Kwa nini JF haina matangazo ya kutosha,licha ya umaarufu wake?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Nimekuwa nikijiuliza kwa nini hapa JF sioni matangazo ya kutosha licha ya umaarufu wake nchini na duniani.Nina amini kwa sasa hapa nchini ukimwuliza mtu mwenye kufuatilia vyombo vya habari nchini hasa mitandao ya kijamii,atakuambia Jf ndio anaujua.

Lakini matangazo ya kibiashara yamekuwa adimu sana hapa jamvini.Kuna blog moja ambayo sidhani kama ina umaarufu sana kuzidi huu lakini imejaa matangazo mengi ya kampuni kubwa kubwa.Labda kama jina la mmiliki ndio ina fanya ipate matangazo zaidi.Hapa JF kuna nini?Hakuna mtu wa marketing anayeweza kutafuta matangazo nje ili kutunisha mfuko wa JF?

Nina amini mtu akitangaza na JF atapata faida zaidi.
Mods tupeni taarifa kama marketer yupo au la.
 
JF hatuendekezi njaa kama hako ka blog. Humu ni Home of Great Thinkers, sisi wanaJF tunalipa ada humun ndani. Au nyie ni wageni humu hamjawai ona thread ya Changia JF?
 
Hata mimi nilishawahi kujiuliza hilo swali. Ninavyojua huu mtandao unaendeshwa kwa gharama kubwa sana. Kama yakipatikana matangazo ya kutosha natumai zitapatikana pesa za kutosha kwa ajili ya mitambo, matengenezo, uboreshaji na kuwalipa watu wanaotumia muda mwingi kuratibu shughuli zote ndani ya hii forum. Matangazo yatakuwa ni chanzo cha uhakika kuliko kutegemea michango isiyokuwa na uhakika. Kwani wengi wetu humu hatujawahi hata siku moja kutoa michango kwa kuendeleza huu mtandao. Nashauri kwa yeyote mwenye kuweza kufanikisha upatikanaji wa yale matangazo ya muda mrefu na yanayolipa vizuri tafadhali afanye hivyo. Huo utakuwa ni mchango wake katika hili jamvi. Asanteni.
 
Wadau,

1. Kwanza makampuni mengi ni waoga wa JF kwa sababu kubwa wanaosema ni kwamba JF ipo kisiasa sana (Controvesal) hawataki kuhatarisha biashara zao. (Its not business friendly)

2. Na wanaokuja kutangaza wana underevaluate value ya JF. Wanataka walipe pesa kidogo sana kwa mwezi.

3. Makampuni yetu hayathamini matangazo kwenye mitandao. Wanaona kama internet ni ya watoto hivi. Makampuni yao wenyewe hayana hata website.

4. Njia nzuri ya JF kupata kipatu ni kwa wanachama wake kulipia subscription fee ndogo kwa mwaka. Matangazo sithani kama ni njia ya uhakika ya kupata kipato.
 
Mkuu hiyo blogu kwanini usiseme kwamba ni michuzi blog? Hata mie inaniboa matangazo ya michuzi yani unascroll kama mara kumi hv ndio unaanza kuona habari,jf is where we dare talk open,usiogope mwana mpe makavu michuzi live.
 
Wadau,

1. Kwanza makampuni mengi ni waoga wa JF kwa sababu kubwa wanaosema ni kwamba JF ipo kisiasa sana (Controvesal) hawataki kuhatarisha biashara zao. (Its not business friendly)

2. Na wanaokuja kutangaza wana underevaluate value ya JF. Wanataka walipe pesa kidogo sana kwa mwezi.

3. Makampuni yetu hayathamini matangazo kwenye mitandao. Wanaona kama internet ni ya watoto hivi. Makampuni yao wenyewe hayana hata website.

4. Njia nzuri ya JF kupata kipato ni kwa wanachama wake kulipia subscription fee ndogo kwa mwaka. Matangazo sithani kama ni njia ya uhakika ya kupata kipato.

•Makampuni ya bongo IT kwishney hata hzo web zao tangia waziupdtae 2010 mpaka leo hawajaupdate!!

•pili hao wana-underate JF kifedha waangalie online How much website worth? Itawapa statistics za traffics inayopita kwenye server then wanyooshe mchele uwe mrefu.
 
Back
Top Bottom