Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,499
- 19,340
Nisemeje.
Kikwete hataki kubadilisha katiba ila anataka kuonekana kuwa anataka kuibadilisha baada ya kujulikana kuwa katiba iliyopo ni mbovu na ubovu huo ndio unaomfanya abaki madarakani hadi leo ingawa watu wenye akili wanajua kuwa alirudi madarakani kwa njia dubious zikichangiwa na ubovu wa katiba ya sasa.
Iwapo anakiri kuwa katiba ya sasa ina mapungufu yanayotakiwa kurekebishwa, asingeweza kuitumia hiyo kama kinga yake ya kumpa madaraka ya kutunga katiba nyingine; alitakiwa atoe milango wazi ya kuwa na utaratibu wa kutunga katiba huru. Huwezi kujenga nyumba imara kwa kutumia msingi mbovu. Vitisho vya kufunga watu wanaohoji katiba hiyo ni vya kijinga sana na vinatokana na akili mbovu ya Werema kwa vile ana upungufu mkubwa sana wa kuona mambo kwa kina, ndiyo maana nimegundua kuwa hukumu nyingi alizotoa akiwa jaji zimekuwa na utata. Vitisho hivi vinaweza vikaaiharibu kabisa nchi hii iwapo watu wa busara hawataingilia kati kulikokoa taifa hili lenye raslimali nyingi za asili na kukosa raslimali za binadamu wa kuiongoza