Kwa nini JK Alishtuka na KUSHANGAA Sana PINDI Wabunge wa CHADEMA Walivyotoka Bungeni

Kweli Tatizo lililopo ndani ya CCM ni kuwa viongozi hawataki kabisa kukubaliana na ule usemi wa Mwl.Nyerere aliwaeleza kuwa 1995 "vyama vya upinzani vilikuwa ni vichanga lakini wanatakiwa wajifunze kuiendesha nchi katika mfumo wa vyama vingi"

Sasa hapo ndipo viongozi wa CCM ndipo walipo kosea njia wakabweteka hawakujua mambo yanakuja kwa kasi na sasa haya hapo usoni kwao wanashindwa jinsi ya kujinasua kinachobakia wao wanataka kujihararisha kuwa waondio wateule wa nchi hii na wengine sio tena kwa mabavu. Itawagharimu sana kawa hawatojipanga mifano mizuri KANU ya kenya leo iko wapi choko choko kama hizi zilianza hivi hivi 1993 FORD Kenya ya kina Jaramogi Odinga Oginga walimgomea Moi kwenye bunge wakatoka nje na matokeo yake KANU ilikufa na vurugu zikaja mpaka sasa wamepata katiba mpya kwa kumwaga damu baina yao kwa wao na ndani ya vyama vyao na ndio hiyo viongozi wa CCM wanaikaribisha sasa

Serikali inatakiwa ilichukulie hili jambo kwa umakini zaidi wasilifanyie mzaha
mifano mingi tu kwa majirani zetu sio kuwa sio ni binadamu kamili hapana nasi tuna mapungufu yetu. na Tuyatatue

Ndugu yangu CCM kufa ni lazima, ni kama sikio la kufa! Halisikii dawa!

Unapoteza dawa zako bure!
 
Maggid huwa anauma na kupuliza bana subiri week ijayo atakuja na agenda nyingine itaudhi tu lakini leo sitaacha kukupa kacredit kadogo kwa article yako.
 
Ama kweli sisi Watanzania ni wepesi sana kusahau na mfano hai ni kwenye hii thread,Majjid huko alipo labda anacheka akisoma hizi posts mpaka jino la mwisho linaonekana.Makala zake sasa hivi mtaanza kuzisoma kwa kwenda mbele halafu 2015 deja vu.
 
Ndugu zangu,

Nilipita Dodoma siku mbili kabla ya JK kuhutubia Bunge. Nilizisikia, fununu za uwezekano wa kutokea kwa tukio lile.

Juzi limetokea, Wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, mbele ya Rais wa nchi, mbele ya wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa, Mabalozi na wengineo. Si habari mpya sana, ilitarajiwa, kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa. Tutayaona mengi mengine.

1. Baada ya tukio lile nilitarajia Rais angesonga mbele na hotuba yake bila kugusia jambo lile.
Hilo la mwisho lingewasumbua sana CHADEMA. Hapana, Rais akagusia tendo lile. Katika nchi, Rais ni mmoja, lakini, kazi ya Urais ni ya wengi. Najiuliza, je, wasaidizi wake hawajua kabla kwamba lililotokea lingeweza kutokea ? Kama walilijua, basi, wangemsaidia Mkuu wa Nchi na kama hawakulijua, nalo ni tatizo.

Nani mshindi?
2. Katika siasa, lililotokea Dodoma ni sehemu ya mapambano ya kisiasa katika mfumo wa vyama vingi. Chama tawala hakina sababu ya kuogopa. Kianze sasa kuyazoea mazingira haya mapya. Tunachokiona ni mchezo wa kisiasa ambao, kama mechi ya mpira, unahitaji team work na wachezaji mahiri katika kufanikisha ushindi. Maana, tukio lile, kwa wakati huu, limeliongezea ponti kadhaa za kisiasa CHADEMA.

3. Watanzania wamelifuatilia, Jumuiya ya Kimataifa imelifuatilia. Ajenda ya haja ya uwepo wa Katiba Mpya imeharakishwa kufikishwa kwa umma katika kasi ambayo haikufikiriwa. Watu wanajadili. Ni ajenda ya umma kwa sasa, CCM wakibaki nyuma, CHADEMA wataonekana kwa umma ndio wenye dhamira ya kweli ya kuwasaidia.

Naam. Katika dakika hizi za mchezo huu wa kisiasa, CCM imerudishwa nyuma kwenye lango lake, wanajihami. Na kuna wanaojiuliza nani mshindi? Mchezo bado unaendelea, tusubiri tuone!

Maggid
Arusha,
Novemba 20, 2010

mjengwa

- Ndugu yangu Majidd, heshima sana article yako iko sawa sana isipokuwa somehow umekua too excited na kuwahi sana mbele ya wakati, kwenye hoja namba moja uko sawa sana, Rais hakupaswa hata kuligusia hili tendo kwa kuligusa amewapa wabunge waliomsusia political attention waliyokuwa wakiitafuta kwake, that was wrong maana hapo inaweza ika-send a message kwa vikundi mbali katika jamii kwamba all it takes ni kususia tu hotuba ya Rais and you get the Presidency Institution's Attention.

- Uko sawa sana, unaposema CCM wajifunze kukubali vitu kama hivi kwamba ni vya kawaida sana katika Demokrasia, isipokuwa kwenye hoja ya kubadili katiba kwa sababu ya hiki kitendo, hapo ndipo mkuu umechemka yaani umekua too excited bila ya kua realistic, kama kweli taifa letu tutabadili katiba kwa sababu ya wabunge 46 kususia hotuba ya Rais, basi hili taifa wote tutakua out of our minds.

- Katika siasa inakubaliwa kuwa na behind the scene moves za pande zote mbili ku-deal na ishu ya NEC, lakini kwa serikali ya CCM kuanza kuhaha na kuhangaika huku na kule kisa wabunge 46 tu wamesusia hotuba ya Rais, itakua inajisema wazi kwamba hili taifa hatuwahitaji kututawala tena. Fairness ya siasa za vyama vingi itakuja pale tu tutakapokuwa na strong upinzani, otherwise ni kupoteza muda tu maana sasa hivi hata ukipeleka muswaada wa mabadiliko ya katiba on NEC unahitaji wabunge wa CCM kuipitisha na huwezi kubadili katiba ya Jamhuri popote isipokuwa bungeni, sasa wabunge 46 wanabadili vipi katiba ya Jamhuri?

- Hivi ni vita vya kisiasa tu kati ya vyama hivi viwili kwa ajili ya the public affection na I hope CCM watakua makini sana ku-read this situation for what it is badala ya kushiriki kwenye kulipeleka hili taifa kusiko takiwa, Wabunge wanaosusia waachwe waendelee kama walivyo, in the meantime vyama vyote viwili viendelee kulumbana on the ishu, halafu sisi wananchi ndio tutaamua nani ni nani, lakini ushauri kwamba sasa katiba ya Jamhuri ibadilishwe kinyume na sheria zetu kwa sababu ya hii very minor political presssure, CCM ikikubali hilo itakua inajichimbia kaburi lake 2015.

- CCM wasimame juu sasa mbele yetu wananchi wa Tanzania watuelimishe mapungufu ya hoja za Chadema kuhusu matokeo ya huu uchaguzi, watuelimishe kwamba hawahusiki na NEC na kwamba hicho ni chombo huru, watuelimishe kwamba Dr. Slaa hakushinda U-Rais kama anavyodai kuibiwa U-Rais, watuelimishe kwa kuwataka NEC waonyeshe wazi jinsi kura za U-Rais zilivyohesabiwa na zilivyopatikana, wapi na lini ni mambo madogo sana haya kwa taifa na vyama vinavyojali Demokrasia, hasa the future ya hili taifa na uchaguzi,

- Otherwise, kuwatishia wabunge wa Chadema kwamba watafukuzwa au kuwakejeli, na maneno mengi sana tunayoyasikia ya kulaumu wabunge na kususa ni dalili zinazo onyesha kwamba wananchi wengi wa Tanzania hatuelewi maana ya Demokrasia tunayodai kuifuata.

Thaanks.

William.
 
kiongozi Malafyle,
Sijagusia kabisa swala la sheria. Wala sijatoa maoni yangu juu ya kilichotokea Dodoma. Nilichofanya ni kuomba tafsiri pana toka kwa mwandishi.
Hapa tunajadili thread iliyoandishwa na mwenzetu Maggid.

Kumbe hutaki maswali magumu ee!!
Sasa unachobweka bweka hapa ni nini wakati majibu yote unayo?
 
watuelimishe kwamba hawahusiki na NEC na kwamba hicho ni chombo huru[/B], watuelimishe kwamba Dr. Slaa hakushinda U-Rais kama anavyodai kuibiwa U-Rais,

W.J Malecela;Mkuu Nimekupata;

Kimsingi madai ya CHADEMA ni ya wapinzani wote toka vyama vingi vilipoanza July 1992;mwaka 1995-2005 CUF walikuwa na madai kama haya haya ya Tume huru ya Uchaguzi lkn kuingizwa serikalini na kupewa vyeo kumewanyamazisha!

Mwaka 1995-2000 NCCR-Mageuzi ya Lyatonga Mrema ilikuwa na mapambano kama haya haya ya Tume huru ya Uchaguzi lkn akaingia"mdudu mtu"na kukigawa chama hicho kati ya pande ya Mrema na Mabere Marando na baadae chama hicho kukosa nguvu ya kusimamia madai yake!

Mwaka 2010 safari hii CHADEMA wamechukua hatamu ya kuongoza jukumu hilo la marekebisho ya Tume ya Uchaguzi na tumeona juzi wakisema kuwa HAWAMTAMBUI Rais JK kwa sababu alishinda kwa matakwa ya NEC na hata wakatoja nje ya Bunge alipoanza kuhutubia lkn tukumbuke kuwa kauli ya KUTOMTAMBUA Rais kwenye siasa za TZ sio mpya kwani CUF ndiyo ilikuwa silaha yao kwenye chaguzi za 1995-2005!

Malecela William;
CCM HAIWEZI kwenda kwa Wananchi kuwafafanulia kuwa haihusiki na lolote na mamlaka ya tume na kusikilizwa badala ya kupuuzwa kwa sababu hizi chini;

Kwanza;CCM haiwezei kueleweka kwa wananchi kama itarudi kwao a kujibu tuhuma nzito hizi za CHADEMA kwani kwa mazingira ya sasa ya Tume ya Uchaguzi wapiga kura wanaelewa kuwa viongozi wote wa NEC huteuliwa na wanawajibika kwa Rais aliyepo madarakani hata viongozi wa NEC-Wilaya ambao ni WAKURUGENZI wana ripoti moja kwa moja kwa Waziri Mkuu aliyechaguliwa na Rais JK!

Pili;mkanganyiko wa matokeo ya U-Rais mwaka huu yamewafumbua sana macho wananchi na labda itawawia vigumu kwao NEC kujaribu kupindisha mambo;kukiri kwa NEC kuwa "ilikosea kujumlisha kwa matokeo ya U-Rais ya Geita,Vunjo,Segerea na Karatu"ambapo kote huko CHADEMA ilinyimwa kura zake maelfu sio jambo la kurudi kwenda kuwaeleza Wa TZ wa sasa;na kwa NEC kumrudishia kura zake zaidi ya 6000 Lyatonga Mrema zilizokutwa kwenye kapu la mgombea wa CCM kumezidi kuharibu mambo kwa NEC na kuonekana kama ni taasisi ya CCM !

Tume huru ya Uchaguzi itakayo ondoka kuwa chini ya Rais aliyepo madarakani na Wakurugenzi wa Wilaya wasiwe ndiyo wasimamizi wa NEC majimboni ndiyo suluhisho pekee la vuguvugu la kisiasa linaloongozwa na CHADEMA;tukumbuke kuwa madai ya CHADEMA karibu yote yanawaangukia NEC na Rais JK anahusika kwa sababu ni yeye anawachagua wajumbe wa NEC;JK na PM Pinda wakinyang'wanywa nguvu hiyo ya uteuzi kwenye NEC demokrasia itakua nchini TZ!

Lkn CCM toka 1992 hawataki hata kusikia habari ya kuundwa kwa tume huru ya Uchaguzi maana uozo wa TUME hiyo unawanufaisha mno; nasisitiza tena madai ya CHADEMA yana msingi;Tume huru ndipo utakuwa Uchaguzi huru!
 
Malafyale!
Nimeipenda 1000 times
 
that action was well researched, timed, and the best way to bring to public and foreign arena their heartfelt intention to make the crooked straight.
I salute that myself.
 
Kilichotabiriwa tumekiona na tulichoandika kimedhihirika , hii ni baada ya wale wanaojiita wanazi wa chadema wanaoishi ulaya kukaa kimya kuhusu mgawanyiko wa chama chao katika sakata la kususia hotuba ya JK.............sasa nauliza wako wapi mamluki hawa wa CHADEMA?
 
Madai ya KATIBA mpya na TUME HURU ni madai ya upinzani wote.. Lakini wengine wameshachoka ndio maana CUF, NCCR wameamua kuwaachia CHADEMA ambao wamepata bahati ya kuwa wengi bungeni na sasa harakati na matunda ya CHADEMA yataonekana kuinufaisha kambi nzima ya upinzani na wananchi.. Pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu ambao wote wanadai hili.....
Kutoka bungeni ni sahihi katika siasa??? Njia hii ni ya kiungwana au maandamano ndio uungwana????

1. Rejea kule CUBA wabunge walishawahi kutoka wakati Fidel Castro anaongea kwa minajili ya kutokubaliana nae na utawala wake wa kijeshi...
2. Marekani walishwahi kutoka nje kwenye mkutano baada ya kiongozi wa Iran kuanza kuongea kwa minajiri ya kutokubaliana nae
3. Iran waliwahi kutoka nje kwa minajiri ya kukataa Marekani kuingilia nchi za kiislamu
4. Rejea nchi mbalimbali na nyingine juzijuzi tuuu wametoka nje kuonyesha kutokukubaliana, India, Malaysia(mwaka 2008 kuhusu DNA bill ), Pakistan, Japan, South Africa(Zuma insult), Zambia(Electroral bill), Kuwait, Gambia, iraqi(residaa reelect), Sri Lanka na nchi nyingine nyingi...

TAFAKURI:
Kama wewe ni mtu wa kawaida na una uelewa mkubwa wa siasa kutoka nje ni siasa pia kwa kuwa unaonyesha jinsi gani unataka meza ya maelewano iharikishwe... Mimi nakwambia hivi kama CUF wasingekuwa watawala Zanzibar wao ndio wangeongoza msafara.. Kwa kuwa madai ya tume isiyo huru hata wao Pamoja na Lipumba wamekuwa wakilalamikia toka 1995...
Hata hao NCCR nao waliwahi kufungua kesi mahakamani kudai tume huru ya uchaguzi... Kusema kweli sio jambo la kushangaza kabisa...
Kilichotokea pale ni lazima kila mtu na jamii ya kimataifa itamshauri Jk kuingia meza ya makubaliano ili uchaguzi ujao uwe huru na wa haki.. JK asiteue tena refa wa uchaguzi kama tulivyozoea...
CUF, NCCR, TLP, UDP kama wanaongea siasa bila vitendo ni ajabu sana... Wakati mwingine ni lazima uonyeshe uhitaji wa hali ya juu wa kile unachokitaka na si vinginevyo...

Kuna watu wanadai njia iliyotumika si sahihi??? Waniambie wanayoona ni sahihi ni ipi!!! Kama una hoja mbadala toa si kupondea ya mwenzako.. Mimi naona hapa kuna umbwe kubwa la fikra na ukungu mkubwa wa kufikiri... Watu wengi kwa sababu ya ushabiki tunakuwa masikini wa mawazo mbadala.. Kama CHADEMA wamekosea nieleze njia gani ni bora toka 1990 ilipoanza mikakati ya katiba mpya pale Karimjee nadhani ambapo National committee for Constitutional Reform(NCCR) iliundwa..
Tuachie mawazo mbadala na harakati zitendeke.. CHADEMA walituma watu wa IT kuchunguza mtambo wa NEC siku hiyohiyo ukagoma mbele yao.. NEC ikawaihidi watawa feedback ukitengenezwa.. Cha ajabu walipata barua ya tar 28 okt ikafika 8 novemba.. Kwa nini NEC walifanya hivi??Jibu mwenyewe.

Mimi naomba CCM na JK wachukulie haya kwa mustakabali wa nchi yetu.. Kikwete kama atakubali Constitution Reform basi atakumbukwa zaidi kuliko watangulizi wake.. Na mataifa ya nje yatampongea kama mwenzie Mwai Kibaki.. Asiangalie kama CCM itaanguka au laaah... Kwa kuwa ameahidi vitu na anao uwezo wa kutekeleza basi CCM itabaki lakini vinginevyo lazima wataanguka... Wasiogope kwa minajili hiyo lakini watende haki... Siku zote haki humweka mtu huru!!!

Nawasilisha
Eliesikia
 
I have never expected this from you Majjid, this thread is very much exiting man go! and I see changes is coming sooner than Later!
 
W.J Malecela;Mkuu Nimekupata;

1. Kimsingi madai ya CHADEMA ni ya wapinzani wote toka vyama vingi vilipoanza July 1992;mwaka 1995-2005 CUF walikuwa na madai kama haya haya ya Tume huru ya Uchaguzi lkn kuingizwa serikalini na kupewa vyeo kumewanyamazisha!

Mwaka 1995-2000 NCCR-Mageuzi ya Lyatonga Mrema ilikuwa na mapambano kama haya haya ya Tume huru ya Uchaguzi lkn akaingia"mdudu mtu"na kukigawa chama hicho kati ya pande ya Mrema na Mabere Marando na baadae chama hicho kukosa nguvu ya kusimamia madai yake!

2. Mwaka 2010 safari hii CHADEMA wamechukua hatamu ya kuongoza jukumu hilo la marekebisho ya Tume ya Uchaguzi na tumeona juzi wakisema kuwa HAWAMTAMBUI Rais JK kwa sababu alishinda kwa matakwa ya NEC na hata wakatoja nje ya Bunge alipoanza kuhutubia lkn tukumbuke kuwa kauli ya KUTOMTAMBUA Rais kwenye siasa za TZ sio mpya kwani CUF ndiyo ilikuwa silaha yao kwenye chaguzi za 1995-2005!

Malecela William;
CCM HAIWEZI kwenda kwa Wananchi kuwafafanulia kuwa haihusiki na lolote na mamlaka ya tume na kusikilizwa badala ya kupuuzwa kwa sababu hizi chini;

Kwanza;CCM haiwezei kueleweka kwa wananchi kama itarudi kwao a kujibu tuhuma nzito hizi za CHADEMA kwani kwa mazingira ya sasa ya Tume ya Uchaguzi wapiga kura wanaelewa kuwa viongozi wote wa NEC huteuliwa na wanawajibika kwa Rais aliyepo madarakani hata viongozi wa NEC-Wilaya ambao ni WAKURUGENZI wana ripoti moja kwa moja kwa Waziri Mkuu aliyechaguliwa na Rais JK!

Pili;mkanganyiko wa matokeo ya U-Rais mwaka huu yamewafumbua sana macho wananchi na labda itawawia vigumu kwao NEC kujaribu kupindisha mambo;kukiri kwa NEC kuwa "ilikosea kujumlisha kwa matokeo ya U-Rais ya Geita,Vunjo,Segerea na Karatu"ambapo kote huko CHADEMA ilinyimwa kura zake maelfu sio jambo la kurudi kwenda kuwaeleza Wa TZ wa sasa;na kwa NEC kumrudishia kura zake zaidi ya 6000 Lyatonga Mrema zilizokutwa kwenye kapu la mgombea wa CCM kumezidi kuharibu mambo kwa NEC na kuonekana kama ni taasisi ya CCM !

Tume huru ya Uchaguzi itakayo ondoka kuwa chini ya Rais aliyepo madarakani na Wakurugenzi wa Wilaya wasiwe ndiyo wasimamizi wa NEC majimboni ndiyo suluhisho pekee la vuguvugu la kisiasa linaloongozwa na CHADEMA;tukumbuke kuwa madai ya CHADEMA karibu yote yanawaangukia NEC na Rais JK anahusika kwa sababu ni yeye anawachagua wajumbe wa NEC;JK na PM Pinda wakinyang'wanywa nguvu hiyo ya uteuzi kwenye NEC demokrasia itakua nchini TZ!

Lkn CCM toka 1992 hawataki hata kusikia habari ya kuundwa kwa tume huru ya Uchaguzi maana uozo wa TUME hiyo unawanufaisha mno; nasisitiza tena madai ya CHADEMA yana msingi;Tume huru ndipo utakuwa Uchaguzi huru!

- Kama ninakuelea vizuri sana mkuu ni kwamba na wewe kama Majidd, unaoenakan kuamini kwamba katiba ibadilishwe kwa sababu wabunge 46 wamesusia hotuba ya Rais, hilo mkuu ninasema hivi ni hatari sana kwa future ya hili taifa mtoto anapozaliwa huanza na kutaamba kwanza baadaye ndio hutembea, sasa vipi leo Taifa tukimbilie kutembea kabla ya kutambaa kwanza?

- KItendo cha kususa ni cha kaiwada sana kwenye Demokrasia, sasa tuwape nafasi CCM waonyeshe nini maturity yao katika siasa hasa kwa jinsi watakavyojibu hili, Otherwise naona umejaribu sana ku-predict what CCM can and cannot do, sawa ni mawazo yako tu na ni sawa kuwa nayo na umeeleweka sana , lakini sio reality ya kitakachotokea!

William.
 
Kilichotabiriwa tumekiona na tulichoandika kimedhihirika , hii ni baada ya wale wanaojiita wanazi wa chadema wanaoishi ulaya kukaa kimya kuhusu mgawanyiko wa chama chao katika sakata la kususia hotuba ya JK.............sasa nauliza wako wapi mamluki hawa wa CHADEMA?
Chadema haina Mamluki nje as unavyosema..............Hukuona Bungeni?????/
 
Kilichotabiriwa tumekiona na tulichoandika kimedhihirika , hii ni baada ya wale wanaojiita wanazi wa chadema wanaoishi ulaya kukaa kimya kuhusu mgawanyiko wa chama chao katika sakata la kususia hotuba ya JK.............sasa nauliza wako wapi mamluki hawa wa CHADEMA?

Kingetokea ccm ...kingekuwa na sifa ya kuitwa mgawanyiko...

... Chadema hakuna mgawanyiko!!
 
Back
Top Bottom