Kwa nini Mwanza/Kanda ya Ziwa kusiwe na Kituo Cha kukusanya Maoni?

Ccm inafahamu kuwa hali yao ya kisiasa kanda ya ziwa sio nzuri.kanda ya ziwa ni moja ya kanda inayoongoza kwa kuichoka ccm.ndio maana wameweka vituo vya kukusanyia maoni huko kwa waswahili ambako ccm inakubalika. Tunajua ccm kimebaki kuwa chama cha waswahili. Wastaarabu wamekichoka.
 
ccm ifahamu kwamba kila kukicha wanazidi kujimalizia umaarufu .Mambo wanayofanya ni ya kihuni sana kiasi kwamba hayaingii kwenye akili za watu wastaarabu. ccm inatuudhi sana kwa mambo yake ya mzaha mzaha kwenye mambo ya msingi.Katiba ya nchi sio jambo la kufanyia mzaha.Nafikiri ccm haina dhamira nzuri na hii nchi yetu.
 
Wananchi wanaoitaji kutoa maoni kuhusu mchakato wa kuanzisha katiba mpya ni wengi,hivyo haikuwa haki kwa serikali kuweka vituo viwili tu vya kukusanyia maoni.
 
Asanteni wadau kwa kuonyesha concern kubwa kwa hili suala la msingi kwa Taifa letu. Tuendelee kupambana tu kwa hizi hoja za kujenga, natumaini mwiso wake utakuwa katiba inayotokana na sisi wenyewe.

Sidhani kama chama tawala kitaweza kuteka hoja hii kama wanavyotaka kufanya sasa hivi. Kwanza ikumbukwe kuwa hii haikuwa hoja yao, wala haipo kwenye ilani yao ya uchaguzi mkuu uliopita, hivyo tendo la kutaka kuiteka ni kutapatapa tu kwa mfa maji, wenye hoja wako makini na wataisimamia mpaka mwisho,...hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
Ccm inaogopa mabadiliko.inajitahidi kuyazuia lakini ipende isipende mabadiliko ni lazima.ccm ifahamu kwamba wananchi wa mwaka 2011 sio wale wale wa mwaka 1970.
 
Ccm ifahamu kwamba kila kukicha ndivyo inavyozidi kuwaudhi Watanzania na kujipotezea umaarufu.Ccm inafanya mambo ya kihuni sana na ambayo hayaingii akilini. Ccm acheni kufanya mizaha kwenye mambo ya msingi.Katiba ya Nchi sio jambo la kufanyia mzaha.Naomba niwakumbushe Ccm kusoma alama za nyakati, bila hivyo mtaiharibu kabisa hii nchi. Ccm ikumbuke kuwa Watanzania wa mwaka 2011 sio wale wale wa mwaka 1970.Tafadhali shirikisheni Wananchi wote katika kuandaa Katiba mpya.
 
Back
Top Bottom