Kwa nini hii ni zaidi kwa wanawake ?!

DAWA YA SIKIO

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
979
180
Hili eneo ninaloishi liko mbele sana kwa ku 'export' vijana wasichana kwa wavulana kwenda kufanyakazi za ndani,mara nyingi Dar,Arusha na Moshi.
Kinachonishangaza baada ya muda fulani vijana hao wanaporudi pengine likizo au kuacha kazi,wasichana wengi huonekana kubadili lafudhi kufuata ya kule walikokuwa. Lakini mara chache kwa wavulana kuchenji lafudhi yao ya asili.
HIVYO NAOMBA KUJUZWA HILO LA KUBADILIKA LAFUDHI KWA NINI NI RAHISI KWA KINA DADA ?!
 
Hehehehehe. . . huu ni ugonjwa?

Nwy ngoja nijaribu kuilezea kwa mtazamo wa kisaikolojia ili jibu liendane na jukwaa husika.

Kwenye saikolojia kuna kitu kinaita Conformity. Hicho ni kitendo cha mtu kubadilika kifikra, kimuonekano, kitabia n.k ili aendane na mazingira yanayomkabili au wakati mwingine anafanya hivyo ili tu atimize hitaji lake la kuwa KUNDINI badala ya nje ya kundi. Yani nae afanane na wenzake, asionekane tofauti/mshamba/asiyejua kitu.

Mf. Mzuri ni asilimia kubwa ya vijana wanapoanza kuvuta sigara/kunywa pombe. Wengi hua wanaanza kufanya hayo kwasababu marafiki zao wanafanya hayo. Kukwepa kuitwa mshamba ama kuonekana mjuaji/wa ajabu kwa kutofanya kitu ambacho ni cha kijinga ila kinachokubaliwa na kundi.

Nikirudi kwa wadada na lafudhi vs wakaka na lafudhi.
Kwa wadada kujionyesha nae ni wa mjini ni muhimu kuliko kwa wakaka. Hao mabinti wanapokuja mjini wanaona hitaji la wao kufanana na waliowakuta ili nao wafanane na waliowakuta pia wasiitwe/wasionekane ni washamba, kitu ambacho hakiwasumbua sana vijana wa kiume.
 
Ahsante sana mkuu!
Kwa ufafanuzi wa kitaalamu zaidi! NIMEIPENDA HII!!
But sorry sikumaanisha ugonjwa! Ila nilikuwa nahisi labda ni tatizo la kisaikolojia (kwa maelezo yako najihisi kuwa sahihi). Hivyo sikuona jukwaa lifaalo zaidi ya hili.

Usijali nlikua nazingua tu. .
 
Back
Top Bottom