Elections 2010 Kwa nini elimu bure inawezekana

Fige,

Umaskini wa akili kitu mbaya sana. Wanaoshangilia wengi ni wale ambao kuanzia kibiriti hadi chumvi ni vya kugongea kwa jirani. Taratibu wanarubuniwa kuwa serikali haina wajibu wowote kwao.

Walianza kukamuliwa kwa kuchangishwa michango ya lazima eti kujenga shule za kata ambazo ni za serikali hadi pale wizi wa richmond ulipostukiwa, jukumu la serikali ni nini? Sasa hivi wanalazimishwa kukesha kwenye patrol na mapolisi eti ulinzi shirikishi.

Hivi serikali kama haiwezi kusimamia majukumu yake muhimu kama ya usalama wa raia wake, tuna haja gani ya kuwa na hiyo serikali?

Ndugu yangu gagnija nashukuru kwa utambuzi wako
 
Kuna jambo linanishanga sana tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu. CCM, hasa kupitia mgombea wake wa urais JK na mwenyekiti wa kampeni wa chama hicho Abdulrahman Kinana wamekuwa kila siku wakiishambulia na kuikosoa vikali sera ya Dr. Slaa ya kutoa elimu ya awali mpaka kidato cha sita bure.

Siku zote wametaka Watanzania tuamini kwamba hizo ni propanga tu za kisiasa za Slaa na ni kitu ambacho hakiwezekani. Hata hivyo, inashanganza kuona kwamba sera ya Prof. Lipumba ya kutoa elimu bure hadi chuo kikuu haipingwi vikali na CCM kama ile ya Dr. Slaa.

Kama CCM wanaamini kwa dhati kabisa kwamba kutoa elimu mpaka kidato cha sita bure haiwezekani basi wangempinga vikali zaidi Prof. Lipumba ambae yeye ameenda mbali zaidi kwa kuahidi kutoa elimu bure mpaka ngazi ya chuo kikuu. Je,unadhani hii ni kwa kwasababu ya upinzani mkali Kikwete anaoupata kutoka kwa Slaa au kwasababu anaamini watanzania hawasikilizi sera za Prof. Lipumba hivyo CCM haioni haja ya kuzijibu?

Tafakari..........
 
Anapata upinzani mkali kutoka kwa Slaa kuliko kwa Lipumba ndio maana hawaishambulii kwa nguvu sera ya elimu bure hadi chuo kikuu ya CUF. Hata hivyo watu wengi hawana taarifa kama CUF wana sera ya elimu bure hadi chuo kikuu, sijui tatizo nini!
 
Chagua Dr. Slaa na Chadema, chagua elimu bure sera ya Chadema. CCM imeleta umaskini kwa kila mtanzania, mkristo, muislamu, mtoto, kijana, mtu mzima na kwa mzee. Tuimwage CCM tupate maendeleo ya kweli, tupate elimu ya bure na thabiti. Mungu ibariki, Tanzania
 
Nimepata uhakika elimu bure inawezekana baada ya kumsikiliza Dr. Slaa. Kama JK anaweza kusambaza picha zake nchi nzima kwenye nyumba za maskini zilizoezekwa kwa nyasi, kwa nini Dr. Slaa asiweze kusambaza elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha sita nchi nzima?

Kwanza pesa kusambaza za kusambaza sura yake kwenye mabango nchi nzima zimepatikania wapi?
 
Hili linawezekana, isipokuwa CCM wanaona aibu kulikubali!!!!!!!!!!!!!!!
 
Anasa zote ziwezekane halafu melimu ishindikane! acaha kabisa.

KAMA ELIMU BURE HAIWEZEKANI BASI JARIBU UFISADI, KODI MGODINI BURE
 
Vyanzo vya elimu bure ni vingi ni kujipanga tu.


Mkuu vitaje vyanzo vyz elimu bure ili watu waelewe kuwa siyo pesa iliyotumika kusambaza mabango ya JK kwenye nyumba za nyasi ingeweza kusambaza elimu bure nchi nzima bali Dr Slaa atatumia vyanzo vingine pia. Mkuu vitaje, tunafanya windo shopingi. Eleza wazi, watu wajue hili linawezekana kuanzia tarehe Dr. Slaa anayoapishwa kuwa rais na kuwekwa sawasawa katika muhula mpya wa masomo wa kuanzia tarehe 1.1.2011.
 
Halafu mbona anasa zote za CCM hazijawahi kukosekana, ila pesa ya elimu na afya tu ndo iwe haitekelezeki!

basi tu kwa vile ni sisi Tanznia. lakini ingekuwa wenzetu CCM ishakuwa chali longiiiiiii!
wewe mpaka waongeze ukubwa wa serikali (yaani wakuu wa mikoa, wilaya) hatuna hela kweli, ufisadi wote wanaofanya!

Elimu bure inawezekana sana tu, na ndo maana wanmwogopa sana Dr. Slaa maana anasema ukweli
 
Halafu wanatoa mishipa kabisa kueleza kuwa haiwezekani, wakati wanajua wanaongea uwongo, unafiki, uzandiki na uzushi!...Ukiweza kutoa tshit, kofia buku5-10 kwa kila mkoa, itawezekana vp kushindwa kulipia elimu bure?
Hii inataka uwe umekunywa PIWA ndipo upate ujasiri wa kupinga, ndio maana wanakataa midahalo, maana wataumbuliwa hawa!
 
Hili linawezekana, isipokuwa CCM wanaona aibu kulikubali!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu ninauhakika kwa asilimia mia moja kuwa inawezekana na kuwa kumchagua Dr. Slaa kuwa rais ni kuchagua elimu bure, ila tueleze vyanzo vingine vingi vya pesa vya kutoa elimu bure ili watu wapate uhakika kwa asilimia mia moja kuwa kuanzia tarehe ya kuapishwa Dr. Slaa kuwa rais elimu Tanzania ni bure na itasukwa vizuri iwe ya kukata na shoka.
 
Nimepata uhakika elimu bure inawezekana baada ya kumsikiliza Dr. Slaa. Kama JK anaweza kusambaza picha zake nchi nzima kwenye nyumba za maskini zilizoezekwa kwa nyasi, kwa nini Dr. Slaa asiweze kusambaza elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha sita nchi nzima?

Kwanza pesa kusambaza za kusambaza sura yake kwenye mabango nchi nzima zimepatikania wapi?
Zimeprintiwa Canada na kulipiwa na Serikali ya Tanzania...!
 
Kuipa thithiemu kura yako ni sawa na kujilaani mwenyewe ili ubaki na umasikini. Wao wanakimbia nyie mwatembea mkiimba ccm, ccm,ccm. Fungua macho mpe slaa kura yako!
 
Amesema watanzania waliambiwa wabane mikanda baada ya vita vya Uganda. Serikali yake sasa ndiyo itakayobana mikanda kwa kupunguza matumizi makubwa ya uendeshaji wa serikali na pesa hizo ziende kwenye maendeleo ya elimu.

Amesema serikali ambayo inaona elimu ni gharama, haitaweza kamwe kujinasua kwenye umasikini, ataweka misingi imara ya elimu kuanzia elimu ya wali hadi darasa la kumi na nne ambayo itakuwa ni ya lazima kwa kila Mtanzania, atakuwa mkali kwa yeyote atakayezembea.


Wanafunzi watakaofaulu darasa la kumi na nne watasomeshwa vyuo vikuu kwa gharama za serikali.


1. Amewahakikishia Watanzania kuwa lile tangazo la kufunga mikanda la mwaka 1980 litakoma kuanzia siku atakapoingia Ikulu,

2. atahakikisha kila mwananchi anaishi kwenye nyumba ya bati,
3. kila mwanachi anapata huduma ya matibabu bure
4. Elimu ya bure kwa lazima
5. Wazee wa Afrika ya Mashariki wanalipwa mafao yao yote.
6. Pesa za DECI Bilioni 15 zinazoshikiliwa na serikali zinarudishwa kwa wenyewe
7. Viwanja vya michezo vilivyoporwa na mafisadi vinarudishwa
8. Atahakikisha Tanzania itarudi kwenye chati ya michezo duniani, kwa kuweka mikakati ya michezo kuanzia ngazi ya chini hadi taifa kwa kutumia Wataalamu wa Kitanzania.
9. Wote waliohusika na ufisadi, sheria za nchi zitachukuwa mkondo wake.
10. Watanzania wote watahusika kuandaa katiba mpya ya Tanzania.
 
Yaani pesa ya serikali inatumika kulipia mabango ya JK, huku si kuvunja sheria ya uchaguzi aliyoisasini kwa mbwembwe?
Kwani umewahi kusikia mtego unajinasa? Lakini ukweli ndio huo, na fedha hizo zimelipwa na Ikulu...!
 
Ninavyowajuwa sisi m hawachelewi ku copy and paste yale Chadema wamesema kuwafanyia wananchi kama wao watarudi madarakani.
We only needs time to confirm this.
 
Back
Top Bottom