Kwa nini hatukumuuliza Pinda?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Asalam aleykum, mabibi na mabwana

leo nakuja na hoja binafsi,hoja hii inamhusu Waziri mkuu Mizengo Kayanza Pinda.mh kiranja mkuu wa mawaziri,ulliposema wewe ni mtoto wa mkulima wengi wetu hatukujishughulisha kukuuliza ni mkulima wa aina gani, mkulima wa jembe la mkono au ni settler. Maana hainingii akili maskini mwenzetu kwenda kinyume na wanyonge ambao asilimia zaidi 95 ni walalahoi.

Kama umesahau kuwa sisi ni wenzako ila kutokana na fukuto la mafisadi waliokuzunguka, kwanini usiachie ngazi ukarudisha heshima yako kwa walalahoi wenzako? Ila kama wewe ni mtoto wa mkulima Bepari hapo sawa utakuwa unazingatia maslahi yako. Nasema hivi kutokana na misimamo yako negative, na hoja zako mfu zisizo na mashiko.

Inaonekana si msomaji au mtafiti mzuri wa kutafiti jambo kabla ya kukurupuka na kulitolea kauli.Ikiwa kiongozi mkubwa katika nchi kama wewe na kurupuka basi nchi ina ombwe la viongozi.

Najaribu kukumbusha uongo wako bado haujathibitishwa na Spika kama ulivyotuhumiwa na Mh Lema,leo tena unakurupuka katika bajeti ya Nishati na madini, swali hivi huwa mnakutana na kuorganise mambo kwa maslahi ya taifa au kila mtu nitoke vipi?
 
Back
Top Bottom