Kwa nini CCM hawafukuzi mara moja makada wao 'mizigo' - wanangoja hadi wawaumbue?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Kwanza kabisa mimi siyo mfuasi wa CCM lakini nauliza tu: Kwa nini vigogo au makada wa CCM wanaoonekana wakorofi hawafukuzwi mara moja kutoa chamani -- wanasubiri hadi waumbuliwe kwa wenyewe kuamua kuhama? Kwa nini wakisha kihama chama hicho ndiyo viongozi wa CCM wanakuja na kauli za "alikuwa mzigo tu, alishapewa karipio lakini hasikii, mkorofi etc etc"?

Natoa mfano: Leo hii Mr 6 akiamua kuhama CCM na kuingia CDM (highly improbable, but quite possible) akina Mukama watakuja na kauli kama hizo ilizozitaja. Kwa nini CCM hawataki kuwa-preempt 'wakorofi wao?
 
NDEVU sii mzigo unaishi nchi gani? CCM ni mzoga ulionona unamiliki rasilimali nyingi za watanzania hivyo kila unayemwona CCM ni mla mizoga kama fisi, makunguru, mwewe, tai, mbeha,na wengine idadi ni ndefu. Wote wapo CCM kwa maslahi yao tuu siyo ya chama chenyewe wala taifa na hao unaowaona wanaondoka ni kwamba urefu wa kamba yao kwenye kula mzoga imefika mwisho. unasahau kuwa mr 6 na wenzake walianzisha chama ccj na walipoona matarajio yao hayakufanikiwa wakaendelea kubaki? wewe subiri tuu mwaka huu 2012 na 2013 utashuhudia maajabu ya musa kwa sababu mzoga wenyewe utakuwa umebaki mifupa mitupu utaona jinsi watakavyokimbilia kwenye vyama vyenye mvuto mkubwa na dalili za kuchukua dola 2015. tafakari halafu chukua hatua
 
Tatizo kubwa ni kwamba viongozi wote wakuu wa ccm wana ugonjwa wa "UPUNGUFU wa MAAMUZI MAGUMU MWILINI". Hivyo usitegemee wanaweza kuchukua hatua yoyote kwa wale wanaowatuhumu kuwa ni mzigo kwa chama chao.
 
Hali ya ccm kwa sasa ni kama ya mgonjwa fulani aliyekuwa ICU na katika hali ya kuchanganyikiwa akawaambia jamaa zake sasa naona hali yangu inaimarika naomba mkaninunulie buti na kombati nataka kwenda jeshini.
 
Ni kiongozi gani msafi wa kumfukuza mwenzie ndani ya CCM?
Kila mmoja anaogopa 'mwaga mboga, nimwage ugali'
 
NDEVU sii mzigo unaishi nchi gani? CCM ni mzoga ulionona unamiliki rasilimali nyingi za watanzania hivyo kila unayemwona CCM ni mla mizoga kama fisi, makunguru, mwewe, tai, mbeha,na wengine idadi ni ndefu. Wote wapo CCM kwa maslahi yao tuu siyo ya chama chenyewe wala taifa na hao unaowaona wanaondoka ni kwamba urefu wa kamba yao kwenye kula mzoga imefika mwisho. unasahau kuwa mr 6 na wenzake walianzisha chama ccj na walipoona matarajio yao hayakufanikiwa wakaendelea kubaki? wewe subiri tuu mwaka huu 2012 na 2013 utashuhudia maajabu ya musa kwa sababu mzoga wenyewe utakuwa umebaki mifupa mitupu utaona jinsi watakavyokimbilia kwenye vyama vyenye mvuto mkubwa na dalili za kuchukua dola 2015. tafakari halafu chukua hatua

Tumeshaambiwa ccm ni gari lenye pancha kibao,abiria asiye na nauli ya kupanda gari lingine atasubiri pancha izibwe na kisha kupanda hilo gari hata haangalii muda.LAKINI ABIRIA MWEREVU ATAPANDA GARI LENYE PANCHA AKIWA NA AKIBA YA NAULI ILI PANCHA IKITOKEA ATAPANDA GARI LINGINE NA KUENDELEA NA SAFARI KWA KUZINGATIA MUDA.TIME IS MONEY.
 
Kila siku mi huwa nasema kwamba hichi chama cha Majambazi CCM kinahitaji sala ya toba ya kweli na maombi kwani ni waongo kupita maelezo kwani jana walisema milya alikuwa mzigo kwa chama. Du..............
 
Nani ataanza kumnyooshea kidole mwenzie wakati wote ni waovu?? sioni alie salama kati yao na ndo maana wanaogopana kiasi hicho!
 
Back
Top Bottom