mkuu leo umeongea ukweli mtupu NIMEIPENDA HIII!Ndugu zangu,
Nilipita Dodoma siku mbili kabla ya JK kuhutubia Bunge. Nilizisikia, fununu za uwezekano wa kutokea kwa tukio lile.
Juzi limetokea, Wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, mbele ya Rais wa nchi, mbele ya wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa, Mabalozi na wengineo. Si habari mpya sana, ilitarajiwa, kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa. Tutayaona mengi mengine.
Baada ya tukio lile nilitarajia Rais angesonga mbele na hotuba yake bila kugusia jambo lile. Hilo la mwisho lingewasumbua sana CHADEMA. Hapana, Rais akagusia tendo lile. Katika nchi, Rais ni mmoja, lakini, kazi ya Urais ni ya wengi. Najiuliza, je, wasaidizi wake hawajua kabla kwamba lililotokea lingeweza kutokea ? Kama walilijua, basi, wangemsaidia Mkuu wa Nchi na kama hawakulijua, nalo ni tatizo.
Nani mshindi?
Katika siasa, lililotokea Dodoma ni sehemu ya mapambano ya kisiasa katika mfumo wa vyama vingi. Chama tawala hakina sababu ya kuogopa. Kianze sasa kuyazoea mazingira haya mapya. Tunachokiona ni mchezo wa kisiasa ambao, kama mechi ya mpira, unahitaji team work na wachezaji mahiri katika kufanikisha ushindi. Maana, tukio lile, kwa wakati huu, limeliongezea ponti kadhaa za kisiasa CHADEMA.
Watanzania wamelifuatilia, Jumuiya ya Kimataifa imelifuatilia. Ajenda ya haja ya uwepo wa Katiba Mpya imeharakishwa kufikishwa kwa umma katika kasi ambayo haikufikiriwa. Watu wanajadili. Ni ajenda ya umma kwa sasa, CCM wakibaki nyuma, CHADEMA wataonekana kwa umma ndio wenye dhamira ya kweli ya kuwasaidia.
Naam. Katika dakika hizi za mchezo huu wa kisiasa, CCM imerudishwa nyuma kwenye lango lake, wanajihami. Na kuna wanaojiuliza nani mshindi? Mchezo bado unaendelea, tusubiri tuone!
Maggid
Arusha,
Novemba 20, 2010
mjengwa
ila noma alishangaa hadi mate yakataka kumdondoka baba wa watu, ila sithani kama atasahau uchaguzi na hii ungwe yakae ya mwisho maishani mwake!
Maggid yuko hivyo siku zote ila huwa mnataka asikosoe mliko nyie!! ndivyo alivyo acheni kujishaua humu!
Nani mshindi?
Katika siasa, lililotokea Dodoma ni sehemu ya mapambano ya kisiasa katika mfumo wa vyama vingi. Chama tawala hakina sababu ya kuogopa. Kianze sasa kuyazoea mazingira haya mapya. Tunachokiona ni mchezo wa kisiasa ambao, kama mechi ya mpira, unahitaji team work na wachezaji mahiri katika kufanikisha ushindi. Maana, tukio lile, kwa wakati huu, limeliongezea ponti kadhaa za kisiasa CHADEMA.
Watanzania wamelifuatilia, Jumuiya ya Kimataifa imelifuatilia. Ajenda ya haja ya uwepo wa Katiba Mpya imeharakishwa kufikishwa kwa umma katika kasi ambayo haikufikiriwa. Watu wanajadili. Ni ajenda ya umma kwa sasa, CCM wakibaki nyuma, CHADEMA wataonekana kwa umma ndio wenye dhamira ya kweli ya kuwasaidia.
Naam. Katika dakika hizi za mchezo huu wa kisiasa, CCM imerudishwa nyuma kwenye lango lake, wanajihami. Na kuna wanaojiuliza nani mshindi? Mchezo bado unaendelea, tusubiri tuone!
Maggid
Arusha,
Novemba 20, 2010
http://mjengwa.blogspot.com
Akisema mnachotaka anasifiwa kwamba anajua uandishi, yupo neutral; akiikosoa CHADEMA mnamwita msaliti, mnafiki, wakala wa mafisadi, nk. Hebu muwe na uwezo wa kutazama pande za shilingi.