WOS,
mojawapo ya maeneo ambayo hawa chagaz wanpendeleana ni kwenye ajira.
nitakupa mifano michache tu,kama kuna mwingine mwenye ushahidi ataweka hapa, kama kuna asiyeamini,afuatilie kunakohusika ili ajiridhishe.
Nenda Barclays bank na Swissport (T) ltd.Hayo ni maeneo mawili ambayo nimefuatilia na kujiridhisha kuwa bila kuwa chagaz au kujuana na chagaz wa hapo hulambi ajira.moja katika hizo mbili, moja waliwahi kutangaza nafasi za kazi ya mhandisi(engineer).nakumbuka tuliofanyiwa usaili tulikuwa 12,nafasi za kazi zilikuwa 3.Baada ya usaili watu watatu tukalamba ajira.nilipoanza kazi, kila ninayeongea naye anataka kujua mimi ni mchaga wa wapi.hiyo ilinishangaza sana.lakini hiyo ilikuwa tisa, kumi ni hivi: baadae nilikuja kubaini kuwa wale wenzangu wawili tuliopata nao kazi ni mafundi mchundo(FTCs).nikajiuliza kulikoni??wahandisi wengi hata niliosoma nao wamekosa kazi halafu wameajiriwa mafundi mchundo???baadae nikaja kubaini kuwa wale wenzangu watatu wote walikuwa chagaz na walipata upendeleo kwa kuwa kwenye panel ya usaili, ya watu sita, watano walikuwa chagaz.
na kwa uzoefu nilioupata hapo, ndio maana nasema chagaz wana safari ndefu sana ya kujirekebisha na huo ukabila wanaoendekeza.
Naomba nikukumbushe mheshimiwa kwamba kun cases ambazo huwezi ku-prove kitu kwa mfano, hasa unapotaka ku-prove kwamba dai litakuwa la kweli kwenye situations zote. Ila ku-disprove unahitaji kamfano kamoja tu.
Tunatumia mifano kuzipa uzito argument zetu tu.
Sina uhakika unachotaka ku-prove ni nini lakini naona posibilities mbili.
Moja
Unataka ku-prove kwamba "wachaga wote ni wakabila maana wachaga wote huwapendelea wachaga wenzao kwenye ajira".
Kwa hili pengine unahitaji zaidi ya mfano kuthibitisha.
Pili
Unataka ku-prove kwamba "wapo wachaga ambao ni wakabila ambao huwapendelea wachaga wenzao kwenye ajira".
Kwa hili pengine unahitaji mfano mmoja tu kuthibitisha.
Likini kuonyesha kwamba katika taasisi fulani kuna wachaga wengi nadhani sio mfano tosha. Ila ukija na mfano wa interview ambayo mtu asiye mchaga na mwenye sifa ameachwa akachukuliwa mchaga asiye na sifa kama zake kwa sababu ya kupigiwa debe na bosi mchaga, then huo utakuwa mwanzo mzuri katika kuthibitisha imani yako.
Na baada ya kuthibitisha hilo, (na kama nilivyosema kabla), sioni kama itakuwa shida kutumia mantiki hiyo hiyo ku-prove kitu hicho hicho kwa makabila mengine. Na unaweza utakuta "wapo [tumbukiza kabila lako hapa] ambao ni wakabila ambao huwapendelea [tumbukiza kabila lako hapa] wenzao kwenye ajira" pia inaweza kuwa kweli kwa kila kabila duniani.
Kuhusu uzoefu wako
Huwa najisikiaga mgumu kidogo kuamini kitu kwa sababu kuna mtu kaniambia. Na sababu ya msingi ni kwamba napenda kuepuka majungu.
Naamini sana kwenye hesabu na sayansi, na majungu mwiko.
Kama unakumbuka tulipokuwa shule za chini kuna kitu tulimegewa wengine wanakiita "Scientific Methods":
1. Observe
2. Formulate hypothesis
3. Experiment/Investigate/Research
4. Conclude
Wewe ulichofanya hapo ni:
1. Ume-observer: kwamba kuna mafundi mchudo waliopewa kazi zisizowahusu; hawa mafundi mchundo ni wachaga; watano kati ya sita katika masaili yao walikuwa ni wachaga;
2. Ukatengeneza hypothesis: kwamba walipendelewa na wachaga wenzao kupata hizo ajira.
3. Experiment/Investigate/Research: Ukairuka (au umesahau kutuambia)
4. Conclude: ukahitimisha kwamba walipendelewa na wachaga wenzao kupata hizo ajira.
Sasa mimi siwezi kujua kama ni kweli au si kweli kwamba wamepewa hizo ajira kwa ukaila. Lakini pia hinsi yako ya kufikia hitimisho hainiridhishi kwamba hitimisho lako linaweza likawa na ukweli.
Nikilichukulia hitimisho lako kama jungu tu usikasirike, ila tumia hiyo kama changamoto ya kutafuta ukweli wa nini kilitokea kwenye interview zao. Ukikuta kulikuwa na interviewee engine wenye sifa na waliachwa, au hao mafundi mchundo kazi wanaifanya kwa ufanisi mdogo zaidi kuliko nyie wenye fani zenu au pengine hawakuwa wanajua kazi kabisa ikabidi nyie wenye kazi zenu ndio muwafundishe, ... pengine unaweza ukawa na case nzuri zaidi. Na hapa hata waweza kumshtaki mtu. Nadhani sheria za nchi haziruhusu ubaguzi, ama?