Kwa nini Mwanza/Kanda ya Ziwa kusiwe na Kituo Cha kukusanya Maoni?

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
Wadau wanahoji? kwa nini?

mwanza ina zaidi ya 1/3 ya waTZ wote. kwa nini imetengwa? kwa nini tukusanye maoni kwa kutumia vijiwe vya waswahili wa Pwani tu?

wadau wanauliza.
 
Ukabila na ukanda hatutaki humu..................ni swali zuri lakini sio la msingi zaidi ni la kuwagawa watz......wewe ni sawa wale wanaosema wengi wape.......utawapa wengi hata km hao wengi ni vichaa?...........tuzungumzie utz kwanza
 
kwa hiyo watu wa mwanza/kanda ya zaiwa ni vichaa?

utanzania ni pale unapokuwa mswahili wa pwani tu?
 
Na wachaga,wanyakyusa,wahaya, wakisema hivyo nani atasikilizwa sasa?..............maana watu hao wana mbongo za maana....ndiyo maana sisi waungwana tunaishia kusema utanzania kwanza then usukuma/umwanza baadaye huko.........tubadilike
 
Kusema kweli kama tunalitakia Taifa hili mema wangetenga vituo kwa kanda, huu siyo ukabila au ukanda bali ni kupata japo michango ya mawazo kutoka sehemu yote ya Jamhuri. Kuwe na kanda saba:-
1) Kanda ya Pwani iwe Dar,
2) Kanda ya Ziwa iwe Mwanza,
3) Nyanda za Juu Kusini iwe Mbeya,
4) Kanda ya kati iwe Dodoma.
5) Kanda ya Kaskazini iwe Arusha
6) Kanda ya Magharibi iwe Kigoma
7) Zanzibar.
Hapa inaonekana kama Serikali (CCM) inaogopa jambo! Acha wachakachue lakini lazima nguvu ya umma itawashughulikia.
 
Wewe utakuwa umeeleweka sawa sawa kwani unazungumzia utaifa na hujazungumzia mkoa...........hili likifanyika itakuwa poa na ni mwanzo mzuri wa kupata katiba ya watz wote.........ila kwa kuwa kikwete na ccm wamelazimishwa na chadema kwa hiyo watafanya wajisikiavyo ili waendelee kujilundikia mavyeo..................

kusema kweli kama tunalitakia taifa hili mema wangetenga vituo kwa kanda, huu siyo ukabila au ukanda bali ni kupata japo michango ya mawazo kutoka sehemu yote ya jamhuri. Kuwe na kanda saba:-
1) kanda ya pwani iwe dar,
2) kanda ya ziwa iwe mwanza,
3) nyanda za juu kusini iwe mbeya,
4) kanda ya kati iwe dodoma.
5) kanda ya kaskazini iwe arusha
6) kanda ya magharibi iwe kigoma
7) zanzibar.
Hapa inaonekana kama serikali (ccm) inaogopa jambo! Acha wachakachue lakini lazima nguvu ya umma itawashughulikia.
 
Kama ambavyo CCM ilikubali kuanzisha mfumoo wa vyama vingi kwa shinikizo la wafadhili lakini moyoni mwao hawakuwa tayari kufuata mchezo safi wa demokrasia. Matokeo yake ni uchakachuaji, rushwa, ufisadi, vitimbwi, vitisho, halmuradi tu wanabakia madarakani. Ndivyo ambavyo wamekubali shinikizo la katiba mpya toka kwa wananchi bila ya wao kuwa tayari na hilo. Matokeo yake ni kutaka kutumwagia changa la macho. Mara hii hapana!
AIBU KWA SERIKALI!
AIBU KWA CCM!
AIBU KWA DEMOKRASIA!
AIBU KWA TANZANIA!
AIBU KWA AFRIKA!
INATOSHA!, INATOSHA!
 
Ukabila na ukanda hatutaki humu..................ni swali zuri lakini sio la msingi zaidi ni la kuwagawa watz......wewe ni sawa wale wanaosema wengi wape.......utawapa wengi hata km hao wengi ni vichaa?...........tuzungumzie utz kwanza

JILE acha ujinga na kupuuza hoja za msingi,lengo ni kukusanya maoni ya wengi na kama ndivyo,kwa nini kanda ya ziwa isiwe na uwakilishi wa maoni na pia haraka ya nini?.....
 
The Prophet,

..lugha uliyotumia haipendezi.

..pamoja na hayo madai yako ni ya msingi.

..ingependeza kama kungekuwa na kanda nyingi zaidi za kukusanya maoni ya katiba.

..kwangu mimi Dodoma na Dar hazitoshi.
 
Umenena kibusara zaidi, nafikiri tunahitaji uwakilishi wa maoni ya Watanzania wengine (wala haitakuwa na maana ya ukabila kama mwenzetu mmoja anavyofikiri). Katiba ni ya wananchi, waachwe wajimwage na maoni yao kadri wanavyoweza
 
Wadau wanahoji? kwa nini?

mwanza ina zaidi ya 1/3 ya waTZ wote. kwa nini imetengwa? kwa nini tukusanye maoni kwa kutumia vijiwe vya waswahili wa Pwani tu?

wadau wanauliza.

Mkuu takwimu yako yatoka wapi? Kwamba Mwanza ina 1/3 ya watanzania?
 
Unajua funny enough AG anatoka kanda hiyo hiyo. Au sababu ya wabunge wote wawili ni wa upinzani? Sijui hiki kitu ni nini na kitazaa nini!
 
point ya msing ni maoni yakusanywe kikanda aliezungumzia mwanza amezungumzia kanda mojawapo hvyo ni vyema wengine wakataja na kanda nyingine kama alivyofanya anko sam.
 
Kusema kweli kama tunalitakia Taifa hili mema wangetenga vituo kwa kanda, huu siyo ukabila au ukanda bali ni kupata japo michango ya mawazo kutoka sehemu yote ya Jamhuri. Kuwe na kanda saba:-
1) Kanda ya Pwani iwe Dar,
2) Kanda ya Ziwa iwe Mwanza,
3) Nyanda za Juu Kusini iwe Mbeya,
4) Kanda ya kati iwe Dodoma.
5) Kanda ya Kaskazini iwe Arusha
6) Kanda ya Magharibi iwe Kigoma
7) Zanzibar.
Hapa inaonekana kama Serikali (CCM) inaogopa jambo! Acha wachakachue lakini lazima nguvu ya umma itawashughulikia.

umenena mkùu wengne naöna wanaleta vumbi tu hapa.
 
The Prophet,

..lugha uliyotumia haipendezi.

..pamoja na hayo madai yako ni ya msingi.

..ingependeza kama kungekuwa na kanda nyingi zaidi za kukusanya maoni ya katiba.

..kwangu mimi Dodoma na Dar hazitoshi.
wanaogopa mikoa mingine/kanda nyingine mambo yatakuwa mabaya kwao, kwani darisalama na dodoma wengi wa wasomi ndio hao wafanyakazi wa serikali? wanaopewa rushwa kidogo ili wailinde serikali, na wengineo hawajui saana mambo ya katiba nk
hizo kanda zingine si ndio maandamano yalipamba moto?
 
Kuandaa mchakato mpaka kuandika Katiba ya nchi siyo jambo la mzaha kama CCM wanavyotaka kufanya. Katiba ndo mwongozo wa kuendesha serikali na ni dila ya mustakabali wa Taifa. CCM wamechelewa sana kwani watu wengi wamekwisha amka, hivyo kulazimisha mawazo ya kikundi kidogo cha watu kitumike kutengeneza Katiba, watasababisha ya Ivory Coast ama Kenya. Tunaelekea huko maana harufu ya damu nyingi kumwagika kwa mambo ya kisiasa inanukia 2015! Subirini mtaona!
 
Back
Top Bottom