katiba Upya yeye mwenyewe halafu wengine wafuate; Tukumbuke tamko la kuandika Katiba Mpya lilitolewa kwenye salamu za mwaka mpya! Halikutolewa Bungeni na wala hakukuwa na utaratibu wa kuonesha kuwa umejali wananchi. Ulikuwa ni uamuzi binafsi wa Kikwete. Tukumbuke kuwa kwenye hotuba ile hakusema "amedhamiria" la hasha alisema "ameamua".

c. Ni kutoka hapo sasa ndio sheria ya kusimamia mchakato wa kuelekea Katiba Mpya ungeweka. Ina maana ya kwamba suala la Kuandika Katiba Mpya lingewekwa ndani ya Katiba ya sasa na kuangaliwa kama tunavyoangalia yale mambo 8 ambayo yanahitaji ridhaa ya pande mbili za Muungano (theluthi mbili ya wajumbe). Lakini kwa hivi ilivyo Kikwete na Shein wataamua wao wenyewe. Sasa hiyo sheria ndio ingezingatia maoni ya watu wengine.

Utaona basi kuwa kosa la kwanza limefanyika kwa kutozingatia Katiba ya sasa kwanza - haina mchakato wa kuandika Katiba Mpya - na hivyo kufanya hoja ya Katiba Mpya haiwezi kutolewa na wale walioapa kuilinda ya sasa na kama inatolewa walitakiwa kwanza kufanyia mabadiliko hii Katiba ili wajipe uwezo wa kuzungumzia "katiba mpya".

Kwa vile suala la Katiba Mpya basi ni la nje ya watawala wetu wa sasa ni wazi kuwa toka mwanzo ushiriki wao ulitakiwa uwepo na siyo mtindo huu wa kuburuzana na kuwapa wananchi taarifa zisizo za kweli kwa ajili ya faida za kisiasa (political expediency). Badala ya kusahihisha makosa wameamua kuendelea katika kukosea. Wananchi wafanye nini?

a. Watahamasishana wasishiriki kwenye hiyo tume na kuwaachia wana CCM wakaambizane wanayotaka kuyasikia. Yaani A total boycott of the exercise. Hakuna namna ya kuwalazimisha wananchi washiriki. Na kama tulivyoona leo hata wana CCM wenyewe hawako katika hali ya kuruka ruka sana na kufurahia mchakato wenyewe.

b. Watasubiri ije siku ya kupiga kura ya maoni watahamasishana kwenda kuungusha kwenye sanduku la kura kuwaonesha watawala kuwa wananchi ndio wako supreme zaidi ya Rais na Bunge. Kwa vile wamekubali kuweka kiwango cha chini ya asilimia 50 kupitisha ni kiwango kidogo sana kukifikia! kwani upinzani unahitaji kuhamasisha asilimia 51 tu!

Sioni dalili yoyote ya watawala kukaa pamoja na kama tuliyoyashuhudia wiki hii ni mfano basi Kikwete hayuko tayari hata kukubali hoja za upande wa pili - ila upande wake ndio anataka ukubaliwe bila kuhojiwa au kupingwa. Na uamuzi wa kuweka adhabu kwa watu watakopinga mchakato huu umethibitisha pasipo shaka kuwa kwa njia ya kawaida haiwezekni kushinda isipokuwa kwa shurti, vitisho na vifungo.

Utabiri wangu: Mswada huu utarudishwa mapema tena Bungeni ili ufanyiwe marekebisho kama walivyofanya kwenye msaada ya gharama za uchaguzi ambao wengine tuliupinga na kuonesha makosa mapema wakang'ang'ania na kusaini kwa mbwembwe lakini miezi mitatu tu baadaye wakaurudisha na bado wanahitaji kuufanyia marekebisho. Mswada huu ukiwa sheria hautekelezeki, haukubaliki, na watawalazimisha watu kuupuza. Tunaposema katiba ni 'mama' hatusemi tu hivi hivi. Sasa mama habambikiziwi! Vingenevyo wapo Watanzania ambao wataiona katiba ijayo kuwa ni 'katiba ya kambo'! Hawataipenda, hawataizingatia na watajaribu kweli kweli kuibadilisha. Kama Rais wa sasa ameweza kufanya hivi bila kuulizwa na mtu guess what akija Rais mwingine?

Hadi wakubali kusikiliza upande wa pili na kufuata ile kanuni ya kwanza - KATIBA LAZIMA ITOKE KWA WANANCHI WENYEWE. Kuanzia mfumo wa kuwashirikisha wananchi, nani anasimamia na inafikiwa vipi ni lazima iwe inasimama kwenye madaraka ya wananchi kutawala.

Mwanakijiji hayo unayosema hayatatusaidia kama JK kasema tutoe maoni yetu hebu tujalibu kutumia jukwaa hili kujenga hoja, hebu tuanzishe bunge letu hapa JF kujenga hoja na kutoa maoni yetu kipengere kwa kipengere ambavyo tunamwomba invisible kuwakilisha sehemu husika kwa ajili ya utekelezaji na kama JK hatasilikiza ndio tunakimbilia kwa wananchi kudai haki yetu
 
Last edited by a moderator:
Jamani kikubwa hapa ni Chama cha wanasheria kitamke kuwa sheria hii iliyopitishwa ni batili kwa sababu inapingwa na watanzania wengi. hawaridhishwi nayo. Kuna sheria nyingi tu ambazo wamedeclare ni unconsititutional. Hii iwe mojawapo na ipingwe hasa. Hotuba ya raisi naona inatumika kama mpira wa kiume kuwezesha kikundi kimoja tu kupitisha Katiba. Kama ameshindwa kutupa katiba tunavyotaka aache anayekuja atupatie. Kwa nini hii sheria ina vitisho vingi na vikwazo hasa kwa suala nyeti kama muungano.

UNAFIKI NI HUU- Wananchi wamepata fursa ya kuujadili, Muswada umejadiliwa Dar, Dodoma na Zanzibar. kote huko hakukuwa na matokeo ya muafaka. Kuna haki gani ya kusema wananchi wameshiriki? Eti wengine kwa e mail, hizo e mail ni wangapi kati ya 44 milion.

Wazanzibari wanaupinga muungano ,viongozi wao ndani ya vyumba na majukwaa wanautaka hiki kiini macho cha nini? Hivi hatuoni vita ya wazi kabisa inakuja jamani.Naunga mkono uanzishwe mchakato PARALEL na huu wa CCM na CUF kwa sababu sheria hii imeshaziba haki nyingi za wananchi.

RAIS WANGU INAUMA INAUMA INAUMA.
Mahakama kuu inaweza kuivunja hii sheria, siyo chama cha wanasheria.... they are just a bunch of lawyers who don't have any constitutional authority zaidi ya mimi na wewe.
 
sisi watanzania ni watu wa ajabu sana JK kasema tutoe maoni lakini sisi tunajadili hotuba yake mwisho tutakuta hatujatoa maoni na muda umekwisha. Jukwaa hili la JF linaweza kuanzisha post maalum kwa ajili ya maoni yatu na watu maalum hapa JF wakatusaidia kukusanya na kuyaweka vizuri kwa point form
 
mimi naona wengi wetu tunapiga kelele bila kwanza kujadili muswada ulipitishwa na bunge dodoma. muswada huu ungeletwa hapa ili tupitie nini ambacho tunaona kimeachwa na kutoa maoni yetu. kuna mambo tunadai lakini yapo kwenye muswada ili mradi tu mtu kasema na kulaumu.
 
muulize mwanakijiji ni nini kimo na hakimo kwenye muswada hatasema kwa undani lakini hotuba ya Rais ataichambua utadhani ndio katiba yenyewe.
 
kwa kuanzia mwenye access na muswada uliopitishwa bungeni dodoma tuletee hapa tuone ni nini hakimo ambacho tulitaka kiwemo tutolee maoni kama JK alivyosema.
 
Back
Top Bottom