Kwa mwana JF mwenzetu FORGIVE na wengine wenye matatizo kama yake

Tatizo lako hunishirikishi komredi,

Samahani sana Komredi wangu, next time utapata FULL CO-OPERATION
Niliguswa sana na tukio la huyu binti, ikanibidi niilazimishe CPU ifanye MAXIMUM PROCESSING yenye EXTREME SPEED then inipe jibu kamili la tatizo la huyu mdada
 
na moto wa madhabahu ya mbinguni ukapate kushuka na kuteketeza mipango yote ya ibilisi juu ya binti huyu, damu ya Yesu ikafanyike kuwa uzio katika maisha yake.....Amen
 
na moto wa madhabahu ya mbinguni ukapate kushuka na kuteketeza mipango yote ya ibilisi juu ya binti huyu, damu ya Yesu ikafanyike kuwa uzio katika maisha yake.....Amen
Naomba nikusalimu mpendwa! Vibaya hivyo unavyonitenga!
 
CPU... hili ombi ni zito sana, nakuunga mkono na sisi husema "twakuomba utusikie"

hebu tupe baCKGROUND KIDOGO ILIKUAJE HADI UKACHUKUA HATUA HII YA KUMUOMMBEA FORGIVE?
 
Huyu Forgive kafanya nini maana sioni sababu za kuombewa huo msamaha ikiwa yeye mwenyewe hajakubali. Na ni vyema aombe mwenyewe kwa Mungu wake.

Samahani kama nimewakera.
 
Naomba nikusalimu mpendwa! Vibaya hivyo unavyonitenga!

mpendwa ubarikiwe sana.....nashangaa sana umekuja kupotelea wapi....sielewi....lakini tuombe muda wa bwana ufike ili tuweze kusakata twist tena
 
Huyu Forgive kafanya nini maana sioni sababu za kuombewa huo msamaha ikiwa yeye mwenyewe hajakubali. Na ni vyema aombe mwenyewe kwa Mungu wake.

Samahani kama nimewakera.

Bila shaka hujui kinachoendelea, ungeuliza ufahamishwe
 
Ndugu wana JF, heshima mbele.
Napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema na Rehema zake kwangu mpaka sasa.
Nimekuwa nikisikitishwa sana mpaka nashindwa hata kutoa mchango wa kimawazo kwa wana JF wenzetu walikumbwa na mikasa mbalimbali ya kusikitisha na ya kutisha kama huyu mwenzetu FORGIVE. Naomba sana waupokee huu msaada wangu kwao. Ingawaje nimetumia jina la Forgive ktk huu msaada wangu (tukio lake ndio msukumo mkuu) naomba msaada huu uwafikie wote wenye matatizo kama yake


Katika jina kuu linalotikisa falme na mamlaka la Bwana wetu Kristo wa Nazareth, katika jina litendalo maajabu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi, Baba wa Mbinguni, Ninaita uwepo wako mahali hapa, ninaita uwepo wa Bwana.

Asante Mungu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu kumsaidia huyu binti FORGIVE katika vita hivi. Baba vita si vya kwake bali ni kwa Roho yako utampigania huyu binti katika jina la Yesu
Baba ninakushukuru kwa kuwa upo pamoja nae kwa ajili ya kumtia nguvu, kumsaidia, kumshika na kuwa na Mungu wake, moyo wake utiwe nguvu, katika vita hii katika jina la Yesu.

Roho Mtakatifu ninaomba uwe pamoja na huyu binti FORGIVE katika vita dhidi ya shetani na wajumbe wake. Roho Mtakatifu wewe ni mfariji wake. Pigana vita hivi kwa ajili yake na umfariji katika jina la Yesu. Siwezi kuomba kama vile uombavyo wewe. Nakusihi sema sasa ukitumie kinywa chake katika Jina la Yesu. Roho Mtakatifu nakuomba umuongoze na umlinde, umfundishe jinsi ya kuomba atumie kama shoka lako katika vita hivi, dhidi ya shetani na wajumbe wake. Roho Mtakatifu wewe ni mfariji wake.

Katika jina lenye nguvu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi. Ninaruhusu malaika wa vita kutoka ufalme wa Mungu sambaeni kila mahali sasa, mjieneze katika Anga, Nchi na Bahari, muangamize nguvu zote za giza na mumpige shetani bila kukoma, haribuni mipango yote waliyoifanya dhidi ya huyu binti FORGIVE. Ninawamuru enyi malaika na Bwana wamzunguke kama wigo sasa

Ninamfunika kwa damu ya Yesu Kristo. Ninawaloweka watu wa familia yake, ndugu zake, nyumba yake, ofisi yake, chakila chake, fedha zake, rafiki zake, majirani zake, n.k katika damu yenye nguvu ya Yesu Kristo wa Nazareth. Ninalifunika anga lote, nchi yote na bahari yote kwa damu ya Yesu Kristo;

Wewe Shetani, imeandikwa katika Ufunuo 12: 11 ''Nao wakamshinda shetani kwa damu ya Mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wao '' nimetumia damu ya Yesu kukushinda sasa na hata milele katika jina la Yesu!

Ninakemea, na kufunga na kuharibu mapepo yote yanayozuia ukombozi wake na mafanikio yake. Ninaharibu kazi zenu dhidi ya maisha yake, ninawatupa wote katika giza la milele na kamwe msiweze kuinuka tena hata siku ya hukumu ya Bwana. Ninawatumia moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote
Ninaharibu kila kifuniko, minyororo, mafundo na uchawi dhidi yake. Ninauamuru moto wa Roho Mtakatifu kuviteketeza vyote na kuvifanya majivu kabisa. Ninauzimisha moshi wangu shetani dhidi ya maombi yangu. Ninatumia damu ya Yesu kuviharibu vyote, katika jina la Yesu

Wewe Shetani, imeandikwa katika kitabu cha LUKA 1:13 kusema ''Hakuna lisilo wezekana kwa Mungu”
Katika Jina la Yesu ninavunja nguvu zote za giza zilizomfunga. Ninamuweka huru kutoka kwenye nguvu za giza. Ninamuweka huru kutoka kwenye vifungo vya Uchawi, Waume wa Kipepo, Watoto wa kipepo, Makazi ya kipepo, Mali za Kipepo, Mapepo ya kurithi, Majini Bahari, Maruhani, Misukule na Mizimu, Subians, Maruani, Zakuani.nk.
Baba wa Mbinguni, ninajishusha na kumtenganisha na laana zote, maagano, mazindiko n.k aliyofanyiwa awe huru sasa, hivyo anayo haki ya kuchagua atakayemtumikia. Hakika atachagua kumtumikia Baba wa mbinguni, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Awe kiumbe kipya na mpya kila siku ya maisha yake. Roho Mtakatifu yu juu yake sasa.

Atayaweza mambo yote katika Yesu Kristo amtiaye nguvu (Fil 4:13).
Neno la Mungu linasema kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa (Mathayo. 12:37)

Baba mfanye kuwa na haki kwa maneno ya kinywa chake kwa kuwa uzima na mauti vimo katika uwezo wa ulimi (Mithali 10:21).

Basi mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli (Yohana. 8:36)

Kamwe hatateswa tena na Shetani pamoja na wajumbe wake kwa maana tayari yuko huru sasa, katika jina la Yesu Kristo. Amen.

eimen
 
Mkuu CPU umefanya njema sana,mbali ya forgive ni kweli kuna wengine kama yeye na hata zaidi yake hapa ila hawajaweka tu wazi.Mungu aliyekuongoza kuandika sala hii atatenda.Ubarikiwe sana mkuu
 
Du!
Yaani nilikuwa sijafika mitaa hii muda kidogo sasa naingia tu na thread ya kwanza nakutana na CPU inatema ombi zito likanishutua kama yale mabomu ya Gombs. Jamani nijuzeni huyo FORGIVE alikuwa na shida gani, ili hata nijue hilo bonge la maombi lilikuwa ni kwa ajili gani
 
CPU... hili ombi ni zito sana, nakuunga mkono na sisi husema "twakuomba utusikie"

hebu tupe baCKGROUND KIDOGO ILIKUAJE HADI UKACHUKUA HATUA HII YA KUMUOMMBEA FORGIVE?

Huyu Forgive kafanya nini maana sioni sababu za kuombewa huo msamaha ikiwa yeye mwenyewe hajakubali. Na ni vyema aombe mwenyewe kwa Mungu wake.

Samahani kama nimewakera.

Du!
Yaani nilikuwa sijafika mitaa hii muda kidogo sasa naingia tu na thread ya kwanza nakutana na CPU inatema ombi zito likanishutua kama yale mabomu ya Gombs. Jamani nijuzeni huyo FORGIVE alikuwa na shida gani, ili hata nijue hilo bonge la maombi lilikuwa ni kwa ajili gani

Wakuu Gurudumu, bitimkongwe, Janjaweed na wengine ambao hawafahamu

Ni kwamba (Nitaeleza kwa kifupi) huyu binti forgive (25yrs now) aliweka post yake hapa jamvini MMU akiomba apewe msaada ya kimawazo.
Alieleza kwamba aliwahi kubakwa mara mbili ktk kipindi cha miaka 7 iliyopita na watu wawili, mmoja akiwa ni mtu mwenye nyazifa kubwa na mzito kimadaraka (hakumtaja ni nani wala cheo chake). Baada ya kufanyiwa vitendo hivyo vichafu na vya kutisha na hao mashetani, alienda hospital na kugundulika ana mimba ambayo hata hivyo baadaye iligungulika imeharibika na then akapoteza kabisa na uwezo wa kushika mimba tena.

Baada ya matukio hayo akaja kupata kijana ambaye walipendana kwa dhati, akampa masharti ya kutofanya nae mapenzi kwa kuwa hakuwa sawa kiafya. Lakin kila wakiwa pamoja faragha kijana akianza kumpapasa binti, basi binti anaanza kukumbuka yote alivyofanyiwa huko nyuma na anaanza kutetemeka. Mpaka sasa anasema bado hajamwambia huyo kijana kuhusu maisha yake na wala hajaenda hospital kupima kama ameambukizwa virusi au la.

Sasa anauliza amwambie ukweli huyo kijana au la. Na akaomba msaada wowote wa kimawazo.

Wakuu wenzangu tuliosoma ule ujumbe wake, kama kuna sehemu nimekosea ktk maelezo haya tuwekane sawa
 
Back
Top Bottom