Elections 2010 Kwa nini kimya hivyo utafikiri tuna msiba?

Mwalimu,
hjapa nakubaliana nawe kabisa. Sijui kama hawa watu wanaelewa ni jinsi gani wenzetu walifanya pinmdi walipokuwa wakipinga serikali zao au chama tawala. Ni majuzi tu waliyaona huko Zimbabwe jinsi wananchi wenyewe walivyokuwa wakiingia mitaani na kuweka upinzani. Lakini kwetu sisi imekuwa kama ni kazi ya Chadema kwa maisha yao wenyewe. Chadema awaletee Uhuru huo mezani kilichobakia wao ni kula maraha tu..

Wakuu zangu yawezekana kweli Chadema hawana PR pengine hawana watu wa kushughulikia maswala ya Utangazaji na mengineyo kibao wakati CCM mbali na Mafisadi wanatumia pia vifaa vya Taifa na watumishi wa serikali kujitangaza. Ifike wakati sisi wenyewe tukichukulie chama hiki Chadema kama ni chama chetu sote na sii cha Mbowe au Dr.Slaa. Unapoweka mawazo ya kusema Chadema hawafanyi kadhaa wa kadhaa ina maana wewe mwenyewe unajitenga na kusema chama kina wenyewe. Chadema ni wewe na mimi nawoote wanaotaka mageuzi.

Jamani inachukua kijiji kizima kumlea mtoto na Chadema ni mtoto wenu nyote, mkianza kuwaachia dhamana yote basi ni dalili ya kutofahamu kazi kubwa ya mageuzi inatuhusu sote na sii Chadema. Chadema ni tools ama nyenzo itakayotuwezesha kufanikisha azma tunayokusudia.. it's like a bus - means of transportation). Kwa hiyo zile fikra za Ujamaa kufuatwa na bus hadi nyumbani na kupigiwa honi ndio unajiandaa kwenda kazini ziondoke...Ni sisi tunaotakiwa kwenda kituoni na kulipanda bus on time, tukiwa ndani ya bus tutaimba, tushangilie na kupiga mayowe ya kuutaka ushindi.
 
Unachosema ni sahihi! Lakini umewahi kuona tangazo la CHADEMA linaomba watu kujitolea zaidi ya lile la michango? Nilitegemea CHADEMA wangekuwa na campaign hata za nyumba kwa nyumba, vijana wapo wanahitaji kuitwa tu na kuwekewa utaratibu! Licha ya hayo mapungufu bado njia rahisi kabisa ya kujinadi na kujitangaza (mtandao youtube na blogs) walengwa wakiwa wafanyakazi walioko maofisini havitumiki! Hapo halihitaji kujitolea waanzishe basi hata hiyo huduma watu wenye video clips na pics wawe wana-upload
 
Hapa ndipo tunapokosea..kwa nini iwe kazi ya Chadema wakati CCM wanaofanya ni wananchi wenyewe wakichangiua pasipo kuombwa na juu ya yote serikali ikitumia mali za Umma pasipo kuomba michango yenu vile vile. They do everything wrong lakini tunashindwa hata kulalamika isipokuwa tunasubiri siku ya Kupiga kura.

Kila JK anapokwenda matajiri hujitokeza na kutoa mabillioni hata bila kuitwa. Chadema hata mkutano wao nin lazima wapite na Helkopta ndio watu wajivute..as if tunawafanyia wao favor. Na tukianza kuifikiria Chadema kwa mtindo wa Marekani tuseme kama alivyofanya Obama utagundua kwamba haiwezi kufanyab kazi sawa kwani Obama aliwafuata wasomi, vijana graduates wanaotegemea kuwa workforce ya kesho wenye nguvu zaidi ya mvuto wa kura wakati McCain alitegemea wazee na veteran ambao mbinu zao zilipitwa na wakati..Lakini wote waliwalenga makundi ya watu hasa 1. Wazee, 2. Wanawake 3. Racial group na mwisho ndio vijana. Kikubwa zaidi kuliko yote wanajua kwa uhakika kila household ina TV, na sasa hivi PC kwa hiyo matangazo yanawafikiaje wananchi.

Ukija Tanzania, ukajaribu kutumia mbinu hizi utakwisha kwa sababu kwanza Diversity yetu bado haijakomaa ktk sekta zote, ukigusia tu maswala utapigwa vita hadi ukome. Ni asilimia chini ya 20 wenye hata tube TV zenye kitambi, acha hizo PC iweje utumie Youtube hali ni asilmia 1 ya wananchi hupitia Blogs tena kati yao asilimia 90 wanaishi Ulaya.

Tazama mikutano yote utaona ni vijana wana attend mikutano zaidi ya wazee wakati nchi za Ulaya ni mature middleage group na wazee ndio hushiriki zaidi ktk hotuba za wagombea. Sidhani kama Chadema hawapiti nyumba hadi nyumba katika sehemu wanazosimamisha wagombea wao Ila nina hakika CCM wamehakikisha uwanja wa mashindano hauko sawa. Wala sintashangaa kusikia kwamba CCM wanalipia kila inchi ya matangazo yao kiasi kwamba chama kingine hakiruhusiwi kuweka Tangazo lake juu wala chini. City wakishakamatishwa kidogo inawezekana usipewe kibali cha matangazo barabarani..

Naijua Bongo vizuri sana kiasi kwamba siwezi kuwalaumu Chadema pasipo kuelewa ni matatizo gani wanakumbana nayo na hakika hawana muda wa kuja hapa kuelezea Ukumbi hali hakuna hata mtu mmoja atakaye saidia kitu zaidi ya kuifanya mada yenye hoja za kuvutia zaidi. Majuzi tu Mnyika kaingia NEC kuweka malalamishi ya chama kuhusianana na Ahadi za JK..Amini maneno yangu watu wameyasoma hapa na kusema saaana kwa hoja kibao lakini ukweli ni kwamba hawakuchangia kitu chochote isipokuwa ni ktk mazungumzo ya kuvuta muda tukisubiri maamuzi ya Tendwa..

Usisahau tu - NDIVYO TULIVYO..
 
Yah! Mkandara Unazungumza Mambo ya Msingi sana, the ishu ni kwamba hakuna a level playing field, hakuna Muda wa Kulaumu bali kila mtu kwa nafasi yake afanye Kampeni
 
CHADEMA wawatumie vijana wa form sx leavers na wanavyuo walioko likizo
 
Uoga Wetu, ndo Umaskini wetu....
Tuamke Jamani.. tunakuja kuahidiwa meli wakati wa Uchaguzi.. na tunapiga tu makofi. bila kujiuliza walikua wapi.. tuamke...
 
Wakuu katika post yangu moja nilizungumzia hili kabla ya hata kampeni kuanza. Sababu nilishavitilia shaka vyombo vetu vya habari kuwa vingi vingejikomba kwa CCM, kwani wenye media hizo watawadirect waaajiriwa wao waipendelee CCM huku wao wakitegemea kulipwa fadhila ikiwa mkulu ataukwaa tena uprezida kwa awamu ya pili, na hivyo silaha ya CHADEMA ilitegemewa kuwa website yao, kwani wapo wanaosafiri na mgombea wanaweza wakapiga picha na kuapload video na CHADEMA kuwa na colum maalum ya kupokea maoni kwenye hiyo website yao, hii ndocho nilichosema, Lakini kama wadau wengine walivyosema speed ni ndogo sana na Octoba 31 haiko mbali, CHADEMA need to wake up now.
Kuna mdau anasema lazima tujiulize tutaifanyia nini CHADEMA kuliko kusubiri CHADEMA itufanyie nini, hili ni kweli. Lakini kwa mfano mimi ni mwajiriwa naishi Dar es salaam, sijapata nafasi ya likizo hivyo hilo jukumu la kupata picha na matukio ya kampeni ni hadi pale mgombea atakapo kuwa mkoani hapa, jukumu amabalo nitalitekeleza kwa makini. Lakini iko mikoa amabayo labda hakuna wana JF wapenzi wa CHADEMA, au hakuna kamera, jukumu hili linapaswa kutekelezwa na makamanda wa CHADEMA wanaozunguka na Mgombea.

Wana JF, siku hizi wala hupati tabu sana kufanya haya, unahitaji laptop ndogo tu, Modem na digital kamera. Hivi vitu ni simple, na kama modem iko moja ukinunua unatumia Mobile netork yoyote iwe ya Zain,Tigo,Zantel au voda achilia ile ya TTCL ambayo inabidi uwe na CDMA modem. hivi vitu ni simple sana na vyenye impact kubwa, lakini inabidi huyu mkurugenzi wa habari na Propaganda wa CHADEMA aonyeshe njia ili wenye nia tuifate. Tupeni basi hata ratiba za wagombea Ubunge majimboni, tujue ili tulete habari hizi, kodini basi hata kampuni binafsi ya Ku-run website katika kipindi hiki, au elezeni namna ya kualika VOLUNTIRES, tuko tayari jamani. Ukombozi wa Taifa hili sio kitu cha mchezo!!! WAKE up CHADEMA we need to fight and the time is now.
 
Ziko kazi nyingi za kufanya lakini CHADEMA hawana watu wengi. Inatakiwa sisi ambao tunataka waongoze mapigano ya ukombozi tuwaendee ili wawe na wafanyakazi wengi.

Mimi ningekuwa Tanzania ningesharipoti ofisini kwa CHADEMA na kusema here I am, send me. Ningekubali kupangiwa kazi, na hata kubuni kazi zenyewe na kuomba tu idhini yao kuzifanya kwa jina la CHADEMA. I have not been a member of a political party up to now, but when I go to Dar later this year, I will seek to be a card carrying member of CHADEMA. I am convinced they are the people we have been waiting for.

Mwenye website ya CHADEMA tafadhali aiweke hapa. Haifahamiki na kila mtu. Tusaidie kutangaza angalau hapa. Ama mnasubiri CHADEMA ifanye kila kitu, hata mpaka huku JF?
 
mkuu website ni hii hapa chini, tatizo ni kwamba hawa i-update na huu ndio ugomvi wetu sisi tunaotaka kussuport, sbb tunategemea tupate information zote hapo za namna ya kuvoluntier huku tuliko sababu wengine hatuko dar es salaam
Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
Back
Top Bottom