Kwa nin Wa Tz hawataki ushauri wa MKE??

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Ninauliza hivyo cause, wakati nilipokuwa katika mchakato wa umiliki wa silaha, niliitwa katika kamati ambayo ilijumuisha mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wapatao saba, Swali la kwanza nililoulizwa na kamati lilikuwa..Wazo la umiliki wa silaha umelipata wapi?? umepewa ushauri na mkeo au ni wazo lako mwenyewe? Nikajibu ni wazo langu mwenyewe, yakafatia maswali mengine.... Kikao kilipoisha mwenyekiti wa mtaa akaniambia kuwa nimejibu vizuri sana, na laiti ningesema nimepewa ushauri na mke na nisingepata kamwe leseni ya silaha.
Tukiacha hayo...pia nimewahi kumsikia mara nyingi sana Baba wa Taifa akikataza waTz
wasiwe ni watu wa kufata ushauri wa wake zao... na kuna kipindi alimkaripia
sana rais wa
awamu ya pili (Ali Hassan Mwinyi) kuwa anaendesha nchi kwa kufata ushauri wa Mke!!

Sasa jamani tusipofata ushauri wa mke...tufate ushauri wa nani?? Na inasemekana pia
Katika kila mafanikio ya Mwanamme, basi kuna mwanamke nyuma yake
 
:smile-big:Huwezi kuendesha nchi kwa ushauri wa mke wakati katiba ipo utakuwa umemgeuza mkeo kuwa katiba ya nchi! Wazo la kumiliki silaha ni very sensitive na muhusika anawajibika kwa hilo ndiyo maana alikuuliza wazo umetoa wapi! Wtz hawakatai ushauri wa mke hasa katika biashara, na maendeleo kwa ujumla
 
ii
Sasa Baba wa Taifa alijuaje kama Mwinyi anafata ushauri wa mke?
 
Usemi wako kuwa 'Watanzania hawapendi ushauri wa mke' si sahihi! Kwani waTanzania wote ni wanaume? Hao wake wao si Watanzania?
Tafadhali wakati mwingine uandike ' Wanaume wa Tanzania'
 
walikuuliza wazo umelitoa wapi ili wajue kuwa unataka silaha kwa matakwa yako binafsi au kwa shinikizo la mtu ilikuwa ni mtego tu na hilo la baba wa taifa lina maana kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya katiba na si vinginevyo

ushauri wa mke ni muhimu sana ktk maisha ya kila siku ya kifamilia na katu hauwezi kupuuzwa ila kama ukiwa sehemu nje ya familia kama kazini unafuata mwongozo wa kazi yako
 
" USHAURI WA MKE" ni msemo tu kuonyesha mtu anayefanya mambo rasmi bila kufuata utaratibu rasmi.

Katika maisha ya kila siku, mwanaume yeyote mwenye kupenda maendeleo haachi kumshirikisha na kutaka ushauri kutoka kwa mkewe. Ukipenda kwenda mbali zaidi, wanaume viongozi, wenye wake makini hupata ushauri mara kwa mara kutoka kwa wake zao. Hii ni mpaka kwenye ngazi za uongozi wa kitaifa.Wake huandaa hotuba na mada mbalimbali zenye kugusa sera na miongozo kuelekeza hatma ya nchi, taasisi nakadhalika.Msijidanganye kuwa ati wanawake wahashauri hata Tanzania.Ila ukikuta mwanamke bomu ndio utaishia kupata ushauri bomu pia.Kumbuka tumepewa karama ya ziada sisi wanawake tuna uwezo kushawishi na kupata tutakacho bila nguvu.
 
Ina maana Tanzania hakuna Wanawake wanaomiliki Silaha??
Hata miye nimeshangaa..kam awanawake wanamiliki silaha, je wao wazo la awali la kumiliki silaha lilizingatiwa vipi ukitilia maana hawatakiwi kutia neno kwenye hili.
 
" USHAURI WA MKE" ni msemo tu kuonyesha mtu anayefanya mambo rasmi bila kufuata utaratibu rasmi.

Katika maisha ya kila siku, mwanaume yeyote mwenye kupenda maendeleo haachi kumshirikisha na kutaka ushauri kutoka kwa mkewe. Ukipenda kwenda mbali zaidi, wanaume viongozi, wenye wake makini hupata ushauri mara kwa mara kutoka kwa wake zao. Hii ni mpaka kwenye ngazi za uongozi wa kitaifa.Wake huandaa hotuba na mada mbalimbali zenye kugusa sera na miongozo kuelekeza hatma ya nchi, taasisi nakadhalika.Msijidanganye kuwa ati wanawake wahashauri hata Tanzania.Ila ukikuta mwanamke bomu ndio utaishia kupata ushauri bomu pia.Kumbuka tumepewa karama ya ziada sisi wanawake tuna uwezo kushawishi na kupata tutakacho bila nguvu.

Hapo kwenye red ni kweli kabisa!na ndio maana mwanamke akiaamua kumpata mwanaume fulani kimapenzi anampata kiulaini tu!kila aina ya mitego!
 
Kwani usipofuata katiba inamaanisha kuwa utakuwa unashauriwa na mkeo? Kwa nini isiwe rafiki, mama, mtoto, n.k.?

Angekuwepo aliyesema tungemuuliza kwa nini alisema hivyo lakini kumbuka hata mke ni rafiki:focus:
 
Hapo kwenye red ni kweli kabisa!na ndio maana mwanamke akiaamua kumpata mwanaume fulani kimapenzi anampata kiulaini tu!kila aina ya mitego!
:whistle:
:dance:
:dance:

Hahahaaa dar waendelee hivyohivyo mie huwa nategeka kirahisi kweli
 
Back
Top Bottom