Kwa nini Chadema Kitabaki Kuwa Chama Kikuu cha Upinzani?

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
552
Chama cha Democrasia na Maendeleo ni chama pekee ambacho watanzania wa kawaida, Wasomi, Wanafunzi, Watoto wa hadi miaka 10 wanakiamini kutokana na kuibua mambo ya msingi ambayo hakuna chama kingine kimeweza kusimamia tangu mwaka 1992 ulipoanza mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Kwanza kabisa unapozungumzia Afya bure, Elimu bure unamgusa mwananchi wa kawaida awe mfanyakazi au mkulima kwa hiyo huwezi kuwabadilisha watu hawa na watoto wao kuacha kuiunga mkono chadema.

Unapozungumzia Katiba mpya unawagusa wasomi wengi wa TZ ambao wamekuwa wakililia Katiba mpya toka zamani, Ambayo kwa sasa chadema wameishikia bango hadi kuamua kutoka bungeni wakati Rais aliyeingia madarakani kwa mapungufu hayo ya katiba anaanza kulihutubia bunge.

Ndiyo maana kwa sehemu ambayo wameonja uongozi wa chadema huwezi kuwaambia kitu, wala hawawezi kuichagua chama kingine mfano KRT, Moshi mjini na Kigoma Kaskazini etc.

Ni chadema iliyotoa hadharani ufisadi wa EPA,Majengo ya BOT, Richmond, Kiwira na mengine ambayo yameonekana ni ya kweli na baadhi ya watu kufukuzwa na pesa zingine kurudishwa kama kwenye EPA sasa leo hii umwambie mtu asikiunge mkono ataunga mkono chama gani?

Jambo lingine ambalo kitaifanya chadema kieendelee kuwa juu ni swala la CCM na makundi yake (CUF, NCCR, TLP,UPDP etc.) kuwa kitu kimoja toka wakati wa Uchaguzi hadi sasa kukiandama chadema ambayo ndo ina wafuasi wengi hasa vijana ambao ni wanavyuo, na wanafunzi mashuleni, Wasomi etc. Hii inafanya hata kama kuna kiongozi ndani ya Chadema ana hila zake za kukihujumu asifanikiwe kutokana kelele zinazotoka nje chama hasa kwa wanachama wake kuanza kusema ukweli hata kabla ya maamuzi ya chama, mfano ukikuta kiongozi au mbunge wa chadema anatumiwa na CCM kuihujumu chama utaona watu wanamkosoa haraka mno.

Peoples Power.

CDM (Nguvu ya Wananchi) kilivyoanza kimeonyesha ni chama cha watu (ukiachilia mbali wenye wivu wajinyonge ambao wanazusha eti ni cha kidini) hata ubadilishanaji wa uongozi na wagombea wa urais havikuwa vimemilikiwa na mtu mmoja. Chama hiki si rahisi kikarudi nyuma kwani kina mchanganyiko mkubwa sana na mzuri unaowakilisha makundi yote unayoyakuta katika jamii. Ni chama makini kila aliye makini anavutiwa nacho kama si kujiunga. Subiri uone mweleka wa nguvu ambao CCM itakula mwaka 2015. Tufanye kazi kwa nguvu na bidii tusilale kwani tuko vitani, lakini kwa sababu tunasimama katika haki hakika tutashinda.
 
Kilichobaki ni kuwapa watu ukweli mtupu na si kuwadanganya kama ambavyo vyama vingine vikifanya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom