Kwa mzazi utajisikiaje? Je, ni sawa?

Eversmilin Gal

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
778
269
wapendwa hope wote ni wazima wa afya,nilisoma thread moja inayosema MATARAJIO YA MZAZI ANAPOSOMESHA MTOTO mletaji mada alikua akilalamika mama yake anataka hela nyingi hata kwa vitu visivyo vya muhimu kama kuchangia harusi ua jirani kisa anacheka naye vizuri ambayo stimes ni sawa pia ,swali langu linakuja je vip kwa mzazi utajisikiaje umemsomesha mwanao tena kwa kujinyima halafu leo anatokea mwanaume anamuoa binti yako hataki afanye kazi akae tu nyumbani amfulie na kumpikia na hata hela hela ya kununua sukari huipati je ni sawa Kwa ule msemo Mtu atamuacha wazazi na kuambatana na mume kwamba hahusiki na maisha ya wazazi au wadogo zake nawasilisha karibuni tujadili
 
mie binafsi swala la kuambiwa acha kazi kaa nyumbani halipo.....kuna raha kutumia hela za jasho lako na inasaidia kufanya mambo yako bila kuombaomba.....unakuta mwanaume anakwambia acha kazi lakini unapokuwa na shida labda unataka kutuma hela kwa wazazi wako unabembeleza hadi hasira loooo mie kazi kwanza
 
Anaekubali kuacha kazi ni MJINGA tena sana.Mfano, mme akitangulia mbele ya haki, ndiyo mtu aanze kujipanga??Hata mwanamme anaeshauri mke wake kuacha kazi hafai kabisaaaa!!!
 
halafu mi naona ndio mwanzo wa kutoendelea maana utoapo chochote wanakuombea baraka upate na zaidi
 
Masuala ya watu kwenye uhusiano wao hayawahusu watu wengine. Na mzazi anayemsomesha mtoto wake akitegemea kulipwa fadhira hiyo ni fikra potofu tena haifai. Kumtunza na kumsomesha mtoto ni wajibu wa mzazi lakini mtoto kumtunza mzazi wake ni utu na sio wajibu.

So kukubaliana mume na mke kuwa mke akae nyumbani inamaana yake. Tatizo hii dot com inawachanganya sana. Ndio maana watoto wanaozaliwa siku hizi ni wahuni hata kabla ya kuvunja ungo.

Mama mara zote ni mlezi wa familia na baba mara zote ni mlinzi wa familia.

Umenipata?
 
mmh! mdogo wangu mwanaum wa kusema uache azi sababu kubwa kabisa hapo ni wivu tu wa kimapenzi. mwanaume huyu binafsi ningemwambia hivi basi tufungue biashara mie niwe msimamizi wa hiyo biahsara ili nami nipate kutoka na kuongeza kipato cha familia.

nimeshuhudia mwanaume akimwambia mkewe mimi itakulipa hiyo hela unayolipwa kazini kwako acha kazi, mke akamwambia amfungulie biashara kwanza ndipo aache kaazi manake kwa maisha haya kila mtu inabidi ajitahidi kufanya kazi kasababu ya ujenzi wa familia.

ila pia mwanaume wa aina hii hupenda sana kuona kila kitu anahudumiwa na mkewe, hatak hata kuona h/gel hapo ndani kisa mke wangu anaweza kufanya vizuri zaid. tena huwa ni hodar sana wa kutoa mahitaj ya familia like shopping for food and other stuffs za ndani na hata kumvesha mkwe na watoto lkn huwa haudumii familia ya mke hata siku moja. na siku akitoa hela yyte kwenda ukwen basi ataihesabu for decades.
 
Yaani kama vile unawajua halafu huu anakufuja umuone kwamba hamna zaidi yake duniani lol,hivi inakuwaje
 
sikiliza dawa ya mwanaume kama huyu, unafungua akaunti kila pesa anayokuachia ya matumizi unapiga panga unaeka kwenye akaunti yako. bei za vitu unapandisha hata kwa 10%.

kila mara mwombe hela za kununua nguo, na unanunua zile za ukweli akirudi home kama vile ulitoka, hakikisha unasave usikose kueka akiba asiyoijua.

mimi nina experience na hawa wanaume wa aina hii tena. ukiona mtu anasema mimi sili chakula alichopika mtu baki jua ana lake jambo ama nguo yangu lazima afue mke wangu basi. huyu ni wivu tu utafikir yy ndo kaoa mwanamke mzuri sana kuliko wote dunian na ambaye anahisi muda wote watu watamuibia.

yaani huyu mlie timing tu zikikaa vizuri wewe unajitajirisha ukiwa humo ndani mwake. mwanamake anayeish na mwanaume wa aina hii asikubali kufujwa hata kidogo yaani apanie kuwa nyoko tu ndo maisha yataenda.
 
ni mambo ya kizamani sana hayo..maisha yamebadilika sana wakati huu, na ni lazima kwa watu kushirikiana na sio kwa mama kuwa tegemezi...wanaume wenye msimamo huo ni wazi kuwa bado hawajajanjaruka na uhitaji wa maisha ya sasa...
wapendwa hope wote ni wazima wa afya,nilisoma thread moja inayosema MATARAJIO YA MZAZI ANAPOSOMESHA MTOTO mletaji mada alikua akilalamika mama yake anataka hela nyingi hata kwa vitu visivyo vya muhimu kama kuchangia harusi ua jirani kisa anacheka naye vizuri ambayo stimes ni sawa pia ,swali langu linakuja je vip kwa mzazi utajisikiaje umemsomesha mwanao tena kwa kujinyima halafu leo anatokea mwanaume anamuoa binti yako hataki afanye kazi akae tu nyumbani amfulie na kumpikia na hata hela hela ya kununua sukari huipati je ni sawa Kwa ule msemo Mtu atamuacha wazazi na kuambatana na mume kwamba hahusiki na maisha ya wazazi au wadogo zake nawasilisha karibuni tujadili
 
Kama ni mimi mumewangu ananikataza nisifanye kazi, basi itabidi mimi na yeye tusign mkataba wa yeye kuwa mume na mwajiri wangu. Kama elimu yangu ni degree, atanilipa mshahara wa kiwango changu plus NSSF/PPF na PAYE ili asiikoseshe serikali mapato, Overtime e.t.c. na mkataba huu utasainiwa mbele ya mwanasheria. Kama hatoweza basi itabidi aniruhusu nifanye kazi na kuhusu kumpikia na kufua mbona simpo tu?
 
sikiliza dawa ya mwanaume kama huyu, unafungua akaunti kila pesa anayokuachia ya matumizi unapiga panga unaeka kwenye akaunti yako. bei za vitu unapandisha hata kwa 10%.

kila mara mwombe hela za kununua nguo, na unanunua zile za ukweli akirudi home kama vile ulitoka, hakikisha unasave usikose kueka akiba asiyoijua.

mimi nina experience na hawa wanaume wa aina hii tena. ukiona mtu anasema mimi sili chakula alichopika mtu baki jua ana lake jambo ama nguo yangu lazima afue mke wangu basi. huyu ni wivu tu utafikir yy ndo kaoa mwanamke mzuri sana kuliko wote dunian na ambaye anahisi muda wote watu watamuibia.

yaani huyu mlie timing tu zikikaa vizuri wewe unajitajirisha ukiwa humo ndani mwake. mwanamake anayeish na mwanaume wa aina hii asikubali kufujwa hata kidogo yaani apanie kuwa nyoko tu ndo maisha yataenda.

Wengine wabahili dada yangu we hujui tu ,anaacha hela ya chakula tu ambayo hata ukipiga panga haitoshi soda lol
 
Nyie KE acheni kujidanganyana. Ndoa ni maelewano ya watu wawili tu. Wakiingilia watu wengine tu basi ndoa inaanza kuwa chungu.

Ushauri:
Msiruhusu any person kuingilia maisha yenu na kutoa mifano ambayo haiwajengi.
Take it from me.
 
We mbona umekua mkali hivyo au we ndo nani ambaye hutaki mkeo ajishughulishe kisa unamtimizia kila kitu,hela ya kupew na ya kwako zina tofauti upo
 
:A S 465::A S 465: eeeeeh bhana eeeeh:nerd::nerd:

Wamekuwa mwili mmoja eeeh...!!!
 
Nyie KE acheni kujidanganyana. Ndoa ni maelewano ya watu wawili tu. Wakiingilia watu wengine tu basi ndoa inaanza kuwa chungu.

Ushauri:
Msiruhusu any person kuingilia maisha yenu na kutoa mifano ambayo haiwajengi.
Take it from me.

Mapweinti...!!
Hao wanaoacha kazi ni wake za majambazi nini..?
 
We mbona umekua mkali hivyo au we ndo nani ambaye hutaki mkeo ajishughulishe kisa unamtimizia kila kitu,hela ya kupew na ya kwako zina tofauti upo
Tatizo lenu mnawaza kuachwa kila wakati. Na mnawaza kujenga nyumbani kwenu. Kwani ukiacha kazi na ukajishughulisha shughuli ndogondogo sio bora?
Familia zetu ndio maana maadili yana potea siku baada ya siku kwa sababu hakuna mlezi.

Nyie wanawake every time mnawaza kushindana tuuu na mwanaume na sasa mnakimbia majukumu yenu.
Acheni kulishana sumu. Ndio maana hamuwezi kuolewa na mtakaa bila kuolewa milele.

Baba anarudi saa nne usiku na mama pia si ujinga huo. Eti mnasema haki sawa yaani baba akae nyumbani anyonyeshe mtoto mama ameenda kutafuta!?
 
Annael upo siriaz na unayoyaandika ama!??

Hivi kweli kumhudumia mzazi leo hii imekuwa ni UTU na sio WAJIBU!??????:baby:
 
Last edited by a moderator:
Annael upo siriaz na unayoyaandika ama!??

Hivi kweli kumhudumia mzazi leo hii imekuwa ni UTU na sio WAJIBU!??????:baby:

Umeweka maandiko ya kwenye biblia kumbe husomi biblia!?
Ni wapi kwenye maandiko ya biblia imeandikwa wewe unawajibu kwa mzazi wako?
Sikumbuki ni wapi kwenye biblia inaeleza Mzazi hunza akiba kwa ajili ya watoto wa mtoto wake na sio mtoto kuwajibika kwa mzazi.
Soma maandiko uyajue.
Ndio maana wengi wamepotoka hawataki kulifuata neno la Mungu na wala hawalisomi.
 
Masuala ya watu kwenye uhusiano wao hayawahusu watu wengine. Na mzazi anayemsomesha mtoto wake akitegemea kulipwa fadhira hiyo ni fikra potofu tena haifai. Kumtunza na kumsomesha mtoto ni wajibu wa mzazi lakini mtoto kumtunza mzazi wake ni utu na sio wajibu.

So kukubaliana mume na mke kuwa mke akae nyumbani inamaana yake. Tatizo hii dot com inawachanganya sana. Ndio maana watoto wanaozaliwa siku hizi ni wahuni hata kabla ya kuvunja ungo.

Mama mara zote ni mlezi wa familia na baba mara zote ni mlinzi wa familia.

Umenipata?

Hapo sikubaliani na wewe hata kidogo! Kwangu kumtunza mzazi/wazazi ni wajibu na wala si suala la utu tu.
 
Back
Top Bottom