Kwa Mtazamo wako Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Je Imetatua tatizo la Ajira Tanzania?

Fredrick Nexus

New Member
Oct 8, 2012
2
0
Kwa upeo wangu mdogo, nadhani kwa kuwa serikali ilifikiri kwa kina au ilikopi na kupest mfumo huu toka nchi nyingine na kujaribu ufanyia kazi utakuwa sio mfumo sahihi, huwezi ita watu 140 kwa post 1 hata kama mnataka ushindani si kiivyo ukizingatia haitoi huduma ya wanaokwenda katika interview,Bora wangeurudisha utaratibu ule ule wa zamani wa kuajiri toka wilayani na mikoani.
 
mkuu mi sioni tatizo la kuita watu wengi, wape nafasi mwenye uwezo apite.

Kuhusu kutatua tatizo la ajira, huwezi kulitatua bila kutengeneza ajira mpya au kuwawezesha watu kujiajiri.
Sekretariet haitengenezi ajira mpya wala haiwezeshe watu kujiajiri, inachofanya ni kuratibu utaratibu wa kuajiri watumishi serekalini.

Ili tutatue tatizo la ajira lazima tuwekeze zaidi kwenye kilimo na tufufue viwanda vilivyokufa na kujenga vipya na sio kuwaachia wawekezaji pekee.
Bila hivyo tatizo litazidi kuongezeka.
 
Kama alivyosema Peri,Sekretariet ya Ajira haikuja kutatua tatizo la ajira bali kueatibu watumishi wa Serikali wanavyoajiriwa.
 
Back
Top Bottom