Kwa mwenendo huu, anayemsifu Kikwete lazima anatetea maslahi binafsi siyo bure!!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu wanaJF,

Kwa jinsi serikali ya kikwete ilivyo legelege na inavyoongoza nchi hovyo hovyo, bado kuna watu wasio na haya wanaojitokeza hadharani na kumsifu. Binafsi nashawishika kuwaona watu hao kama wenye maslahi binafsi. Ukweli ni kwamba kikwete nchi imemshinda na Dunia ndivyo inavyomwona.
 
Kuna mwandishi alishasema "viongoziwa CCM wanahitaji ujasiri wa mwendawazimu kusimama mbele ya umati kuelezamafanikio, matarajio na kuomba umma kuunga mkono"

Kwa maana hiyo... "MTU ANAHITAJI UJASIRI WA MWENDAWAZIMU KUSIMAMA MBELE YA UMATI KUELEZA MAFANIKIO,NA MATARIJIO YA SHAROBARO WETU MKWELE"

Wote wanaomsifia kikwete na hawana maslahi binafsi na mfumo wa kifisadi unaoongozwa na kikwete lazima wana mtindio wa ubongo
 
Nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao, lakini Kikwete ni lulu iliyobaki ya Afrika. Tazama jinsi alivyotatua mgogoro wa Kenya na ule wa visiwa vya Comoro.
 
Nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao, lakini Kikwete ni lulu iliyobaki ya Afrika. Tazama jinsi alivyotatua mgogoro wa Kenya na ule wa visiwa vya Comoro.

Lulu ni kwako, kwa Watanzania Kikwete ni Janga la Taifa, ni bora kuongozwa na mtoto wa 3 kuliko Kikwete. Anashindwa kutatua matatizo ya ndani ataweza ya nje? Kwa wasio na upeo ndio watamuona Kikwete kwao kama ni mfalme kumbe ni kanyaboa
 
Nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao, lakini Kikwete ni lulu iliyobaki ya Afrika. Tazama jinsi alivyotatua mgogoro wa Kenya na ule wa visiwa vya Comoro.
kwi kwi kwi... umesahau na mgogoro wa Zanzibar Mkuu
 
Nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao, lakini Kikwete ni lulu iliyobaki ya Afrika. Tazama jinsi alivyotatua mgogoro wa Kenya na ule wa visiwa vya Comoro.
offcourrse hata nyie wakurya hamtamsahau alivyotawanya majeneza yenu kule north mara..hongereni sana
 
Mnaemponda Kikwete mna mawazo mgando au mna sababu zenu za siri kumponda. Nataka nianze na hoja moja moja kutoka katika yoyote kati yenu tuichambuwe halafu tuoine ukweli uko wapi. Wanaoponda hata aliyeanzisha mada kaonesha chuki binafsi na hakuna alipoonesha hata pamoja kuwa Kikwete hakufanya vyema tuianze hoja:
 
Nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao, lakini Kikwete ni lulu iliyobaki ya Afrika. Tazama jinsi alivyotatua mgogoro wa Kenya na ule wa visiwa vya Comoro.

Mgogoro wa Kenya umetatuliwa na Kofi Anna, Benjamin Mkapa na Graca Machel. Porojo zingine hazina mipaka.
 
Simu yangu haina opt. Ya ku-LIKE, dr. G umenena kweli tupu, rais anatakiwa awe na upeo mkubwa wa kuelewa na kuamua mambo, Huyu ****** hana hizo kwalitiz labda Angeenda Big brother huko angefaa sana.!
 
wewe kweli kwenye wendawazimu nawewe umo je?libya kuna kitu kasema,tunabidi tuwe wakweli siku zote maraisi wa afrika wengiwao niwake wa nchi za magharibi kasoro kidume kama gadafi mugabe tu.
 
je,unaweza kuelezea jamii kwanini kashindwa kusema chochote,kuhusiana na majeshi ya nato kuhivamia libya sema ukweli kuwa tanzania tumekosa kiongozi tumepata galasha tu kama uko dsm niambie uchumi wanchi unaweza kupanda bila viwanda kufanya kazi au siyo mtanzania ndiomaana unamsifia ujinga unaweza kwenda ukampa mtoto wamwenzio wakati wako anakufa njaa.nitaludi kupata upeo wawajinga wanao msifu kikwete.
 
Nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao, lakini Kikwete ni lulu iliyobaki ya Afrika. Tazama jinsi alivyotatua mgogoro wa Kenya na ule wa visiwa vya Comoro.

Kuwa "chizi" siyo lazima uokote makopo na vyakula vilivyooza jalalani.
 
Ndugu wanaJF, Kwa jinsi serikali ya kikwete ilivyo legelege na inavyoongoza nchi hovyo hovyo, bado kuna watu wasio na haya wanaojitokeza hadharani na kumsifu. Binafsi nashawishika kuwaona watu hao kama wenye maslahi binafsi. Ukweli ni kwamba kikwete nchi imemshinda na Dunia ndivyo inavyomwona.
GGL sio kweli kwamba kila anayemsifu JK ni kwa maslahi binafsi. Mimi naamini katika ukweli hivyo nitamsifu JK kwa mazuri yake na kumbonda kwa mabaya yake. Pamoja na matatizo lukuki yanalolikabili taifa letu, sio kweli kuwa JK na serikali yake hawajafanya jema lolote kwa nchi hii. Yako mema mengi tuu wamefanya na yanastahili pongezi. Mfano ni UDOM na Mchakato wa Katiba Mpya. Hata kama ni kwa shinikizo au mambo fulani ni sera ya chama fulani, aliyefanya ni yeye na anastahili pongezi. Kwa kusema haya lazima pia ni declare may interest kuwa nimesifu huku I stand to gain nothing toka kwa JK zaidi ya kuwa ndiye rais wetu. Pamoja na kumsifu lakini kwenye hili la umeme, amefanya madudu makubwa.
 
Back
Top Bottom