Mzalendo
Senior Member
- Mar 10, 2006
- 181
- 32
Kaka thanks huyu jamaa ni kichwa na uwezo wake aufichiki, kapigwa mizengwe yetu yakitanzania full stop, hii nchi naona bora waliokwepo milembe wanajijua wao vichaa sie wengine tumebaki tupo tupo tuMkuu,Inapokuja kuhusu Dr Idrissa huyu mtu kuna mapungufu anayo ila kiuongozi he is a person with credible image and highly professional. Mie namfahamu tangu NBC alikuwa mtu asiyependa mtu aonewe ofisini, anayependa usawa (hasa kwa wafanyakazi wa chini), mtu wa sala tano (nakumbuka kuna vikao NBC vikiifanyika ijumaa akawaambia jamaa wabadilishe utaratibu kwani ilikuwa ni siku anaenda kusali na hakupenda akose vikao hivyo). Kiufupi alikuwa ni mtu muadilifu na mwenye kutetea maslahi ya wanyonge. Ndio maana wakurugenzi wenzie walafi hawakuwa wakimpenda kwani alikuwa hapendi ufisadi.BOT alisafisha uchafu uliomo kiasi watoto wa vigogo waliotumwa kulinda maslahi ya baba zao pale walikuwa wakiona cha moto, amesaidia kuifanya banking system ya tanzania iwe ni stable kwa kuhakikisha ule utaratibu wa vimemo na wanasiasa kuingilia taratibu na uendeshaji wa kibenki zinapotea. Alifinya mianya ya ufisadi pale BOT (hata scandal ya radar SFO wamemtuhumu isipokuwa nilitarajia wangelimfikisha mahakamani ndio tungelijua ukweli uko wapi) ijapokuwa sina uhakika kwani naye binaadamu na hakuna mtu msafi.Tanesco aliendeleza rekodi yake aliyotoka nayo nyuma kwa kusafisha ufisadi uliokuwa unaendelea pale Tanesco. Baadhi ya wakurugenzi na wanasiasa hawakupenda hilo kwa sababu wajuazo wenyewe. Waulizeni wafanyakazi wa kawaida wa Tanesco wanamuonaje Dr Rashidi ndio utakapopatwa na mshangao ila viongozi wenzie walikuwa hawampendi. Ndio sababu aliamua kukaa pembeni awaachie shirika liwafie wenyewe.Ukisoma thread moja ilianzishwa na Tausi Mzalendo utafahamu kuwa tatizo la umeme nchini sio vyanzo vya umeme bali Tanesco inasumbuliwa na gonjwa sugu la UFISADI!!!! Mtu kama Dr Rashidi anakuwa left in the middle of the mess. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema If you think education is expensive try ignorance ndio matokeo ni haya umeme tunakatiwa masaa 24 na watu tunabakia bado tunavumilia, senegal wametangaziwa mgao tu wameandamana, kweli sisi watanganyika ni watu wavumilivu sana!!!!!