Kwa nia njema..,sema hapana...!

pinguli

Senior Member
Oct 12, 2010
122
14
405223_346521995385614_189339031103912_892441_739061690_n.jpg

wametuhadaa wakatumia nguvu zetu katika kuwapamba na kuwabeba..,

wametufanya tupigwe risasi na kuuawa wakaita vifi vya kishujaa..,

wametuibia na kufanya ufisadi wakidai ni akiba ya kizazi chao kijacho..,

wanagawana vyeo kwa hila wakituambia tusubiri muda wetu bado..,

wanatumia midomo yetu kusemea ajenda zao..,

wanatuahidi madaraka na kutupa vifo..,

vijana kwa pamoja tuseme NO COUNTRY FOR OLD MEN...!
 
Hamna kitu unatatua hapo.... Like father like son..

Tafuta suluhu nyingine...
 
Umuhimu wa wazee kwenye uongozi hauwezi kubezwa kwa vyovyote vile. Hata Mungu, kipindi cha Mussa, aliwatumia wazee kumfikishia ujumbe wake kwa wananchi.
 
Mbona simuoni Prof wa ukweli, Professor Ibrahimu Lipumba au yeye ni KIJANA?
 
Inawezekana hawa wazee hawafai ila urais sio tuingie kwenye try n error ...
vijana wameonyesha udhaifu kiasi kikubwa.

wanazunguka na guns ;Masha huyu analewa na kutishia watu silaha akiwa waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha usalama wa raia.Malima skendo bado mbichi.

Wengine hawako royal kwa team;Zitto huyu inabidi kuonyesha kukomaa ingawa kijana kuonyesha anaweza kuflow na team ,yes kuna ku agree to disagree but you must be royal to the team flow by resolution ..ukishindwa hivyo utaweza wapi kwa nchi.

January never been tested mengi anayofanya inaonekana is to make impression
Track record ni muhimu sana jamani...ila kwa kuwa ni vijana wana muda wa kufanyia kazi mapungufu
jamani kuna mambo mengi ikulu ...naunga mkono vijana ila sio hawa tunao wajua ...
na usithubutu kuwapima katika comfort zone...you dare ..brother!!
 
View attachment 49791

wametuhadaa wakatumia nguvu zetu katika kuwapamba na kuwabeba..,

wametufanya tupigwe risasi na kuuawa wakaita vifi vya kishujaa..,

wametuibia na kufanya ufisadi wakidai ni akiba ya kizazi chao kijacho..,

wanagawana vyeo kwa hila wakituambia tusubiri muda wetu bado..,

wanatumia midomo yetu kusemea ajenda zao..,

wanatuahidi madaraka na kutupa vifo..,

vijana kwa pamoja tuseme NO COUNTRY FOR OLD MEN...!

Nyerere, Mwninyi, JK sio wazee vipi Lipumba? au una chuki na hao tu? hujanidanganya, binafsi sina ugomvi na uzee au ujana ila dhamira safi na nchi yetu
 
Kuwa rais si kwenda kubeba karai la zege ikulu,SAY Malicela and mrema.hoja yako haina mashiko
 
Kabla ya kutaja watu wa kugombea urais ingefaa zaidi kama tutajikita katika kujua sifa za mtu anayefaa kuwa rais! Otherwise tutakuwa tunapoteza muda bure na possibility ya kumpata rais bomu itakuwa kubwa. Kwanini hatujifunzi kutokana na makosa? Kabla ya mwaka 2005 tulijikita katika kujadili nani anayefaa matoleo yake wote tunayaona. Tubadilike jamani let us go extra miles please!
 
View attachment 49791

wametuhadaa wakatumia nguvu zetu katika kuwapamba na kuwabeba..,

wametufanya tupigwe risasi na kuuawa wakaita vifi vya kishujaa..,

wametuibia na kufanya ufisadi wakidai ni akiba ya kizazi chao kijacho..,

wanagawana vyeo kwa hila wakituambia tusubiri muda wetu bado..,

wanatumia midomo yetu kusemea ajenda zao..,

wanatuahidi madaraka na kutupa vifo..,

vijana kwa pamoja tuseme NO COUNTRY FOR OLD MEN...!

NAPE ni kijana mdogo ila anayoyafanya unayafahamu.
A prudent man always judge people by the content of their character and not their age/colour/sex/race etc...
Hebu rethink critically then ulete hoja za maana bana.
 
View attachment 49791

wametuhadaa wakatumia nguvu zetu katika kuwapamba na kuwabeba..,

wametufanya tupigwe risasi na kuuawa wakaita vifi vya kishujaa..,

wametuibia na kufanya ufisadi wakidai ni akiba ya kizazi chao kijacho..,

wanagawana vyeo kwa hila wakituambia tusubiri muda wetu bado..,

wanatumia midomo yetu kusemea ajenda zao..,

wanatuahidi madaraka na kutupa vifo..,

vijana kwa pamoja tuseme NO COUNTRY FOR OLD MEN...!

Ukisikia bigotry ndiyo hii. Kwa nini usihamasishe vijana kujitokeza kwa wingi kugombea kuliko kutaka kuzuia kundi la umri fulani lisiwe na haki ya kugombea?.

Huoni kwamba unavunja katiba na kupandikiza mbegu ya ubaguzi. Kesho ukija na tamko la kuzuia wanawake, keshokutwa utakuja na watu wa kabila fulani then what next?
 
Sitta Hapana kabisa hata kama angekuwa kijana...

Kwani kati ya sita na lowasa bora nani? Maana lowasa ana kashfa ambazo kwa serikali ambayo ni shupavu na imara angekuwa ashafungwa na kunyongwa siku nyingi sana, jambo kubwa kwake yeye la kumshukuru Mungu ni kutozaliwa CHINA na kuzaliwa nchi kama TZ yenye serikali legelege na inayojua kubebana yenyewe ndani ya chama chao
 
Umuhimu wa wazee kwenye uongozi hauwezi kubezwa kwa vyovyote vile. Hata Mungu, kipindi cha Mussa, aliwatumia wazee kumfikishia ujumbe wake kwa wananchi.

Na siyo wazee wote wanaweza kutoa ushauri wenye kuleta maendeleo
 
Back
Top Bottom