Kwanini na ni namna gani Dr Idrissa Rashidi aliondoka TANESCO?

Bolivar

JF-Expert Member
Oct 23, 2010
229
103
Nimemkumbuka Dr Idrissa baada ya mgao huu mkali wa umeme.

Kufuatia rekodi yake nzuri akiwa BOT na kwa mujibu wa watu waliofanya naye kazi TANESCO Dr Rashidi ninaamini aangepewa mamlaka ya kutosha na rasilimali angeweza kuligeuza shirika hili kufanya kazi kwa ufanisi na sina shaka tatizo la umeme linalotukabili sasa lisingekuwa kubwa kiasi hiki.

Binafsi namuona Dr Rashidi kama mtu mwenye vision na anayeweza kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia.

Ni kwa nini Dr Rashidi aliondoka/aliondolewa TANESCO ilihali alikuwa mtu muafaka to turn around this Company?

Naomba kujua wadau!
 
TAtizo ni kubwa na sio dogo kama unavyofikiria. Shirika limeshahujumiwa vya kutosha. Pesa karibu yote inayopatikana kwa siku ni kulipa madeni yatokanayo na mikataba iliyopewa jina la " best practice". Siasa za kiafrica(ubinafsi)na utendaji vitu viwili tofauti.
 
Nimekugongea senks.

Chini ya Idrissa, hali tuliyonayo isengeweza kukatiza. Hii ndiyo tofauti ya Kiongozi anayeendesha kwa kutafuta matokeo na Kiongozi anayeogoza kwa kufuata taratibu tu.
 
I think he is among the outstanding Tanzanians, YES tatizo ni kubwa lakini with brains kama za Dr Rashid lisingefikia this magnidute!
 
Mbona inasemekana ni kilaza? au watu wamenimislead?

Jamaa ni smart sana, kwa mujibu wa watu wa BOT wakati wake hakukuwa na upuuzi, alipoingia aliwaambia wazi anajua kuna watoto wa vigogo kibao pale ila if they can deliver hana shida kama hawawezi mlango uko wazi waondoke. Kati ya aliowatimua kwa kushindwa kazi ni Malima naibu waziri!
 
Huyo Jamaa ni kichwa no wonder Mkapa akamuondoa akamuweka swahiba wake Ballali na wote mliona kilichotokea.

The moral of the story is wanasiasa wa tanzania ndio wanatukwamisha. Mtu kama Dr Rashidi alikuwa anasema ukweli kwamba shirika limechoka na pesa hakuna. Wanasiasa wanaogopa Ikulu , jeshini na Zanzibar kukosa umeme.Alivyoona hawamsikilizi akajiweka pembeni kimya.

Kituko cha kwanza kabisa alichokikuta DR Rashidi pale Tanesco ni kukuta Chairman wa Bodi Mr Balozi naye eti ana ofisi pale anakuja kazini kila siku na anahudumiwa kama mfanya kazi.Sasa huo kama sio ujuha ni nini??????

What a pathetic situation we have in this country!!!
 
He did make a lot of 10% during his tenure, so he's rich he was in Tanesco from Bank of Tanzania... so he collects some Greens and leave as every other official in that Government after Azimio la Zanzibar no one cares about the country called Tanzania.

NO ONE GAVE A DAMN ANYMORE WHO CARES!!!
 
Huyo Jamaa ni kichwa no wonder Mkapa akamuondoa akamuweka swahiba wake Ballali na wote mliona kilichotokea. The moral of the story is wanasiasa wa tanzania ndio wanatukwamisha. Mtu kama Dr Rashidi alikuwa anasema ukweli kwamba shirika limechoka na pesa hakuna. Wanasiasa wanaogopa Ikulu , jeshini na Zanzibar kukosa umeme. Alivyoona hawamsikilizi akajiweka pembeni kimya.

Kituko cha kwanza kabisa alichokikuta DR Rashidi pale Tanesco ni kukuta Chairman wa Bodi Mr Balozi naye eti ana ofisi pale anakuja kazini kila siku na anahudumiwa kama mfanya kazi.Sasa huo kama sio ujuha ni nini??????

What a pathetic situation we have in this country!!!

Hivi kumbe jamaa aliamua kuondoka mwenyewe?
 
Nimekuwa nikiangalia kwa muda mrefu kwa jinsi gani Watanzania wanavyoipenda nchi yao hususani katika uchangiaji wa mada mbalimbali hapa ndani.

Mimi naungana na watu ambao wanamuelewa Dr. Idris Rashid kwa utendaji wake mzuri na wa hali ya juu. Lakini napenda kuwakumbusha kwamba katika kupambana na matatizo ya umeme nchini, mipango yake mbalimbali iliyokuwa na mwongozo wa kulikwamua shirika ilipingwa na baadhi ya waheshimiwa.

Wanasiasa wanaopewa mamlaka ya usimamiaji mashirika ya umma kupitia vyombo mbalimbali nao ni tatizo kubwa hasa wanapoweka maslahi yao mbele.

Umuhimu wa maslahi ya waheshimiwa hawa ndio uliomfanya Dr. Idris aamue kukaa pembeni ingawa alikuwa TANESCO kwa mkataba.
 
Kati ya maamuzi ambayo sikumwelewa ni pale abapo alitangaza kujiuzulu baada ya amri yake ya kukatia umeme kiwanda cha sementi (tanga),halafu akabatilisha uamuzi wake huo
Kati ya vitu vingine ambamo jamaa ametajwa sana kuhusika ni yeye na chenge ktk ununuzi wa rada kwa bei ya kuruka,na wakati huo akiwa BOT
 
Nimemkumbuka Dr Idrissa baada ya mgao huu mkali wa umeme. Kufuatia rekodi yake nzuri akiwa BOT na kwa mujibu wa watu waliofanya naye kazi TANESCO Dr Rashidi ninaamini aangepewa mamlaka ya kutosha na rasilimali angeweza kuligeuza shirika hili kufanya kazi kwa ufanisi na sina shaka tatizo la umeme linalotukabili sasa lisingekuwa kubwa kiasi hiki. Binafsi namuona Dr Rashidi kama mtu mwenye vision na anayeweza kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia.

Ni kwa nini Dr Rashidi aliondoka/aliondolewa TANESCO ilihali alikuwa mtu muafaka to turn around this Company?

Naomba kujua wadau!

Mkuu,

Inapokuja kuhusu Dr Idrissa huyu mtu kuna mapungufu anayo ila kiuongozi he is a person with credible image and highly professional. Mie namfahamu tangu NBC alikuwa mtu asiyependa mtu aonewe ofisini, anayependa usawa (hasa kwa wafanyakazi wa chini), mtu wa sala tano (nakumbuka kuna vikao NBC vikiifanyika ijumaa akawaambia jamaa wabadilishe utaratibu kwani ilikuwa ni siku anaenda kusali na hakupenda akose vikao hivyo). Kiufupi alikuwa ni mtu muadilifu na mwenye kutetea maslahi ya wanyonge. Ndio maana wakurugenzi wenzie walafi hawakuwa wakimpenda kwani alikuwa hapendi ufisadi.

BOT alisafisha uchafu uliomo kiasi watoto wa vigogo waliotumwa kulinda maslahi ya baba zao pale walikuwa wakiona cha moto, amesaidia kuifanya banking system ya tanzania iwe ni stable kwa kuhakikisha ule utaratibu wa vimemo na wanasiasa kuingilia taratibu na uendeshaji wa kibenki zinapotea. Alifinya mianya ya ufisadi pale BOT (hata scandal ya radar SFO wamemtuhumu isipokuwa nilitarajia wangelimfikisha mahakamani ndio tungelijua ukweli uko wapi) ijapokuwa sina uhakika kwani naye binaadamu na hakuna mtu msafi.

Tanesco aliendeleza rekodi yake aliyotoka nayo nyuma kwa kusafisha ufisadi uliokuwa unaendelea pale Tanesco. Baadhi ya wakurugenzi na wanasiasa hawakupenda hilo kwa sababu wajuazo wenyewe. Waulizeni wafanyakazi wa kawaida wa Tanesco wanamuonaje Dr Rashidi ndio utakapopatwa na mshangao ila viongozi wenzie walikuwa hawampendi. Ndio sababu aliamua kukaa pembeni awaachie shirika liwafie wenyewe.

Ukisoma thread moja ilianzishwa na Tausi Mzalendo utafahamu kuwa tatizo la umeme nchini sio vyanzo vya umeme bali Tanesco inasumbuliwa na gonjwa sugu la UFISADI!!!! Mtu kama Dr Rashidi anakuwa left in the middle of the mess. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema If you think education is expensive try ignorance ndio matokeo ni haya umeme tunakatiwa masaa 24 na watu tunabakia bado tunavumilia, senegal wametangaziwa mgao tu wameandamana, kweli sisi watanganyika ni watu wavumilivu sana!!!!!
 
Mkuu, huu uvumilivu unatugharimu sasa
 
Kuna wakati mwanasiasa mmoja wa Kambi ya Upinzani aliwahi kusema Watanzania ni watu wa ajabu sana, "Umeme ukikatika wanafurahia na Umeme ukirudi wanafurahia pia" kuwabadilisha watu altitude si kazi ndogo.
 
..Dr.Rashid alituhumiwa ktk ripoti ya kamati ya bunge iliyoongozwa na Edward Ayila kuhusika na ufisadi uliofanyika BOT.

..baada ya hapo akateuliwa kuwa DG wa NBC ambako inasemekana alifanya kazi nzuri ya kurekebisha benki hiyo.

..kutokana na utendaji wake NBC akawa-promoted kwenda kuwa Govenor wa BOT kulekule alikokuwa ametuhumiwa kwa ufisadi.

..alipofika BOT akahusika na kashfa ya ununuzi wa rada with Chenge, na kujichotea pesa yeye na Sumaye toka NPF.

..utendaji wake pale Tanesco haueleweki-eleweki, kwa mfano alingangania sana kununua mitambo ya Dowans, badala ya kujielekeza kununua mitambo mipya. halafu alipoona mawazo yake hayakubaliki he didnt give a chance kwa mawaza mbadala yaliyokuwa yanatolewa. kwa mtizamo wangu ni kama alikuwa anasubiri crisis itokee halafu aseme "..I told you so..."

..I do not deny kwamba he is very SMART lakini sifa hiyo inakuwa negated na ushiriki wake kwenye UFISADI.
 
Hii ndiyo namna 99.999% ya waTZ wanavyofikiria. Fisadi, Fisadi, fisadi....

Mtazamo wa namna hii unajenga jamii ya watu wasioweza kufanya lolote. Wanabaki kuangaliana, nani anafanya ufisadi. Mwishoni mnakuaja hata kusingiziana wasio na hatia.

Tuko tayari kuwavumilia watendaji wabovu wasio na ufanisi eti tu kwa sababu siyo mafisadi. Wewe unamjua fisadi anafanana vipi lakini?
 
Back
Top Bottom