Kwa nini CCM inatetemeka mbele ya Chadema? Soma hapa kupata ushahidi


Mwenyekiti wa NEC ambaye ni mteule wa bosi wa CCM, anajua fika kwamba ni ukiukwaji wa sheria na kanuni kutorekebisha daftari la wapiga kura la Arumeru Mashariki (kama ilivyokuwa Igunga), lakini bado hafanyi chochote, huku akijuwa wazi kwamba kuna maelfu ya vijana waliofikisha miaka 18 tangu marekebisho ya mwisho katika daftari hilo ya mwaka 2010 wamenyimwa fursa ya kupiga kura katika uchaguzi huu.

mweyekiti huyo wa NEC anatambua fika kwamba wengi wa vijana hao ni Chadema, kwa hiyo ili kuiokoa CCM, basi anaona bora wasiandikishwe.

Huyu Mwenyekiti wa NEC wa sasa nilidhani atakuwa tofauti na yule wa zamani ukikumbuka alivyosema katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kuapishwa. Hakika kaambiwa na CCM "usithubutu kuandikisha vijana, hawa vijana wataiangusha CCM."


Yana mwisho ndg yangu hata utawala wa farao uliangushwa na kuwaachia wana Misri kuondoka hivyo tusubiri tu hukumu liko hapahapa hata kama watafanya ujanja leo lakini kesho watashindwa. Mungu hawezi kuwaacha wana wake wateseke hivi uku baadhi ya watu wakiishi kama sodoma na gomora.
 
Ndio maana tunaposema mabadiliko ya katiba tuna sababu kubwa ya kumwondolea rais mamlaka ya kutengeza tume ya uchaguzi lakini pia tunataka mamlaka wapewe wananchi wenyewe.
Huu ni uonevu kwa wapiga kura.

sina imani sana kama katiba itafanya tunavyotaka
 
Back
Top Bottom