Kwa nini inakuwa ni vigumu kwa msichana kuamini wewe ni rafiki yake tu wakawaida!

wangonyo

Member
Oct 27, 2011
43
3
Hi, wana jamii,

Ndo kwaaaaaanza natokea kwa mara ya kwanza na mada yangu hii, ivi ebu vuta hisia siku ambayo unahisi kukutana na msichana au mvulana katika mazingira flani ya sherehe au mahali pengine na uhusiano wenu kuwa mkubwa kiasi cha kupeana promisi za kukutana mahali baada ya shughuli za kila siku na kubadilishana mawazo.

Ni vipi basi tabia tofauti huanza kutokea pale msichana anapogundua hauhisi mapenzi nae ila unampenda kuwa na urafiki nae na badala yake anakuchukia kiasi kwamba hata salamu inakuwa shida kwa muda mfupi?
 
Labda tuseme kwamba alikuwa anakutaka na we humtaki, ndo unachomaanisha au??? Otherwise, wellcome to the jamvi!
 
kama yamekutokea pole coz labda unabahati mbaya ya kukutana na mademu ambao bado wana akili za kitoto, unataka kuwa na rafiki wa kike go for big girls.
 
sawa bwana lakini japo inaweza kuwa imenitokea lakini haya yanatokea sana na haijalishi umri, je unahisi big girls wao wanakuwa hawana tatizohili?
 
Run, Run, Run away. Kabla haijafikia hatua ambayo huwezi terminate mahusiano, yalinipata nikapatikana,. Tena huyu nadhani uhahitaji kuwa careful maana hata kama na salam inakuwa ugomvi basi si mtu mzuri sana. rejea mada "Kupendwa na Usiyempenda"
 
good! lakini kuna vitu ambavyo nafaidika nikiwa nae karibu, kwani ni mzuri kiasi kwamba nikitoka nae out inapendeza pia ananipa ushauri na mi pia na katika ndoto za kupunguza baadhi ya matatizo yake anaitegemea sana kimawazo na ushauri, nampenda kwa sababu amenipa nafasi kubwa sana hiyo, vp nifanye nini!
 
Nakupa pole coz nahis huwa unakutana na mabint ambao hawajui au hawana uwezo wa kumsoma mtu na kumjua anahitaji nn kwao,kwan kuna wanaume wengine wako kiromantic wakati wote hata kwa marafiki zao yani ile ongea yao,anavyokujali,ukaribu unaokuwepo yani km huna uwezo wa kumsoma utashaangaa,kumbe mwenzio anahitaji kampani wala hana hisia zozote za mapenzi juu yako na vile ndivyo alivyo,haya huwatokea wengi na kuishia kumchukiana na mtu!
 
Hi, wana jamii,

Ndo kwaaaaaanza natokea kwa mara ya kwanza na mada yangu hii, ivi ebu vuta hisia siku ambayo unahisi kukutana na msichana au mvulana katika mazingira flani ya sherehe au mahali pengine na uhusiano wenu kuwa mkubwa kiasi cha kupeana promisi za kukutana mahali baada ya shughuli za kila siku na kubadilishana mawazo.

Ni vipi basi tabia tofauti huanza kutokea pale msichana anapogundua hauhisi mapenzi nae ila unampenda kuwa na urafiki nae na badala yake anakuchukia kiasi kwamba hata salamu inakuwa shida kwa muda mfupi?

Kwa nini unamind yeye kukumind? Nadhani mnapendana.
 
Sio wanawake wote au wanaume wote wanamtazamo huo, mimi binafsi marafiki zangu wengi no wanaumme ndio nnabadilishana nao mawazo kwa miaka mingi na wengine mpaka tumekua kama ndugu, wake zao na mie tunaelewana sana na hakuna anenivunjia heshima. hao wengine wenye tabia hizo ni wale wa nanihiiii....
 
Mimi sina uzoefu na hilo tatizo lako labda kama wananichukia bila mimi kujua.
 
Basi hao wakwako wanabahati sana, may be siku ipo na mimi nitabahatika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mada ni kwamba mi binafsi nahitaji friends yake, na sio mapenzi, vip hapo!
 
hebu sema! sema wanajamii wakusikie, sema usiogope!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
huyo ana matatizo............ ndo wale wasioamini kuna urafiki wa kawaida wa jinsia tofauti. mimi hii inanishangazaga sana kiukweli. na huyo akiolewa hatakuwa na imani na mumewe kuwa na urafiki na mdada yeyote
 
Back
Top Bottom