Kwa nini? Kadri siku zinavyokwenda Watanzania tunazidi kuwa WAJINGA

kimboka one

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
734
85
Mi ninajiuliza hili swali sana sipati jibu.kwa nini kila kukicha wtz tunakuwa wajinga,tunakosa UZALENDO na ubunifu.ninasoma historia ya Mkwawa hapa jamaa alikuwa na akili sana na UZALENDO wa hali ya juu.wajerumani walipata tabu kubwa kuliko sehemu nyingine walizo tawala.sijui kwanini? hakupewa nishani ya uhuru.hoja yng kwa nini? Kizazi hiki hakuna wa aina ya mkwawa?.kadri siku zinavyo kwenda ata watu aina ya slaa hawataoneka sijui nchi itakuwa je?. Au ni haya madawa,vipodozi,net,vyakula vya makopo na tv za ughaibuni?.nisaidieni wadau.
 
Hapana mi nakukosoa! Kila siku zinavyozidi kwenda Watanzania wanazidi kuwa na akili, wanaozidi kuwa wajinga ni Watawala wetu ambao wanafanya ujinga wa kuwatunuku nishani kina Bibi KIROBOTO wakata hata kazi aliyonayo imemshinda!
 
Ujinga umeu generelize lakini sidhani kama watanzania wengi ni wajinga. Wapo wazalendo, wenye hekima lakini hawapati nafasi ya kuonyesha vipawa vyao badala yake vichwa vya nazi aka panzi ndiyo vimepewa nafasi ya kuongoza.
 
je wewe ni mzalendo? Kama jibu ni ndio ni kitu gani cha maana ambacho umewahi kuifanyia nchi yako? Kama kweli unataka watz wabadilike anza wewe usiwe kibao cha matangazo
 
Hakuna kitu kinaudhi kama hii tabia ya kujidharau. Mara sisi watanzania ni wajinga, mara sisi watanzania hatuna uzalendo! Kwa vipi? Huu ni ukoloni wa ki-fikra. Tangu jana watu wengi wamekuwa wanachambua utoaji wa nishani na kuhoji vigezo vilivyotumika kuwapa baadhi na kuacha wengine. Sasa inakuwaje watanzania wote tujiite wajinga? Au ina maana ni watanzania wote waliokaa na kuandaa orodha ya wapewa nishani? psychological scar ni hatari zaidi kuliko physical scar. Ukikazania kumwambia mtoto wako kila siku kwamba yeye ni bure hawezi kitu anaweza kweli akawa bure kwa kukata tamaa.
 
Unategemea mtawala aina ya m.k.were afanye nini zaidi ya hayo anayoyafanya? Uwezo wake umeishia hapo

Hapana mi nakukosoa! Kila siku zinavyozidi kwenda Watanzania wanazidi kuwa na akili, wanaozidi kuwa wajinga ni Watawala wetu ambao wanafanya ujinga wa kuwatunuku nishani kina Bibi KIROBOTO wakata hata kazi aliyonayo imemshinda!
 
Mimi nadhani wewe ndio mjinga Watanzania ni watu wenye ufahamu wao na kujitambua!
 
Wajinga ni sisiemu na cuf tu nchi hii,wengine wote wana akili zao,namuunga mkono muanzisha mada kwani najua anamaanisha nini aliposema kwanini watanzania tunakua wajinga.
 
Kwenye ujinga hapana,watanzania si wajinga hata kidogo!Ila kwenye UZALENDO tuwe wakweli.Uzalendo nchi hii umeshuka sana sana!Huo ndiyo ukweli vinginevyo niwe sifahamu tafsiri sahihi ya neno UZALENDO!Hivi kwa mfano wale jamaa waliokuwa wanasukuma gari ya Jairo siku ile pale wizarani,tena walijikakamua hadi ushuzi ukawatoka utawaita wazalendo wale?Mungu apishe mbali itokee vita kama ile ya Kagera leo hii,ni nani yuko tayari kutoa nguvu,mali ama damu yake kuifia nchi hii?Hivi kijana wa leo utamshawishi vipi aende vitani wakati mwenyewe anaamini nchi imeshauzwa na yeye hakupewa mgawo wake?Ndugu zangu tusijifariji uzalendo sasa hivi haupo!THINK TWICE.
 
uko sawa watu wa aina ya Rumanyika,kimweli,mangi meli na mkwawa ni wachache sana na tunazidi kuwapoteza..
 
Kwenye UJINGA mie simo kabisaaaa, uzalendo ndio umepungua kidogo maana naogopa kupata ugonjwa wa presha, Tumemchagua Mkapa Mr. Safi akawa Mr. AnaBEM na Meremeta-Kiwila, sasa Kama huyu Mr. Dowans na Kagoda mnataka uzalendo gani? kama wewe mzalendo kweli kazifuate Pesa za Mr. Rada Mzee wa vijisent huko new jes..... si ulishaambiwa!
 
ngojeni jkt irudi,tatizo lenu mnaongea tu kwa kuwa wengi wenu hamkupitia national service!
 
ngojeni jkt irudi,tatizo lenu mnaongea tu kwa kuwa wengi wenu hamkupitia national service!

Mkuu sidhani kama JKT itaweza kurudisha uzalendo uliopotea!Tena vijana wa sasa walivyopinda wanaweza kuchoma moto makambi.Unajua tatizo ni kwamba watu wote hivi sasa wanaona jinsi mgawanyo wa keki ya Taifa unavyofanywa kwa kutokuzingatia usawa!Na hapo ndipo tatizo la watu kupoteza uzalendo linaapoanzia.
 
Mi ninajiuliza hili swali sana sipati jibu.kwa nini kila kukicha wtz tunakuwa wajinga,tunakosa UZALENDO na ubunifu.ninasoma historia ya Mkwawa hapa jamaa alikuwa na akili sana na UZALENDO wa hali ya juu.wajerumani walipata tabu kubwa kuliko sehemu nyingine walizo tawala.sijui kwanini? hakupewa nishani ya uhuru.hoja yng kwa nini? Kizazi hiki hakuna wa aina ya mkwawa?.kadri siku zinavyo kwenda ata watu aina ya slaa hawataoneka sijui nchi itakuwa je?. Au ni haya madawa,vipodozi,net,vyakula vya makopo na tv za ughaibuni?.nisaidieni wadau.

hapo kweney red.
Stay Foolish,
stay hungry

Steve Jobs (1955-2011)

hapo kwenye blue:
kila kila zama na kitabu chake, sii lazima watu woote wafanane otherwise the world would have been a very boring place to live! mkwawa had his weaknesses to and so is Slaa! just play your part all will be fine! and by the way, je, wewe una uzalendo? (remmember it begins with you)
 
Watanzania si wajinga, ni kwamba wamebanwa na vingunge vya ufisadi. Wanaowachezesha music wanaotaka wao kwa kutumia pesa uchwara pamoja na nguvu za dola!!!
 
je wewe ni mzalendo? Kama jibu ni ndio ni kitu gani cha maana ambacho umewahi kuifanyia nchi yako? Kama kweli unataka watz wabadilike anza wewe usiwe kibao cha matangazo
Nimefanya mengi kulingana na umri wng na elimu yng au mawanda yng ya kuwafikia.kubwa kuwaelimisha watanzania kudai haki yao na kuacha ushabiki.kimsingi unahitaji utambulisho wangu kamili ili upate rejea si maneno tu
 
Hakuna kitu kinaudhi kama hii tabia ya kujidharau. Mara sisi watanzania ni wajinga, mara sisi watanzania hatuna uzalendo! Kwa vipi? Huu ni ukoloni wa ki-fikra. Tangu jana watu wengi wamekuwa wanachambua utoaji wa nishani na kuhoji vigezo vilivyotumika kuwapa baadhi na kuacha wengine. Sasa inakuwaje watanzania wote tujiite wajinga? Au ina maana ni watanzania wote waliokaa na kuandaa orodha ya wapewa nishani? psychological scar ni hatari zaidi kuliko physical scar. Ukikazania kumwambia mtoto wako kila siku kwamba yeye ni bure hawezi kitu anaweza kweli akawa bure kwa kukata tamaa.
mkuu utaendelea kuudhika tu! Kwa ukweli huu
 
labda watu hakunielewa chukua mfano wa hesabu hii rahisi na tazama majibu ya kama si ujinga ni nini?. 1.madini+mafuta+makaa ya mawe+vivutio+aridhi nzuri+nyanda ya maji+watu=UMASIKINI 2.Kwa wiki karibu migodi yote tz hakuna ambao unazalisha chini ya tani moja kwa wiki kwa aina ya madini husika,mfano gold ikiwa kiwandani inauzwa m 90 kwa kilo mara 1000 ni shilingi ngapi?.na sisi tunabaki na ngapi?.na kwa nini ni masiki mpaka sasa?.huu si ujinga?,kama walifanya wakina cheif mangunga?, kubadilisha dhahabu kwa vioo au kwa net na mradi wa pango uzazi au kunawa mikono?.aaah inaudhi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom