Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Hivi accademic staff wa UDSM wakistaafu wanaomba mkataba wa kuendelea; au chuo kinamuomba mtu aendelee kufundisha kama kuna upungufu wa service hiyo at that particular time? Nadhani ku avoid maneno mengi ni muhimu kujua ukweli.

Mkuu Felister
Utaratibu ni lazima wewe mwenyewe mstaafu au mtu mwingine mwenye mkataba wa muda maalum ujaze fomu. Tena zinapita kuanzia kwa mkuu wako wa idara kwenda skuli hadi utawala. Kama hukujaza fomu moja kwa moja ni kwamba umeamua kuachana na taratibu za chuo. Kilichofanyakia ni kuongeza muda wa kujaza mkataba mpya. Kama sijakosea ukijaza mkataba mpya kwa mstaafu unatumikia miaka 2. Ukishajaza mkataba, kuna kukubaliwa au kukataliwa maana majina yanapelekwa serikalini kwa uamuzi. Kama kawa, la Baregu halikurudi
 
Vijana ajira zetu zitakuwa na utata kama kama kila anayestaafu ataongezwa mkataba. Pale UDSM kuna lecturers vijana hawana nafasi ya kuonekana kisa mikataba wanayopewa retired professors.

Kama hakujipanga mpaka amefika umri wa kustaafu,imekula kwake. Vijana wanataka ajira zao na ni haki yao. Kuongezwa mkataba siyo lazima kwani si haki yake kwa mujibu wa sheria. Kama kungekuwa na uhaba kama unavyodai sawa lakini otherwise hakuna haja ya kuongezeana mikataba
 
Kama kawaida yake serikali ya CCM huwa haithamini wataalamu na badala yake wanafikiria nchi itaendelela kwa siasa na maneno mengi ya uwongo. Profesa Mwesiga Baregu ambaya amekuwa mhadhiri mwandamizi pale UDSM kwa muda mrefu na alipostaafu amekuwa akifanya kazi pale kwa mkataba.Inavyo onekana kwa sababu yeye ni mwanachama wa CHADEMA basi CCM kwa kushirikiana na serikali na uongozi wa UDSM wameamua kutompatia mkataba mpya na hii ni kwa sababu ya msimamo wake mkali dhidi ya uzembe unaofanywa na serikali iliyopo madarakani.

Napenda niseme tu kwamba bila kuthamini wataalamu na kukubali kukosolwa maendeleo hakuna. Hili liko wazi kwa sababu miaka zaidi ya 40 CCM imeendekeza siasa na uwongo ktk kuendesha nchi ndiyo maana wananchi wake bado ni maskini wa kutupwa na wajinga (hawana elimu).

Sote tunajua kuwa UDSM inakabiliwa na uhaba wa wahadhiri wandamizi, leo mnamyima mkataba profesa Baregu ambaye ni tegemeo kubwa ktk fani ya sayansi ya jamii nani ataziba pengo lake? hapo ndo tutamkumbuka prof. Luhanga ambaye alikuwa hatumii siasa kuendesha UDSM.

Prof. Baregu karibu jiunge hapa SAUT na uendelee kuwapiga bakora tu hao CCM wamefulia.

Ndiyo maana Rwanda wametuacha kwa sababu Kagame anawatumia sana wataalamu waliotoka hapa Tanzania lakini CCM inaona taabu ikikosolewa na wasomi wake.

Hivi mnataka hawa wazee waendelee kufanya kazi mpaka lini wakati vijana wanaomaliza vyuo hawana ajira? Sasa hivi kuna madarasa mengine yanatoa vijana zaidi ya 10 wenye upper second lakini wanabakizwa 3 tu kwa sababu ya hawa wazee wanaoendelea na mikataba. Nafikiri ni wakati wa kutoa ajira kwa vijana sasa kwani tukiendekeza hii mikataba mpaka Prof. afikishe miaka sabini itafika wakati kutakuwa hakuna replacement yao kwani watakuwa wazee watupu. Bravo JK Bravo Prpf. Mkandara and Prof. Maboko. Kazeni uzi huohuo lakini muajiri vijana kwa wingi angalau 50 kila mwaka. DIRA IWE AJIRA KWA VIJANA.
 
Naunga sana mkono ajira kwa vijana na serikali ianzishe Mfuko maalum kwa ajili ya kusomesha Watanzania (hasa Wahadhiri) digrii mbalimbali za Uzamivu (PhD). Tukianza na bajeti ya shilingi bilioni 12 kwa mwaka si mbaya.
 
Mkataba ukiisha sio lazima kuongezwa!

Tanzania hakuna wataalam wa kutosha na ndio maana UDOM ina uhaba wa wahadhiri na serikali inahaha kuwatafuta nje ya nchi.
Ukumbuke Prof Baregu sio kilaza ni kichwa hasa na hajasoma enzi hizi za kudesa au kununua masters na Phd. yule amesoma zamani bwana. tatizo lake kubwa ni SIASA UPINZANI ndio imeharibu
 
Ni serikali ya ajabu sana hii inayoshindwa kuthamini michango ya watu kama Baregu, mimi sipingi vijana kupata nafasi za ajira za kufundisha vyuoni, kuna jamaa anasema pale UD vijana 10 wanaweza kumaliza na Upper second zao lakini wakabakizwa 3 tu! Upper second sio kigezo cha kuwa mwalimu wa chuo kikuu, kigezo kikubwa kubaki pale kama mwalimu ni GPA, unatakiwa uwe na GPA isiyo chini ya 3.8, sasa ni vijana wangapi wanaomaliza sasa hivi vyuoni mwetu wanafikisha GPA hiyo! waliosoma universities watasema ni wazi ni wachache sana. Na hata wanapoajiriwa hawa vijana sio busara kuwapa full teaching responsibilities maana wanakuwa bado hawajapata uzoefu wakutosha na hapo ndio watu kama Baregu ni muhimu. Tuache mambo ya siasa kwenye vitu muhimu kama elimu, ninyi ni mashahidi haya mambo ya kukurupuka kwenye elimu tumeyaona kwenye matokeo ya darasa la saba, walimu form four failures, wanaenda kupata teaching course kwa miezi sita sasa product yake ni hiyo more than 50% darasa la saba wamefeli.
 
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
Chair (0773265265), Secretary (0713 212161), Treasurer (0784888284), Editor (0754462810)

14 Desemba 2009

TAMKO LA UDASA KUHUSU KUSITISHWA KWA AJIRA ZA WANATAALUMA WAANDAMIZI

Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imefadhaishwa na uamuzi wa serikali kusitisha ajira ya Profesa Mwesiga Baregu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliwasilisha serikalini ombi la kuendeleza mkataba wa ajira ya Prof. Baregu pamoja na wanataaluma wengine. Idhini ilitolewa kwa wale wote walioorodheshwa isipokuwa Prof. Baregu. Hakuna sababu zilizotolewa na serikali ya kutoidhinisha ajira ya mwanataaluma huyu mwandamizi.
Katika mkutano wa Jumuiya ya Wanataaluma wa tarehe 14 Desemba 2009, uongozi wa Chuo Kikuu ulitoa taarifa kwamba wanataaluma wengine kadhaa pia wamenyimwa fursa ya kuendelea kukitumikia chuo chetu.
Jumuiya ya Wanataaluma inapinga utaratibu wa maafisa wa serikali kuidhinisha ajira ya wanataaluma wa Chuo Kikuu wa sababu kadhaa: Kwanza, hakuna sababu zinazotolewa kwa kusitisha ajira ya mtu ye yote na hakuna vigezo vilivyowekwa wazi katika kutathimini ombi la Chuo Kikuu la kumwajiri mtu yeyote. Hali hiyo inatoa mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyofanyika katika kushughulikia nafasi ya Prof. Baregu.
Pili utaratibu huu unakiweka chuo chetu katika hali ya hasara kwa kukinyima huduma ya wanataaluma waandamizi na wenye uzoefu mkubwa. Wanataaluma hawa wanategemewa sana katika kuwakuza walimu wapya na kusaidia kubeba mzigo wa ungezeko la wanafunzi katika vyuo vikuu. Ikumbukwe kuwa kuna vyuo vingi vipya vinavyohitaji wataalamu wenye uzoefu wa muda mrefu kama hawa wanaokataliwa hapa kwetu.
Tatu utaratibu wa kuomba idhini ya serikali ili kumwajiri mwanataaluma unapingana na kanuni ya msingi ya Uhuru wa Wanataaluma (Academic Freedom). Uhuru wa taaluma umetambuliwa na Tamko la Dar es Salaam kuhusu Uhuru na Wajibu wa Wanataaluma (1990). Pia Azimio la Kampala kuhusu Uhuru wa Wanataaluma na Wajibu wao kwa Jamii (1990) ambalo lilipokelewa rasmi na Umoja wa Nchi Huru za Afrika liliwekea mkazo suala hili. Kwa kuleta wasiwasi juu ya hatima ya ajira ya wanataaluma, utaratibu huu wa serikali unakuwa kikwazo kikubwa kwa Uhuru wa Wanataaluma. Hali hii inaviweka vyuo vyetu katika hali ya unyonge na kuviondolea uwezo wa kukuza mawazo na hoja mbadala ili kukabiliana na changamoto za kuleta mabadiliko katika jamii.
Jumuiya ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inaitaka serikali kurejesha ajira ya Profesa Baregu pamoja na wanataaluma wengine ambao, kwa utaratibu huu, wamenyimwa fursa ya kukitumikia chuo chetu. Wanataaluma wanaihimiza serikali kutoingilia masuala ya ajira za vyuo vikuu na kuacha kazi hiyo ifanywe kikamilifu na mabaraza ya vyuo vikuu husika. Jumuiya hii itafanya mkutano wa kutafakari suala hili na kufanya maamuzi mahususi kabla ya mwisho wa mwezi Januari 2010.

Dalmas Nyaoro,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Mbona nawashangaa, badala ya kujadili haja iliyowekwa mezani mnaanza kulumbana tena juu ya udhaifu na ubora wa vyuo vikuu. Hebu tafuteni vielelezo vya hoja zenu kuhusu chuo fulani kuwa na mapungufu!

Ninachoweza kusema kuhusu hoja hii ni kwamba muwasilishaji hajatoa vielelezo vyovyote vya madai yake. Tutajadilije haja isiyo na vithibitisho vya hayo yaliyosemwa? Lakini pia, nikirudi nyuma; kufanya kazi ndani ya muda wa kustaafu siyo lazima kuongezewa muda, ila kama amenyimwa kwa chuki ya kuwa ni mwanachama wa chama pinzani hayo nitayasema madhaifu ya watendaji waliohusika. Vinginevyo, siyo lazima mimi nikistaafu kuwa na ulazima wa kufanya kazi mahala nilipokuwa nafanya kazi.
 
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
Chair (0773265265), Secretary (0713 212161), Treasurer (0784888284), Editor (0754462810)

14 Desemba 2009

TAMKO LA UDASA KUHUSU KUSITISHWA KWA AJIRA ZA WANATAALUMA WAANDAMIZI

Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imefadhaishwa na uamuzi wa serikali kusitisha ajira ya Profesa Mwesiga Baregu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliwasilisha serikalini ombi la kuendeleza mkataba wa ajira ya Prof. Baregu pamoja na wanataaluma wengine. Idhini ilitolewa kwa wale wote walioorodheshwa isipokuwa Prof. Baregu. Hakuna sababu zilizotolewa na serikali ya kutoidhinisha ajira ya mwanataaluma huyu mwandamizi.
Katika mkutano wa Jumuiya ya Wanataaluma wa tarehe 14 Desemba 2009, uongozi wa Chuo Kikuu ulitoa taarifa kwamba wanataaluma wengine kadhaa pia wamenyimwa fursa ya kuendelea kukitumikia chuo chetu.
Jumuiya ya Wanataaluma inapinga utaratibu wa maafisa wa serikali kuidhinisha ajira ya wanataaluma wa Chuo Kikuu wa sababu kadhaa: Kwanza, hakuna sababu zinazotolewa kwa kusitisha ajira ya mtu ye yote na hakuna vigezo vilivyowekwa wazi katika kutathimini ombi la Chuo Kikuu la kumwajiri mtu yeyote. Hali hiyo inatoa mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyofanyika katika kushughulikia nafasi ya Prof. Baregu.
Pili utaratibu huu unakiweka chuo chetu katika hali ya hasara kwa kukinyima huduma ya wanataaluma waandamizi na wenye uzoefu mkubwa. Wanataaluma hawa wanategemewa sana katika kuwakuza walimu wapya na kusaidia kubeba mzigo wa ungezeko la wanafunzi katika vyuo vikuu. Ikumbukwe kuwa kuna vyuo vingi vipya vinavyohitaji wataalamu wenye uzoefu wa muda mrefu kama hawa wanaokataliwa hapa kwetu.
Tatu utaratibu wa kuomba idhini ya serikali ili kumwajiri mwanataaluma unapingana na kanuni ya msingi ya Uhuru wa Wanataaluma (Academic Freedom). Uhuru wa taaluma umetambuliwa na Tamko la Dar es Salaam kuhusu Uhuru na Wajibu wa Wanataaluma (1990). Pia Azimio la Kampala kuhusu Uhuru wa Wanataaluma na Wajibu wao kwa Jamii (1990) ambalo lilipokelewa rasmi na Umoja wa Nchi Huru za Afrika liliwekea mkazo suala hili. Kwa kuleta wasiwasi juu ya hatima ya ajira ya wanataaluma, utaratibu huu wa serikali unakuwa kikwazo kikubwa kwa Uhuru wa Wanataaluma. Hali hii inaviweka vyuo vyetu katika hali ya unyonge na kuviondolea uwezo wa kukuza mawazo na hoja mbadala ili kukabiliana na changamoto za kuleta mabadiliko katika jamii.
Jumuiya ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inaitaka serikali kurejesha ajira ya Profesa Baregu pamoja na wanataaluma wengine ambao, kwa utaratibu huu, wamenyimwa fursa ya kukitumikia chuo chetu. Wanataaluma wanaihimiza serikali kutoingilia masuala ya ajira za vyuo vikuu na kuacha kazi hiyo ifanywe kikamilifu na mabaraza ya vyuo vikuu husika. Jumuiya hii itafanya mkutano wa kutafakari suala hili na kufanya maamuzi mahususi kabla ya mwisho wa mwezi Januari 2010.

Dalmas Nyaoro,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
For the time being nitakaa kimya!
Nasubiri kwanza nione kama Jakaya Mrisho Kikwete ataridhia kuongezewa mkataba wa kuongoza TANESCO yule fisadi na mla rushwa No_One in the name of Dr. Idris Rashid swahiba wake who has glatoaned over 300bn Tanzanian shilling loan from the syndicated local Banks . Sifahamu umri wa Prof.Baregu lakini what I know hata huko uzunguni anakotamani sana kutembelea Kikwete Professors huwa wanachapa kazi even after the age of 70 as long as afya inaruhusu. Haitaingia akilini kuwaambia wakafuge kuku hayo ni matumizi mabaya ya raslimali and then Jakaya goes on a trip kutafuta consultants huko anakokupenda USA si bora wampatie Green Card akaishi huko. As long as Mwesiga yuko fiti aruhusiwe kufundisha kwanza walimu hatuna naskia UDOM wanaagiza warusi sasa noma kwa Baregu inatoka wapi? We all know Mkandara alipewa birthday cake kuongoza UDSM wakati uwezo hana kisa mpambe wa JK.....
 
He is being punished for biting the hand that feeds him. Do you know that our leaders in third world countries behave like rouge village chiefs?
 
Ni aibu tupu
Afu kesho anasimama waziri wa elimu ya juu ..eti vyuo vinaupungufu wa walimu..
Natamani yule jamaa aliemtwanga Belusconi,Waje kama 20 wakati Huyo waziri akitangaza hayo...
Lini mtabadilika???....
 
Hii CCM haiwezi kuwa na udikteta namna hii, ikumbuke hawahawa walim-frustrate Dr Lamwai mpk akarudi CCM walimfukuza kazi UDSM wakamnyanganya licence ya kupractice in Mainland mpk alipoona watoto wake wanakufa njaa pasipo support ya anaowapigania akaona isiwe tabu akajitoa upinzani!

Nimefurahishwa na msimamo wa Udassa this time kuuliza ni kwanini Prof. Baregu hajaongezewa mkataba ilhali kuna upungufu wa maprofesa na kuna wengi wenye umri wake na zaidi wanaofanya kazi hapo chuoni! Huu ukiritimba wa CCM sasa basi au sasa tosha mageuzi huja hata wasipopenda! kuanza kuwa-fix intellectuals namna hiyo ni kuogopa kivuli chao maana wanajua nguvu ya hawa magwiji wa taaluma wanavyoweza ku-influence public!

Hii nchi si ya babazenu pekeenu nyie CCM mliolaaniwa, mmeshindwa kazi na inapaswa kuacha demokrasia ichukue mkondo wake! Kama mtu ni shabiki wa chama pinzani why should that be your issue? Are you ready to compromise the scarcity of lecturers in UDSM by letting a competent Prof. Baregu out of teaching? Where is the brain here? Are there any explanations you can give? au ni wajinga flani kama wakina Makamba ndo wanaamua who to be employed and who to be sent packing! Huyo Makamba ana hata diploma basi? For sure you will saw what you planted soon!
 
D they care? watoto wao wanasoma ulaya kwa pesa za kifisadi na scholarship za nchi, so life goes on. But this is the highest level of stupidity in the name of politics.
 
Hii CCM haiwezi kuwa na udikteta namna hii, ikumbuke hawahawa walim-frustrate Dr Lamwai mpk akarudi CCM walimfukuza kazi UDSM wakamnyanganya licence ya kupractice in Mainland mpk alipoona watoto wake wanakufa njaa pasipo support ya anaowapigania akaona isiwe tabu akajitoa upinzani!

Nimefurahishwa na msimamo wa Udassa this time kuuliza ni kwanini Prof. Baregu hajaongezewa mkataba ilhali kuna upungufu wa maprofesa na kuna wengi wenye umri wake na zaidi wanaofanya kazi hapo chuoni! Huu ukiritimba wa CCM sasa basi au sasa tosha mageuzi huja hata wasipopenda! kuanza kuwa-fix intellectuals namna hiyo ni kuogopa kivuli chao maana wanajua nguvu ya hawa magwiji wa taaluma wanavyoweza ku-influence public!

Hii nchi si ya babazenu pekeenu nyie CCM mliolaaniwa, mmeshindwa kazi na inapaswa kuacha demokrasia ichukue mkondo wake! Kama mtu ni shabiki wa chama pinzani why should that be your issue? Are you ready to compromise the scarcity of lecturers in UDSM by letting a competent Prof. Baregu out of teaching? Where is the brain here? Are there any explanations you can give? au ni wajinga flani kama wakina Makamba ndo wanaamua who to be employed and who to be sent packing! Huyo Makamba ana hata diploma basi? For sure you will saw what you planted soon!

hapa greti thinka limekasirika kweli kweli! dah! hawa ccm watauwa halafu mazikoni wasihuzurie.
 
CCM wanawatiha wasomi wengine kuachana na siasa za upinani wanataka wasomi wajiunge na chama chao ili waendelee kujisifu na kujivuna, Cccm inawaogopa wasomi ndo maana hawaishi vitimbi....ila wasomii wakomavu hawayumbishwi kimaamuzi na kimsimamo na mfisadi hawa.
 
Niliweka thread regarding this issue some few days ago kwa hiyo nashukuru kama UDASA wameliona hilo. Kusema ukweli matendo haya ya CCM ndo yametufikisha hapa kwenye umaskini ulio kithiri. Ukiona mtu yeyote anadharau wasomi na anapenda ushabiki wa kisiasa basi ujue pale kichwani kwake pako tupu.

Wajue tu CCM kwamba watabanaaaaa lakini mwisho wataachia tu, huu ndo mwanzo wa mabadiliko. Think of a guy like makamba hajawahi kutoa hotuba hata mara moja ya kiinglishi, hii inadhihirisha ukihiyo wake.
 
Hii CCM haiwezi kuwa na udikteta namna hii, ikumbuke hawahawa walim-frustrate Dr Lamwai mpk akarudi CCM walimfukuza kazi UDSM wakamnyanganya licence ya kupractice in Mainland mpk alipoona watoto wake wanakufa njaa pasipo support ya anaowapigania akaona isiwe tabu akajitoa upinzani!

Nimefurahishwa na msimamo wa Udassa this time kuuliza ni kwanini Prof. Baregu hajaongezewa mkataba ilhali kuna upungufu wa maprofesa na kuna wengi wenye umri wake na zaidi wanaofanya kazi hapo chuoni! Huu ukiritimba wa CCM sasa basi au sasa tosha mageuzi huja hata wasipopenda! kuanza kuwa-fix intellectuals namna hiyo ni kuogopa kivuli chao maana wanajua nguvu ya hawa magwiji wa taaluma wanavyoweza ku-influence public!

Hii nchi si ya babazenu pekeenu nyie CCM mliolaaniwa, mmeshindwa kazi na inapaswa kuacha demokrasia ichukue mkondo wake! Kama mtu ni shabiki wa chama pinzani why should that be your issue? Are you ready to compromise the scarcity of lecturers in UDSM by letting a competent Prof. Baregu out of teaching? Where is the brain here? Are there any explanations you can give? au ni wajinga flani kama wakina Makamba ndo wanaamua who to be employed and who to be sent packing! Huyo Makamba ana hata diploma basi? For sure you will saw what you planted soon!

walaaniwe mara ngapi aiseee.... waangalie braza wao wa-kubembea anavyojichora cku hizi...kila cku anatema dusty akijitahidi sana basi shudu kama sio vumbi...utafikiri hana washauri...!!!
 
Back
Top Bottom