Kwa mzazi utajisikiaje? Je, ni sawa?

Tatizo wabongo swala kusomesha tunachukulia kama kuwekeza.Ipo hivi mzazi kumlea mtoto ni wajibu wake ikiwemo kumsomesha ila mtoto kumlea mzazi ni option na ukichunguza utagundua iwapo mzazi atakataa kumlea mtoto sheria inaweza kumuandama ila mtoto hawezi kuandamwa na sheria iwapo hataprovide malezi.So mtoto kumsaidia mzazi ni swala la kiutu tu kama asaidiavyo ndugu wengine.
 
Big up Annael,yote ulosema is very true kulingana na Biblia(kwa wale wakristo).Kina dada tusibishe,huo ndio ulikuwa mpango wa Mungu,sema ni ukali tu wa maisha,na ukali huu wa maisha ni kutokana na kutokumtii Mungu.Cha muhimu kama kuacha kazi huwezi basi jitahidi kutimaza wajibu wako kama mama,maana mpango w a shetani ni kuwachosha sana sana wana ndoa,especially kina mama ili washindwe kutimiza wajibu wao kwa watoto na waume zao,matokeo yake ndio siku hizi unaona watoto wameharibikiwa na waume wanatoka nje ya ndoa,ukichunguza utakuta mama anafanya kazi na ni bosi flani hivi,muda mwingi yuko job,anarudi usiku,na jmosi yuko job,yani ni hatari,kwa kifupi shetani amewin kampango kake kwa kiasi fulani.Yatupasa kuombea sana familia zetu.EE MUNGU OKOA FAMILIA ZETU,UTUWEZESHE NA SISI KINA MAMA KUWA WATII,MAANA UTII WETU UTAWAFANYA WAUME ZETU WATUPENDE NA WAWAJIBIKE/WATAJIFUNZA VIA SISI!!!AMEEEN!!
 
Muumba wetu anasema asiefanya kazi na asile, sasa wewe kwa kuwa tu umependwa ndo usifanye kazi? huoni unamkosea mungu wako kwa kula nguvu za wengine

kwani kwa kufanya kazi unashindwa nini kumtii mme wako, au mpaka uletewe kila kitu ndo unakuwa utii huo, nadhani hapa na uvivu unaingia, halafu tunasingizia utii
 
My dear kazi za nyumbani nazo ni kazi,Mungu hakumaanisha kazi za ofisini tu au self-employed,kazi za nyumbani pia ni kazi,tena zinachosha kuliko hata ofisini,kutwa na watoto acha hiyooo,huku upike huku kufua,na wengine mpaka leo wafua kwa mikono,hujafanya usafi wa nyumba,nyumbani acha kabisa kunachosha.Pole,biblia inasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".Na kama mmekubaliana na mwenzio kwamba mama ulee watoto,sioni sababu ya kutomtii mwenzio!ok by the way kila mtu na uelewa wake na mtakanyokubaliana,ni ushauri tu.
 
Japo mara nyingi wanaume ndio hushinikiza mwanamke akae nyumbani, lakini kuna baadhi ya kesi wanawake wao wenyewe hutaka kukaa nyumbani hususan baada ya kuzaa watoto

Wanawake wa hivi wanaamini priority yao kubwa ni kuhakikisha watoto wanalelewa kwenye malezi stahiki na hawaamini kuwa kuna yoyote mwengine anaeweza kutoa malezi hayo zaidi yao wao.

Pia kuna wanaume wanaowalipa wake zao posho/mshahara kila mwezi kutokana na wao kukaa nyumbani.

Kwa hiyo sio kila anaekaa nyumbani kosa ni la mwanamme au ndio hana pesa ya kumsaidia mzazi wake
 
Tushaibiwa kila kitu watu weusi,mtu aliyebarikiwa anatakiwa kuacha urithi kwa watoto wa watoto wake,na ndivyo wahindi,waharabu,n.k wanafanya.

mtoto wako tu wa kiume anaoa unafanya kila mbinu ndoa yake unaiharibu kwa chuki zisizo na sababu,je utaweza kweli kuwaachia urithi watoto wa watoto wako?mtu mweusi ana safari ndefu ya kurudisha alivyoibiwa.tumeibiwa mema tumejaziwa mabaya yote:wizi,chuki,zinaa,uchawi,n.k.

Km kuzaa lengo ni kumgeuza mtt pension ni heri uishi peke yako,kuliko kuzaa na kutesa viumbe visivo na hatia.mwishowe wanaomba ufe haraka wawe na amani.
Wazazi wangefata neno linavosema,wala tusingekuwa na shida ya ajira leo hii,eg indians,waarabu.
 
Back
Top Bottom