Kwa nini IGP hasemi lolote juu ya kipigo cha OCD Nzega

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,165
Tukio hili nalilinganisha na jinsi mkuu wa Wilaya alivyo wachapa viboko waalimu huko Bukoba. Tofauti ni kwamba waalimu walichapwa kwa usimamizi wa askari. Huyu OCD ni kwa upuuzi wake tu maana kila mtu pale kituoni alikuwa chini ya amri yake. Alishindwa kutumia amri yake.

Najua ni matokeo ya kudhani wateule wote wako chini ya chama na siyo serikali. Lakini lazima IGP alinde heshima ya Jeshi kama Chama kilivyolinda heshima ya waalimu.

IGP yuko wapi au ndo ushemeji wa kipuuzi na kutojua thamani ya jeshi.
 
IGP ni mteule mwaminifu wa rais aliyeko madarakani na si kwa ajili ya katiba
wanajisahau sana hawa miamba wa majeshi yetu
 
Huwajui polisi! Mi nilishuhudia RPC mmoja akizungumza na mwenyekiti mmoja wa chama cha upinzani na kila mara alikuwa akimjibu huyo mwenyekiti na kutumia neno 'afande'. Nikashangaa sana, baadae nikamwomba askari mwingine ofisa mdogo anifafanulie kwa nini bosi wake alikuwa anamwita mwanasiasa yule 'afande'. Nikajibiwa kuwa hata wao polisi huwa hawajui baadhi ya wanasiasa wako upande gani, kwa hiyo kujihakikishia uhakika wa ulaji wake, anatoa heshima za jumla kuwa naye ni 'afande'.

Kwa kifupi huyo OCD alimwogopa huyo mgombea. Na si huyo tu anayeogopwa. Kuna wafanyabiashara wanaogopwa sana, wengine majambazi wanajulikana lakini polisi wanawaogopa vibaya!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom