Kwa nini JK amezunguzungumzia Mgomo wa Madaktari?

mvunjamiwa

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
453
116
Katika vikao vya Bunge linaloendelea Dodoma, Wabunge wamezuiliwa kujadili jambo lolote linalohusiana na mgomo wa Madaktari na Spika wa bunge kwa sababu kuwa kesi ipo Mahakamani hivyo bunge haliwezi kuingilia Mhimili mwingine wa dola (Mahakama).

Kama kuna ukweli katika hilo ni kwa vipi Rais ameongelea suala la madaktari tena kwa kirefu sana katika hotuba yake. Je, Rais yupo juu ya sheria? Ana uhuru wa kuingilia Mahakama?

Ni kwa nini Wabunge wasiruhusiwe pia kuzungumzia jambo hilo tupate upande wa pili wa mambo yaliyojificha?
 
Yaani we acha hii nchi imejaa madudu kutoka kwa Serikali yetu hadi aibu,ukiwaambia kwamba wao ni dhaifu wanalalama. Spika yule si spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa TZ ni spika wa bunge la CCM na hakika kabla hajaingia pale anaambiwa leo hakikisha A,B,C,D na si vinginevyo!
 
Hii wanayoita sijui mihimili hapa Tanzania ni kichefuchefu sana.Kama suala liko mahakamani ilikuwa ni busara sana kutokuingiliwa na mhimili wowote.Kazi bado ipo, Mkuu maji yako shingoni
 
Tena rais ambae ndie jemdari mkuu wa majeshi yetu anadai kuwa serikali haijahusika na kumdhuru Dr. Ulimboka wakati huhuo kaagiza vyombo vyake kufanya uchunguzi kujua ukweli juu ya hilo. Haoni kuwa hao waliotumwa sasa wanajukumu la kujustify statement ya boss wao na sio kuja na kitu kinachoweza kwenda kinyume na statement hiyo. Tunaongea maneno matamu midomoni yasiyo na muunganiko wa fikra tulizonazo
 
kweli jk ni dhaifu, anajaribu kuzima moto bila ya kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu huu mgomo. madk wanaweza kurudi na kuanza mgomo baridi km walimu . Wananchi tuamke kuibana serikali ama sivyo ni sisi ndo tutataumia zaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom