Kwa nini hutaki niende?

KIPAPATIO

Member
Feb 29, 2012
13
3
Habari wana JF.

Nina mdogo wangu ambae alikuwa anaishi na mpenzi wake kwa takriban 5 years, na mtoto walizaa pia. Wakati ulifika ambapo walitaka wahalalishe ndoa yao, lakini ghafla mwanaume akasitisha zoezi hilo akidai kuwa huyo mwanamke hakuwa na tabia nzuri, ingawa yeye (mwanamke) alidai kuwa alipata mwanamke mwingine. Walitengana na mwanaume alisema kuwa mkewe akajirekebishe tabia before they get married. Ajabu jamaa anaishi na mwanamke mwingine, tena a close friend wa mdogo wangu.

Huu ni mwaka wa 3, mdogo wangu kampata mchumba ambae anataka wafunge ndoa. Tatizo mwanaume alosema ana tabia mbaya hataki kumruhusu aolewe!Alishalipa mahari, sasa anaombwa arudishiwe mahari yake, jamaa hataki. Akiombwa hata tu walizungumzie hili suala anakwepa. Mshenga na wazee wamemsihi sana akubali kukaa chini na kutoa msimamo wake lakini jamaa kagoma.Mchumba wa sasa anampenda sana huyo dada ila anaogopa jamaa anaweza kuwafanyia kitu kibaya ukizingatia walishazaa mtoto na alishatoa mahari. My sister yuko ktk wakati mgumu sana, je inawezekana kumchukulia hatua za kisheria ili bwana huyu aridhie waachane for good tena peacefully?

Kuna habari toka kwa friends wake kuwa bado anampenda mdogo wangu na anadai hatoruhusu aolewe na mtu mwingine. Hebu nisaidieni ushauri hapa huyu binti afanyeje?

Asanteni.
 
waachane mara ngapi?
hana ndoa nae. anaruhusiwa kuoana na yeyote
hivi ukiachana na mchumba wako/tena amekuacha ukitaka kufunga ndoa na mwingine lazima wa awali aidhinishe?
 
waachane mara ngapi?
hana ndoa nae. anaruhusiwa kuoana na yeyote
hivi ukiachana na mchumba wako/tena amekuacha ukitaka kufunga ndoa na mwingine lazima wa awali aidhinishe?

Issue ya mahari inakuwaje hapo Smile ukiachilia mbali mambo mengine? What if siku ya harusi aje na kusema this is my wife, tulizaa na mtoto na mahari nilishamtolea?
 
Sasa ushauri wa nini na hali halisi inaonyesha kuwa huyo kijana ni muhuni? Au anataka magonjwa!?
 
hapo chacha...., kumbe jamaa ni sitaki nataka eeh, go ahead dada, funga ndoa na huyo wa sasa hatoweza kukuharibia. maana ndoa si mahari, kama kanisani kwetu (RC) cheti cha ndoa ndo kinaweza kusitisha harusi, wala si mahari au eti nilizaa naye. hakunaga hzo...
 
mwambie bana hakunaga kabisa .hizo zingekuwepo kuna ndoa ingefungwa kweli?
 
Hakuna hoja ya mahari hapo kwani alitoa shilingi ngapi....? wait kwanza lakini ishu kama hizi huwa ni tata sana wakati mwingine huwa tunapenda kuonekana hatuna makosa..anyway nenda kwa wazazi wa huyo jamaa muwakabidhi hiyo mahari kwao wao watajua namna ya kumpa mtoto wao...tena hakikisheni mnatunza kumbukumbu za kikao
 
ndio kawaida ya baadhi ya wanaume, anakuacha ili aone unadorora lakini ukipata mwingine wa kukuthamini ndipo anajifanya anajua. He wants to eat his cake and still have it.

Kama walivyokushauri hapo juu, ilimradi hakuna cheti, ndoa yaweza kufungwa tu. Na ushauri mwingine; case hii mtafuteni mzee wa kanisa analoabudu huyo jamaa ili amwitishe na kuongea naye/nanyi.
 
waongeekuhusu nini? Huyo mwanaume ana mwanamke ndani hata kama wangekuwa wana ndoaingevunjwa.wanaume wa tanzania ndivo walivo.shame on him
 
Hakuna hoja ya mahari hapo kwani alitoa shilingi ngapi....? wait kwanza lakini ishu kama hizi huwa ni tata sana wakati mwingine huwa tunapenda kuonekana hatuna makosa..anyway nenda kwa wazazi wa huyo jamaa muwakabidhi hiyo mahari kwao wao watajua namna ya kumpa mtoto wao...tena hakikisheni mnatunza kumbukumbu za kikao

Kwa kumbukumbu zangu jamaa alitoa mahari laki4 tu ambazo dogo ye yuko tayari kuzitoa hata leo. Hao wazazi wake wanadai mahari hairudishwi coz kawazalia mtoto. Tuliwauliza mahari was for mtoto au mke? Hawakuwa na jibu zaidi ya kujikanyaga tu. Hofu iko kwa hawa wapenzi wa sasa, jamaa anaonekana staki nataka, na jamaa ni mkorofi fulani hivi!
 
ndio kawaida ya baadhi ya wanaume, anakuacha ili aone unadorora lakini ukipata mwingine wa kukuthamini ndipo anajifanya anajua. He wants to eat his cake and still have it.

Kama walivyokushauri hapo juu, ilimradi hakuna cheti, ndoa yaweza kufungwa tu. Na ushauri mwingine; case hii mtafuteni mzee wa kanisa analoabudu huyo jamaa ili amwitishe na kuongea naye/nanyi.

Bora hata angekuwa na kanisa analoabudu we could do something, kifupi hata mlango wa kanisa haujui!Lol!
 
mrudishieni mahaari yake kwa M-PESA kama hataki kuonana na nyie .............
MP
 
Back
Top Bottom